Katika Mjadala wa wazi Kati ya Viongozi wa Dini na Wananchi kuhusu Amani na yaliyotokea Oktoba 29, 2025 unaoendelea leo Machi 18, 2026 Arusha kwenye ukumbi wa Centre house, kijana mmoja amehoji uwazi wa kuzungumza akielezea changamoto aliyopata kutafutwa baada ya kutoa kauli Oktoba 22, 2025 " Nilisema kuelekea uchaguzi mkuu inabidi tutende haki ili amani iendelee kuwepo, tusiendelee kuimba wimbo wa amani pasipo kutenda haki".
Anaeleza baada ya kutoa kauli hiyo clip ilisambaa mitandaoni hali iliyopelekea yeye kutafutwa sana kazini kwake, anaposhi hadi kwa wazazi wake na kumpelekea kwenda uhamishoni zaidi ya wiki tatu, baadaye ilimbidi akaripoti Polisi na kuhusihwa katika tuhuma za kuhamisha maandamano lakini aliponya kwa sababu alishiriki kwenye kupiga kura.
Amehoji "Kama tuna uwazi wa kuzungumza alafu baadaye tunakutana na changamoto, je tuendelee kuamini vijana wataendelea kuzumgumza kwa uwazi au watakua waoga?