Mwananchi wajibu Mapigo ya Mengi

Mwananchi wajibu Mapigo ya Mengi

Joined
May 6, 2009
Posts
19
Reaction score
8
Mwananchi Communications Ltd inayomilikiwa na kampuni ya Nation Media Group Ltd ya Kenya imemteua Muhariri wa Habari wa Nipashe, Deniss Msacky kuwa Naibu Mhariri Mkuu wa Gazeti La Mwananchi.

Bwana Msacky aliyejiuzulu ghafla anafasi ya uhariri wa uhabari katika gazeti la Nipashe mwezi huu, ataanza rasmi kazi mweizi ujao. Hatua hiyo imeelezwa na vigogo wa ndani ya Mwananchi kuwa ni kujibu mapigo ya Bwana Reginald Mengi yaliyofanywa mwaka jana kwa kunyakua zaidi ya waandishi waandamizi kumi kwa dau kubwa.

Mwananchi Communications wataendelea kuchota wale waliotajwa kuwa watu hao asilia ambao kwa sasa wako njia panda baada ya kuondoka Sakina Datto aliyehamishiwa This Day.

Awali kulikuwa na tetesi kwamba Msacky alikuwa anakwenda ikulu katika kitengo cha mawasiliano. Lakini kwa mujibu wa barua ya ajira ambayo nimefanikiwa kuiona hii leo asubuhi, Bwana Msacky amerudi nyumbani alikokuwa kwa kupanda cheo na ni mmoja wa washirika wa karibu wa Bwana Theophil Makunga, Mhaariri Mtendaji wa gazeti hilo makini.
 
Lets be realistic kama Mengi alichota 10 toka Mwananchi na ni mmoja tuu ndiye amerudi kundini, headline haisemi kweli. Kujibu mapigo ni kama Mwananchi nayo ingetoa pigo kwa IPP Media, hivyo hakuna pigo lililojibiwa labda ungesema Mwananchi yamkomboa mmoja kati ya wana wapotevu 10!

Baadhi ya waandishi ninawaheshimu sana na siamini huwa wanahama kwa sababu ya maslahi bora, ila naamini waandishi wote wa vyombo vya Mangi lazima wasimame kwa machale mguu ndani mguu nje ili wasianguke.
 
Back
Top Bottom