Kiukweli dada yangu huyu hivi sasa ni kama kachanganyikiwa hivi na muziki ni kama unamshinda sasa
Alilalamika bongo fleva. Hailipi akakimpilia gospel, kufika huko kitu cha kwanza tu kakimbila studio na kuanza kuomba kolabo na magwiji wa gospel akina Rose muhamdo Christina shushi Ben Mwaitege nk
Wakamchomolea kwa mantiki ya kwamba wanahitaji kumjua zaidi kafuata wokovu kweli au kaja tu kupiga hela kwenye gospel?
Basi alivyoona hivyo karudi tena kwenye media na kusema muziki wa gospel sasa basi sababu wasanii hawampi ushirikiano, kila akiomba kolabo wanamchomolea
Akarudi tena rasmi kwenye bongofleva ambayo kiukweli imekuwa ngumu kwake kukabili changamoto za wanachotaka wapenzi wa sasa wa muziki huo ambao vitorondo ndio habari ya mujini