Mwananchi: Ni Mzee Pinda Ameyasema Haya?

FDR Jr

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
249
8
Habari za kawaida
Posted Date::4/10/2008
Utajiri wa mafisadi kikwazo kushitakiwa

* Waziri Mkuu asema uwezo wao kifedha unaiogopesha serikali

*Wahusika wa Richmond kuchukuliwa hatua za kinidhamu tu

*Asema kuna upungufu mkubwa ofisi ya Mwanyika

*Serikali yazikataa mvua za Lowassa

Na Michael Uledi, Dodoma


SERIKALI imesema utajiri wa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni moja ya kikwazo cha kuwafikisha mahakamani kwa pupa.



Kauli hiyo ya serikali inayoonyesha kuwa, watuhumiwa wa EPA ni vigogo na watu wenye mtandao mpana ndani na nje ya serikali, imetolewa mjini hapa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akizungumza na waandishi wa habari.


Awali, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, ambaye ni mjumbe wa Timu ya Rais (Task Force) ya kuchunguza kukamata na kuchukua hatua za kisheria, aliwafananisha mafisadi wa EPA sawa na magaidi ambao wakifuatwa kwa pupa wanaweza kuilipua nchi.


Hata hivyo, Pinda ambaye amezungumzia suala hilo kwa mara ya kwanza tangu awe Waziri Mkuu, alisema bado serikali inaweza kutumia ushahidi wa fedha zinazorudishwa na baadhi ya

makampuni yaliyochota fedha kutoka EPA, kama ushahidi wa kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafungulia kesi za jinai mahakamani.


Pinda ambaye aliamua kuitisha mkutano huo na waandishi na kuwapa fursa waandishi waulize maswali bila yeye kuzungumza, alisema watu waliohusika na uchukuaji zaidi ya Sh133 bilioni lazima watakuwa ni vigogo, hivyo iwapo watapelekwa mahakamani

bila umakini wanaweza kuitia hasara zaidi serikali kutokana na uwezekano mkubwa wa kuweza kushinda kesi na fedha zisirudi.


Alisema kutokana na hali hiyo njia inayotumika na Kamati inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, ndiyo mwafaka katika kulishughulikia suala hilo ambalo kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa fedha zinarejeshwa na kisha ikilazimu zitumike kama ushahidi mahakamani.



Pinda aliyekuwa akitimiza siku 60 tangu ateuliwe na kuthibitishwa kushika wadhifha huo, alisema kamati inayoongozwa na Mwanyika itaendelea kufanya uchunguzi juu ya ukiukwaji wa taratibu katika uchukuaji wa fedha za EPA na kwamba hakuna sababu

ya kamati hiyo kuingiliwa na watu wengine kwa sasa.


Katika kuhakikisha kunakuwa na mafanikio katika suala hilo ambalo limeifanya serikali kuanza kupoteza imani yake kwa wananchi, alisema ni kuhakikisha kuwa kila jambo linafanyika kwa uangalifu ambapo kamati husika inatakiwa kuwa na uwezo wa kuchunguza kwa umakini na kisha kupatikana ufumbuzi wa suala hilo.



?Watu waliochukua fedha zaidi ya Sh46 bilioni ukiwapeleka mahakamani wanaweza kushinda kesi na hivyo hata fedha zisirudi, kwa maoni yangu naona njia inayotumika hivi sasa ni njia bora na inayowezesha kufanikisha mkakati huo wa kurudisha fedha hizo. Kama kuna umuhimu wa kwenda mahakamani fedha hizo zinaweza

kutumika kama ushahidi, ?alisema.


Hata hivyo, Pinda aliweka bayana awali kwamba hakuwa na uhakika kama majibu yake yangeweza kuwa mazuri kwa umma kutokana na unyeti wa suala lenyewe.


Alisema kamati ya Rais ina uwezo wa kueleza hatua kwa hatua juu ya hali ilivyo kuhusiana na suala hilo na amekemea kusijetokea viongozi wasiokuwa katika kamati hiyo, na kuanza kuingilia uchunguzi, jambo linaloweza kuharibu mustakabali wa kazi hiyo.


Juu ya kutaja wahusika wa wizi wa fedha hizo za walipakodi, Pinda alisema ni suala gumu kuwataja waliorudisha kwa kile alichodai kunaweza kuharibu uchunguzi


Alisema imani yake ni kuwa Watanzania wote akiwamo yeye, wana shauku ya kuwajua watu wote waliohusika katika wizi huo uliolitia hasara kubwa taifa, jambo ambalo likiunganishwa na misukosuko ya Kampuni ya kufua umeme ya Richmond lilishaanza kupunguza imani ya wananchi kwa serikali.


Waziri Mkuu, alisema uchunguzi utakapokamilika serikali itachukua hatua mbalimbali kwa watu waliohusika ikiwa ni pamoja na watumishi wa umma waliojihusisha na ufisadi huo katika maeneo yao ya kazi.


Kuhusu Richmond, alisema Tume ya Serikali ya kupitia mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu uchunguzi wa mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura Kampuni ya Richmond imemaliza kazi, lakini watumishi waliozembea hawatashitakiwa.


Kauli hiyo ya serikali imemaliza kile ambacho watu walikifikiri kwamba kungekuwa na uwezekano wa kuwafikisha mahakamani watumishi hao waliozembea hadi kutiwa saini mkataba huo.


Uamuzi huo wa serikali kuachana na mpango wa kushitaki watumishi wake, unatokana na ugumu wa ushahidi mahakamani kuthibitisha tuhuma hizo za uzembe wakati mchakato

ulifanyika katika vikao mbalimbali vya Timu ya Majadiliano ya Serikali (GNT).


Pinda ambaye anakabiliwa na mtihani mzito na wa kwanza katika mkutano huu wa 11 wa Bunge wa kuitetea na kutoa ufafanuzi wa mambo ya serikali bungeni, alisema Kamati yake ndogo (Task Force) ya wataalamu iliyopewa kazi ya kufanyia kazi

mapendekezo ya Kamati ya Mwakyembe (Dk Harrison-Mbunge wa Kyela), imekamilisha kazi.


Kwa mujibu wa Pinda, iwapo Spika atampa fursa katika mkutano huo atatoa taarifa kuhusiana na hatua zilizochukuliwa na zile zitakazochukuliwa siku za usoni dhidi ya wahusika.


Waziri Mkuu alisema iwapo hakutakuwa na nafasi katika mkutano ni imani yake suala hilo linaweza kushughulikiwa katika mkutano wa Bunge ujao wa Juni.


Alionya kuwa, serikali haitakuwa na subira na wale wote watakaothibitika kuwa walisababisha hasara kwa taifa kwa namna moja au nyingine, na kuongeza kwamba serikali itawawajibisha kwa mujibu wa taratibu za kiutawala ili kuepuka uwezekano wa serikali kushitakiwa na kushindwa kesi.


Hata hivyo, alisema kuwa baada ya kamati yake kupitia mapendekezo ya hiyo Kamati Teule, imebainika kuwepo mapungufu ambayo ni pamoja na kuwapo uwezo mdogo wa kiutaalamu katika nyanja ya majadiliano ya mikataba kwa watumishi wa umma , hususan kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.



Alisema uwezo huo mdogo wa wataalamu umewafanya kushindwa kuzingatia maslahi ya Taifa na kuongeza kwamba, kasoro nyingine ni pamoja na matatizo ya usimamizi wa manunuzi

ambapo Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), bado haijawa huru kutokana na kufanya kazi zake chini ya Wizara ya Fedha tofauti na kama ilivyo Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).


Sanjari na hilo kasoro nyingine ambayo imebainika ni pamoja na kukosekana kwa taratibu bayana za uwajibishaji wa watumishi wa umma na viongozi wa kisiasa, na kuongeza sakata la Richmond limedhihirisha kuwa suala la maadili kwa watumishi na viongozi halijapewa kipaumbele katika masuala ya kitaifa.


Kuhusu mapendekezo ya wabunge wakati wa mkutano wa Bunge uliopita kutaka wahusika wa sakata la Richmond wafilisiwe, Waziri Mkuu, alisema hata kama ingebidi kufilisi mtu si jambo rahisi ni muhimu kwenda mahakamani.


Wakati huo; Waziri Mkuu amesema mradi wa mvua ya Thailand maarufu kama mvua ya Lowassa, umeshindikana kutokana na gharama kubwa.


Alisema utatifi kuhusiana na mvua hizo, ungeligharimu serikali zaidi ya Sh15bilioni, kiasi ambacho alisema ni kikubwa.


Taarifa za mvua hizo, zilikuja baada ya aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa kutembelea nchini humo na kukutana na wataalamu waliomuahidi kuja kutengeneza mvua hizo nchini, ili kukabiliana na ukame katika mabwawa yanayozalisha umeme, likiwamo la Mtera na Kidatu, ambayo yalikauka maji na kusababisha kuwapo kwa mgao wa umeme.
 
Back
Top Bottom