Mwananchi: Azam yapeta, Simba yala kichapo Angola

Mwananchi: Azam yapeta, Simba yala kichapo Angola

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Azam imesonga mbele Kombe la Shirikisho kwa kuichapa Al Nasri kwa mabao 5-0, huku Simba na Jamhuri ya Pemba zikiogelea vipigo visivyoweza kusahaulika katika michuano ya katika Ligi ya Mabingwa.

Mabingwa wa Tanzania, Simba walikubali kipigo mabao 4-0 kutoka kwa Libolo FC ya Angola, huku Jamhuri ikinyukwa kwa mabao 5-0 na St Geogre ya Ethiopia.

Juba, Mshambuliaji Khamis Mcha alifunga mabao matatu na kuiongoza Azam kuichapa Al Nasri 5-0 na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 6-1, baada ya mchezo wa kwanza Dar es Salaam kushinda 3-1.
Katika mchezo huo Azam walicheza kwa kujiamia, huku kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Tchetche akitengeneza mabao yote ya matajiri wa Chamazi katika dakika za 23, 31 kwa magoli ya Mcha na John Bocco bao dakika 49.
Bocco alitegeneza bao la nne baada ya kuwatoka beki wa Al Nasri na kupitisha krosi nzuri kwa Abubakar Salum 'Sure Boy' aliyeumalizia mpira huo wavuni.
Jahazi la wenyeji Al Nasri lilizidi kuzama katika dakika ya 74, baada ya Mcha kumnyang'anya mpira beki Ladol Manasa na kumchambua kipa kuipa Azam bao la tano. Mcha alifunga bao lake la tatu katika dakika 74.
Luanda, Safari ya Simba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa ilishia mjini Calulu Angola baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Libolo.
Wenyeji waliutumia vizuri uwanja wao baada ya kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika 8 kupitia winga wao Vado aliyeunganisha vizuri krosi beki wa kushoto Ari.
Katika mchezo huo kocha wa Simba, Patrick Liewig aliwaweka benchi Mrisho Ngasa, na Mwinyi Kazimoto na kuwaanzisha chipukizi Abdala Seseme na Haruna Chanongo.
Chipukizi hao walishindwa kuhimili kasi ya viungo wa Libolo iliyoongozwa na Ruben nyota wa zamani ya Braga ya Ureno pamoja na Manu Lopesa na Sidnei.
Mfaransa Liewig aliwaingia Ngassa na Kazimoto kipindi cha pili na dakika ya 62, krosi nzuri ya Ngassa ilitua kichwani kwa Felix Sunzu lakini kichwa chake hakikueleka golini.
Libolo waliamka na dakika 80, Rasca alifunga bao la pili akiunganisha krosi ya Vado na dakika mbili baada Reuben alifunga bao la tatu kwa shuti la mita 25, lilomshinda kipa Dhaira na kujaa wavuni.
Vado alihitimisha karamu hiyo ya mabao ya Libolo kwa kupachika bao la nne akimalizia mpira uliomtoka mkononi kipa Dhaira alipojaribu kuzuia krosi ya Dario.
Akizungumzia matokeo hayo kocha Liewig alisema: "Tumepoteza umakini wakati tulipokuwa tukisaka bao la kusawazisha."
"Mabeki walifanya uzembe mkubwa na kupoteza mipira mingi bila ya sababu," alisema
Wakati huohuo, Jamhuri ya Pemba ilikubali kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Georgena kuondolewa mashindano kwa jumla ya mabao 8-0 baada ya kufungwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza.


By:Mwananchi: mwanzo - Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza
 
Naona aibu na kununa nimenuna wakuu.
 
Back
Top Bottom