Mwanamke wa sasa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke wa sasa!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bazazi, Oct 5, 2012.

 1. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,030
  Likes Received: 564
  Trophy Points: 280

  Wazo letu la sasa juu ya wanawake ni kuwa mtaalamu, mtemedeni, mrembo na maridadi. Hukaidi ukubwa na utawala wa mwanaume katika mambo yote ya maisha. Hushindana na mwanaume kwa ajili ya uhuru wa maslahi na uchumi. Kinyume cha mwanamke wa zamani aliyekuwa mtumwa na mtumishi wa kazi ngumu kama kibarua. Mwanamke wa zamani alionekana mchana na usiku nyumbani na jikoni, kuzaa na kulea umati wa watoto, na mwenye lazima ya kufanya kazi ya kuangalia faraja ya bwana: mume wake.


  Walakini mambo yamebadilika sasa. Kazi ya mwanamke sio utii. Hutaka usawa wa cheo na wa haki. Mwanamke wa sasa ni asi. Si vibaya kwa kadri mambo yaendeleavyo, lakini kujichukulia kibubusa – kama kipofu – kila litendwalo na mwanaume ili kuonyesha ulimwengu kuwa ana usawa ni upuzi pengine. Wanawake wameanza kuvuta sigara kwa sababu wanaume wanavuta. Huvaa suruali na mashati kwa sababu wanaume huvaa. Matokeo yake ni fujo kubwa. Hujui nani mwanaume au nani mwanamke!


  Mipaka ya nguvu za mwanamke, hali hafifu, kuchoka upesi na moyo dhaifu humfanya hafai kwa kazi ngumu. Mwanamke ni malaika wa roho. Na apate usawa wa haki na wa cheo, lakini daraka lake katika maisha ni la Mapenzi, Huruma, Sanaa na hifadhi.
  NB

  1. mtemedeni = aliyestaarabika, aliyeendelea
  2. asi = kutotii
  3. kibubusa = kipumbavu, kipofu, kama kipofu.


  Shaaban Robert (1967). Diwani ya Shaaban 5: Insha na Mashairi. Thomas Nelson and Sons Ltd. Dar es Salaam. 105pp.
   
 2. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,123
  Trophy Points: 280
  Hahahaaaaaaa! Bazazi kwanza nikupongeze kwa LUGHA SAFIII ULIYOTUMIA (NAMASHAKA UMECHAKACHUA NA KAMUSI PEMBENI) Ila kwa unadhifu wako na ufasahaa naomba nikupongeze kwa KAHAWA NA KASHATA KAMA KIBURUDISHO CHETU ASILI CHA WATU WA PWANI!!!!

  Back to topic!!!! Napingana na wewe 100% sibishii msuli, ila nabishia logic!

  1. Zamani MWANAMKE PAMBO TU YEYE NA KULETEWA TUU (GOAL KEEPER) ndo maana alishinda jikoni sababu alijua KATU JIKO HALITANUNA yakheeeee! Ila hizi zama za kina Kibelaaaaaa! Hamueleweki atiii! Ukijifanya Goalkeeper mbona utadaka nyavuuu! Hali yatufanya tutafute position maishani, Wajikuta mchezeshaji kiungo ili mambo ya balance, wengine wanaojasiria miili, wameamua kuwa MASTRAIKA atiii! Nyumbani tumemuachia Dada kama Beki tatu kuweka ulinzi golini!

  2. Sasa kama na mie FIGHTER basi haki ziongezekeee! Na mie niafaidi jasho langu! Twarudi wote saa 1 usiku wewe umetoka Bank mie Skuliii kufundisha, Wote tumeingiza siku atiii, afu wataka nianze kuwasha mkaa we umeketi wasoma zako gazeti? La hashaaa! Katu haikubaliki!

  3. Utemi saingine GENES tuu, wengine sie vizazi vya hawa wafuatao

  Rahabu! (Alichomtenda mjeda mwakijua)
  Mke wa isaka ( Alivowachakachua wanawe)
  Esther! ( Alivomuingiza KING mfalme myahudi, mzima mzima)
  Delila ( Alichomfanyia Samsoni)
  Mke mpya wa Herode (Alivomwmbia bintie aombe kichwa cha Yohane!!!!)
  Cleopatra ( Alivomtenda Kaisari wa watu.)

  Yaani hata HISTORY inaonesha kuna PERCULIAR species za kike ambazo currently researchers wamezipa chromosome XXX badala ya XX ambazo ni NOMAAAAAAAA!!!!
   
 3. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  ich liebe die! :poa:poa:poa Kaizer njoo utafsiri!:A S-coffee:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Bazazi una mambo! Nimefurahishwa na ubunifu wako kwa kuleta thread kwa staili tofauti kidogo.
  Anyway kwa kuwa haya ni mashairi ya Shaaban Robert na tafiti zake, nisingependa kuongeza neno.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...