Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 638
- 1,038
Katika harakati za maisha ya kila siku, tunashuhudia tabia ambazo, kwa kiasi kikubwa, zinaashiria kupungua kwa maadili, nidhamu, na staha ndani ya jamii yetu.
Sio kila jambo linahitaji sheria kali. Baadhi ya mambo yanahitaji tu busara, utu na heshima ya msingi. Ustaarabu ni namna mtu anavyoishi na watu , si kwa nguvu wala kwa maneno makali, bali kwa hekima, utu, na ukomavu wa fikra.
Yafuatayo ni mambo yanayoonesha kukosekana kwa ustaarabu!.,katika maisha yetu ya kila siku….
Mtu hujijenga kwa busara yake, lakini hujibomoa kwa matendo yake.Ustaarabu hauhitaji pesa , unahitaji utu.
Ustaarabu hauanzi kwa sheria, huanza na moyo wa kujiheshimu na kuwaheshimu wengine. Kama kila mmoja wetu ataamua kuishi kwa staha, busara, na nidhamu ya ndani , basi jamii yetu itasonga mbele kwa heshima na hadhi inayostahili.
-Chavalikungu.!

- Mtu anaongea kwa nguvu kwenye simu ndani ya daladala iliyojaa watu, hadi abiria wenzake wanajua kila undani wa maisha yake , kutoka A hadi Z. Hii si tu kero, bali ni kukosekana kwa staha na busara ya mawasiliano hadharani.
- Dereva wa daladala anakula miwa huku anaendesha, akitupa maganda nje ya dirisha. Huu ni uzembe, ni hatari, na ni kielelezo cha kutowajali watu wengine na mazingira.
- Watu wanakula ndani ya daladala, wengine hata vyakula vyenye harufu kali, bila kujali abiria waliowazunguka.
- Wengine wanatembea mitaani huku wanakula, bila kuzingatia hadhi ya maeneo ya umma.
- Kushusha vioo vya magari na kutupa taka barabarani, kana kwamba barabara ni jaa la mtu binafsi.