Mwanamke wa kuoa utamjua tu

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
BABY NUMBER ONE.

Sio kazi ngumu sana kuelewa mwanamke anaekupenda kiukweli. Mwanamke anaekupenda kweli hawezi kukuomba wewe kitu chochote bali atachohitaji kutoka kwako sana sana ni muda wako na 'attention' yako kwake.

Hayo mengine kuhusu pesa, outing, shopping na mengineyo unatakiwa kujiongeza wewe kama mwanaume na sio kubweteka na kupendwa, kwasababu mwanamke wako anahitaji matunzo vilevile.

Anachohitaji mwanamke ni wewe tu na muda wako. Wanawake wameumbwa na moyo 'strong' lakini katika suala la mapenzi na hisia wako 'sensitive' sana. Wanahitaji kupendwa na wanahitaji kuona akijaliwa.

Mwanamke akikupenda kweli kutoka moyoni mwake atahitaji awe na wewe muda mwingi, atakutext mara kwa mara, atakupigia simu every time when she feels she wants to talk to you.

Atakuwa kama mtoto mdogo anayehitaji kupendwa, kukumbatiwa, kubebwa na kutizamwa kwa umakini.

Mpende sana mwanamke wa aina hiyo, muda mwingine aweza kuwa anakufuatilia sana mpaka unajiuliza nina 'date' na shushushu ama nini? Ila unapaswa kutambua kuwa anakupenda kwa dhati na anataka ajihakikishie kuwa yupo peke yake kwako.

Ukipata mwanamke wa aina hiyo tulia, usimuumize wachana na mitambo mingine, utazunguka bucha zote lakini nyama ni ile ile sana sana utamaliza nauli yako na nguvu zako za kuzunguka kila bucha.

Na ukiona mwanamke wako hayupo angalau kidogo tu ya hayo niliyotaja hapo juu basi jikatae kwake mapemaaa, sio baadae nikiandika status kuhusu wanawake hapa unakuja kutoka povu ooh wanapenda pesa ooh wanapenda vitu vya gharama ooh sijui nini.

Hutakiwi kulalamika, wanawake wa aina hiyo unaowalalamikia ni wajasiriamwili na wewe sio level yao, ambao ni level yao hawaoni tabu kuhonga wanaweza kuhonga hata meli. Mariah Carey pete yake tu ya kidoleni aliyopewa na Mchumba wake bilionea wa Australia ni takribani Tsh Bilioni 15 za Kitanzania.

Kama umeona hapo sio level yako wewe jikatae mapema, huwezi pigana na ukuta mwisho wa siku utaumia wewe, mwache aendelee kuchimba bwawa kama ndio maisha aliyoyachagua.

Wanawake wenye upendo wa kweli wapo. Ukimpata jifanye kipofu kwa wengine wote, ila ona kwake tu! Kilicho kizuri kitunze kidumu.
 
Nyongeza:

1) Ana maisha yake mwenyewe: "Katika mawazo yangu, mwanamke awe na maisha yake mwenyewe. Na kwa 'maisha yake mwenyewe' nina maana: kazi yake mwenyewe, kuweka mambo yake mwenyewe na marafiki, kujitegemea mwenyewe, ndoto zake mwenyewe, na rundo la kumbukumbuku, ndoto na matarajio yake mwenyewe. Haya bila ya shaka ni mambo mhimu na ya haki kwa mwanamke unayetaka awe mkeo".

2) Mwenye kuleta changamoto: "Yeye ni changamoto kwangu ili binafsi yangu iwe bora"
 
Humu wanasemaga wanaoolewa ni form 4 tu,wenye digrii hakuna kitu,sasa sijui Leo watasemaje
 
Usiombe mwanamke akupende ni shida hasa kama unamfikisha kisawasawa
1460145974140.jpg
 
Na mwanaume wa kukuoa haombi papuchi

Weeee weeee wewe., usirudie kusema hicho.

Mwanaume ana mama yake, ana dada zake, ana wasichana marafiki maeneo anayoishi au kufanyia kazi, ana marafiki wa kushirikiana naye biashara, kumshauri mambo mengine mengi tu. Ila hajakamilika bila mke. Je huyo mke kazi yake ni nini? Wa nn? kwani ndoa ni nn?

Faida za kuwa na girlfriend, mchumba, mke jina lolote utakalomwita ni
1. Sexual fulfillment. ..
2. Sexual fulfillment. ..
3. Sexual fulfillment. ..
4...
.
.
.
N
 
Hiyo ni baada ya kumuoa.. ila wakati unamfukuzia hutakiwi kuomba papuchi mpaka uoe kwanza
 
Back
Top Bottom