Now lipo on line,,, but naona ka linapungua ubora, vile sijajua Mwanahalisi hatma yao ni nini.
Kweli kabisa usemavyo. Hem linganisha hizo blue mbili hapo chini na ndio utaona ubabaishaji uliopo
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Cheka atakiwa kupunguza uzito
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]
Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]
Tuesday, 18 September 2012 13:18
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Imani Makongoro
BONDIA Francis 'SMG' Cheka atalazimika kupunguza uzito wa kilo moja kabla ya pambano lake la kuwania ubingwa wa kimataifa wa mkanda wa UBO dhidi ya Karama 'Captain' Nyilawila
litakalofanyika Septemba 2 kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Cheka anapaswa kupunguza uzito huo ili kufikia uzani wa super middle kg 76 anaopigania katika pambano hilo la raundi 12 dhidi ya Nyilawila, litakalosimamiwa na chama cha ndondi cha PST.
Kocha wa bondia huyo, Abdallah 'Comando' Salehe aliliambia gazeti hili wakati wa mazoezi ya bondia huyo kwenye uwanja wa Gymkhana kwamba Cheka ameongezeka uzito kidogo.
"Cheka anapigana uzani wa kg 76, lakini sasa ana kg 77, nategemea katika mazoezi yake haya anatakiwa kupunguza kilo hiyo moja kwa haraka," alisema kocha huyo.
Saleh alisema hivi sasa bondia huyo yuko katika hatua za mwisho mwisho za mazoezi tayari kumkabili Nyilawila na kusisitiza kwamba 'iwe usiku ama mchana'Cheka lazima achukue mkanda huo.
"Tayari bondia wangu anarekodi ya kumkung'uta Nyilawila, naamini ataendeleza rekodi yake hiyo kwa kuwapa mashabiki wake zawadi ya kufunga mwaka ya kutwaa mkanda huo," alisema kocha huyo.
Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]