Mwanamke wa Kimasai wa Loliondo atoa ushuhuda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke wa Kimasai wa Loliondo atoa ushuhuda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Nov 14, 2009.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mwanamke wa Kimasai Kooya Timan, kutoka Loliondo, ameingia na kutoa ushuhuda Banjul katika mkut ano wa Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika ([FONT=&quot]African Commission on Human and Peoples’ Rights) Banjul, Gambia. Ameelezea yaliyotokea akisema hata wanawake walibakwa.

  [/FONT]
   
 2. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Picha za jana za Mwana mama wa Kimasai toka Loliondo na mwenzake mzee Orkoskos Yaile
   

  Attached Files:

 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Katika mkutano huo pia kulikuwa na pretentation kuhusu Loliondo, mfano Marrianne Wiben Jensen wa International Work Group for Indigenous Affair (IWGIA) alisema:


  na ingine ilisomwa na Edward Porokwa wa PINGOS Forums na yeye alisema:
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Porokwa ndiye aliyekuwa akitafsiri maelezo ya Kimasai.
   
 5. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Jambo la kusikitisha ni kwamba Serikali haijatuma mwakilishi, wakati Kamishna aliyemaliza muda wake, Advocate Nyanduga, anatoka Tanzania. Hata ripoti iliyowasilishwa muda mchache uliopita, imehoji ni kwanini Tanzania haijatuma mwakilishi wala haijajibu hoja kuhusu Loliondo ambayo Rais Kikwete aliandikiwa barua mara mbili ya kwanza Agosti 6, 2009 na Oktoba mwaka huu.

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/42563-barua-kwa-rais-jakaya-kikwete-kuhusu-loliondo.html

  ACHPR Wamesema watamuandikia tena. Na hii ACHPR ni chombo cha AU ambako JK alikuwa akiongoza na kuna mikataba.
   
 6. K

  Kibori Member

  #6
  Nov 14, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mimi sioni haja ya kutoa picha na majina ya watu waliotoa habari... I stand to be corrected , but to me mtoa habari ni kama vile anashitaki au anawahumu waliotoa habari... Mimi nidhani ingekuwa inatosha tu kusema chanzo cha habari bila kusema kama niilivyo nukuu hapo juu .....

  It is a good story and it shows how serious the issue or matter is, lakini ndugu mtoa habari nadhani ingetosha bila kusema nani na kutoa picha ya waliofanyahivyo... otherwise kwa sura hii inaonyesha sura ya kuwashitaki wahusika
   
 7. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Uko sahihi kwa majina. Lakini hakuna tatizo. Kwani hakuna wa kuogopwa na hiyo ni public session na muda si mrefu wanaonyesha video ya matukio ya Loliondo na wanaoonyesha ni Makamishna wa Tume ya AU ya Haki za Binadamu. KWanza hao serikali wameshindwa kufika, wanazidiwa na watendaji wa serikali za Ethiopia, kenya na ZImbabwe wanajitetea hapa. Nadhani kuna kujiamini kupita kiasi.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  who cares in the Tanzania government? Loliondo tayari imepewa kwa Generali just like Dowans italipwa. Kwani alivyokuja Zayed mdogo hii summer hapo Bongo mliambiwa alikuja kwa ajili gani? Loliondo ilitosha kabisa kumuondoa madarakani Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete. Kama vile Dowans watu wale wale hawaendi kokote na wanaamini kuwa tukipiga kelele basi tutafukuza wawekezaji!

  Kwani hao wapambanaji CCM kuna yeyote amesema lolote kuhusu Loliondo zaidi ya uchunguzi sijui ufanyike kama walivyotuma kamati ya Bunge kwenda huko zaidi ya miaka 18 tangu ufisadi wa Loliondo uanze?
   
 9. K

  Kibori Member

  #9
  Nov 14, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji you correctly said it all ....Halisi Congratulations for your keen follow up on the issue ... I am gald to hear that there is a close follow by the ACHRP . Lakini Mwanakijiji viongozi hawafanani kiutendaji na kifikira na nyakati ni tofauti pia let us see how the situation is going to like this time, I believe kama umesoma hiyo barua alioandikiwa JK na ACHPR chair, in fact some thing good for the community might come out of it . I understand that your wish this time is to expect something different against the government, and there is no reason why it should not but let us wait and see otherwise once again I wish to thank Halisi kwa kutuhabarisha .... You never know !
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kibori, kuna watu hapa wame-specialise kudai sources za kila kinachoandikwa... nadhani hpa hawatakuwa na hoja
   
 11. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tanzania inayokimbia hoja Gambia
  [​IMG]

  Ndimara Tegambwage ​

  [​IMG] SITAKI kuamini kwamba Tanzania imesusia mkutano wa 46 wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) ya Haki za Binadamu unaoendelea mjini Banjul, Gambia – Afrika Magharibi.
  Hakuna kibao kinachoonyesha ujumbe wa Tanzania unakaa wapi. Hadi jana, jina la mjumbe kwenye mkutano huu lilikuwa halijaonekana kwenye orodha ya wajumbe kutoka nchi za Afrika. Tanzania iko wapi?
  Huu ni mkutano mkubwa unaoleta wajumbe kutoka nchi wanachama wa AU. Hoja kuu ni Haki za Binadamu. Kila nchi ina wawakilishi wa serikali. Vilevile kuna wawakilishi kutoka asasi mbalimbali za kijamii zinazojihusisha na haki za binadamu.
  Tanzania iko wapi? Kikao cha Alhamisi kilikuwa na hoja zinazohusu Tanzania. Hoja kuu na ambayo haijapatiwa ufumbuzi ni ile ya wafugaji wa Loliondo na sehemu nyingine nchini. Mara hii aliyeanza kuchokonoa hakuwa Mtanzania. Alikuwa Marianne Wiben Jensen wa Copenhagen, Denmark.
  Marianne ni Mratibu wa Mipango wa kundi la kimataifa linalohusu masuala ya jamii za asili (indigenous people) kwa kanda ya Afrika (IWGIA) alivyosema Marianne:
  "Hali ya wafugaji wanaohamahama inaendelea kuwa ngumu zaidi katika nchi za Afrika ikiwamo Tanzania ambako wafugaji wametupwa nje ya ardhi walikokuwa wakiishi miaka nendarudi." Baada ya hapo aliorodhesha kinachowasibu wafugaji.
  Alisema kitendo cha kuchoma makazi ya Wamasai katika vijiji vinane vya Loliondo; mali zao kuunguzwa na mifugo yao kusambaa na mingine kupotea kabisa, ni cha kuvunja haki za binadamu. Aliorodhesha yafuatayo na kutaka yajibiwe na serikali.
  Kwamba zaidi ya makazi 200 ya Wamasai yalichomwa moto; maghala ya chakula chao yaliunguzwa; kwamba zaidi ya watu 3,000 hawana mahali pa kuishi kutokana na ukatili huu na mashamba ya mahindi ambayo yalikuwa na mazao yaliyokomaa yaliunguzwa moto. Mtu wa serikali hayupo. Nani atajibu?
  Hayo yametendeka wakati ukame mkali umesababisha njaa kubwa, mito midogo kukauka; madimbwi kuwa mashimo tu yasiyokuwa na tone la maji na kufanya mifugo kukosa malisho na maji; hivyo kufa kwa wingi.
  Mratibu wa IWGIA anasema mali ya thamani ya mamilioni ya shilingi imeharibiwa katika zoezi lililohusisha askari wa FFU na walinzi wa kampuni ya Ortello Business Corporation iliyopewa na serikali eneo la Loliondo kwa ajili ya kufanyia uwindaji.
  Kwamba askari wa FFU walifanya ukatili kwa wafugaji; kwamba katika zoezi hilo , wanawake walibakwa na wengine waliofukuzwa makazini mwao walitoa mimba wakiwa wanakimbia moto wa risasi za polisi. Mtu wa serikali hayupo. Nani atajibu tuhuma hizi?
  Marianne haishii hapo. Anasema familia zimevunjwa na mafundo yake kuteketea kwani baadhi ya watoto wamepotea kutokana na woga wakiwa wanakimbia milio na moto wa risasi. Kwamba matambikio ya Wamasai yalichomwa pia na baadhi yao wamekamatwa na polisi na kutungiwa mashitaka ya kubuni.
  Mwanaharakati huyo anasema serikali haijachukua hatua yoyote kusaidia waliokumbwa na maafa hayo; badala yake imewaacha wajihangaikie katikati ya ukame, njaa, ukosefu wa makazi na ukosefu wa malisho kwa ng'ombe waliosalia nao. Hakuna msemaji wa serikali. Nani atajibu haya?
  "Tunataka kukumbusha kwamba serikali ya Tanzania, Septemba 2007, iliunga mkono Azimio la Umoja wa Mataifa juu ya haki za watu wa asili…na Tanzania imetia saini mikataba kadhaa ya kimataifa inayolinda haki za binadamu," ameeleza Marianne.
  Lakini anasema tendo la serikali kuhamisha wafugaji wa Loliondo, kwa mabavu na a kuharibu makazi yao na chakula chao, ni kukiuka sheria na mikataba ya kimataifa. Hakuna msemaji wa serikali. Nani atajibu?
  Inawezekana mjumbe hajatoka Dar es Salaam au yuko katika moja ya hoteli za mjini hapa akisubiri siku ziishe. Lakini kwa vyovyote vile, haya ni madai makubwa ambayo yanastahili kujibiwa na serikali.
  Juzi Alhamisi, wakati wasilisho hilo likifanywa, watu wengi walikuwa wakitupa macho huku na kule kutafuta kuona msemaji wa serikali ya Tanzania. Kwa kuwa hoja hiyo itaendelea kujitokeza leo na kesho, bado shauku ya kuona msemaji wa Tanzania ingalipo.
  Agosti mwaka huu, Tume ya Haki za Binadamu ya AU ilimwandikia Rais Jakaya Kikwete ikimwomba maelezo juu ya hali ya Loliondo – wafugaji kutishiwa, kufukuzwa kwenye makazi yao, kuchomewa nyumba, mazao na mifugo.
  Kwa mujibu wa ofisa wa tume hiyo, serikali ya Tanzania haijatoa maelezo yoyote. Haijulikani itatoa lini maelezo hayo. Haijafahamika ni hatua gani zitachukuliwa iwapo haitatoa majibu. Aidha, wafugaji wawili wa Loliondo wako mjini hapa na kwa mujibu wa ofisa wa tume, watakutana na Mwenyekiti wa Tume hii ya AU kesho, Jumatatu.
  Yuko wapi mjumbe wa Serikali ya Tanzania kumaliza kiu ya Watanzania walioko hapa pamoja na wajumbe kutoka Afrika nzima ambao wamesikia tuhuma hizi? Labda atafika kesho. Sitaki ashindwe kufika.


  http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=10350
   
 12. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Tungeiunganisha na ile ya Loliondo kule kwenye Jamii inteligence
   
 13. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #13
  Nov 15, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hii issue ni very serious..ibaki hapa hapa. Duh! maskini Tanzania..inaelekea wapi hii 21 century??
   
 14. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #14
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  mmmmmh
   
 15. m

  matejoo Member

  #15
  Nov 16, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Swala la Loliondo na haki za wafugaji kwa ujumla ni mwiba mbaya sana kwa serikali ya Kikwete. Kwa kifupi kuna wasaidizi wake (wakiwemo mawaziri) wanaona ni vitu vidogo lakini visipopatiwa ufumbuzi legacy nzima ya Kikwete itaishia kule kwa kina Al Bashir na wenzake. Hapa hakuna ubishi. Ukiukwaji WA KUTISHA wa haki za binadamu umefanyika. Serikali iwa wajibishe wahusika kisha iombe radhi na kuwa fidia waathirika tusonge mbele. Kuziba masikio dhidi ya wananchi/wafugaji masikini kiasi cha kuwasingizia kuwa ni raia wa Kenya can not be justified by any sensible government. Tumefikia udikteta mbaya sana Tanzania. Sijui tunaelekea wapi. Mungu atunusuru!
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Chadema, Dr. Slaa, Zitto, Mkandara, na wengine wote.

  Kama hili hamlioni basi kweli TUMELIWA. Kama Mbowe unaliona hili na mmekaa kimya, basi nyie na CUF wote ni MAPACHA ambao kaka yenu ni CCM.

  Kwa mawazo yangu ni kuwa hapa mmepewa zawadi ya wazi kabisa. Nendeni huko na mchukue film zote hadi zile walizoweka kwenye YOUTUBE nina uhakika mnaweza kupata copy nzuri. Nendeni kwenye hospital ambazo zimemliza hadi Naomi na chukueni film documental.

  Mwakani badala ya kupita na helkopita, nendeni vijijini na Projectors na onyesheni hizi film kwa wananchi. Waambieni kuwa hata watu wa Loliondo mwanzo walikuwa wanaona CCM ndiyo baba yao na milele atawatetea. Hiki ndicho kimewapata na tena wakiwa chini ya mbunge wa CCM.

  Nendeni kwenye wachimba madini huko Mara wanaounguzwa na chemicals za wachimba dhahabu na wote hao mtengeneze film. Badala ya kupita na kuwaambia watu, piteni na muonyeshe. Na mwisho piteni na mchukue picha za misarafa ya Vigogo, majuma yao, magari yao na ndugu zaona muwaonyeshe Watanzania jinsi wenzao wanavyoishi wakati wao wanasota. Na muwatakie heri kwa kuiweka tena CCM na Rais wao madarakani.

  Inatakiwa itengenezwe film yenye ukweli asilimia 80 na propaganda asilimia 20. Mtu akiona basi atoke machozi. Kama ZAWADI kuzidi hii, basi mtasubiri milele..
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mambo haya hapa kama kuna watu wamepika kila kitu na nyie ni kupakua tu na kula:

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=iqP2MRuJ4Ac[/ame]

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=i-FP2gRvziw&feature=related[/ame]

  Ningelikuwa Scotland juzijuzi, kulikuwa na haja ya kumpa Mwinyi na Mkewe coffee nyingine ya MOTO ili na wao waone utamu wa kufanyiwa UNYAMA kama huu. Kuna haja siku moja hawa viongozi anakuja kichaa na ANAFILISI mali zao zote (Waliohusika) na kuwatupa kwenye vibanda vya kawaida kabisa na inakuwa wananyang'anywa Pasport.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwani Loliondo inagusa vipi Tanzania yote? kwani Buzwagi inagusa vipi Tanzania yote? Kwani Meremeta inagusa vipi Tanzania yote? Mwananchi Gold? EPA, CIS, na mengine lukuki? Kwani watu wa Dar wamechukizwa na mlipuko wa mabomu au mlipuko wa kipindu pindu kila mwaka? Kwani Hospitali ya Temeke ambako wajawazito wamekuwa wakijazana kwa miaka sasa huku serikali inampango wa kujenga mabarabara ya kwenda juu kwa juu mmesikia Temeke wamelalamika?

  Well.. we get what we deserve, and what we have now is what we deserve!
   
 19. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #19
  Nov 16, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hili jambo la loliondo lilishawahi kujadiliwa sana hapa JF. Waziri alikanusha kuwa hakuna unyanywasaji uliofanyika na pia watu waliochomewa maboma hawakuwa watanzania, swali ninalojiuliza: ikidhibitika kuwa kulikuwepo na vitendo vya unyanyasaji na waliochomewa maboma walikuwa watanzania,Je waziri atawajibika kivipi kufuta kauli yake ya hawali kuwa hakuna madhara yeyote yaliyo tokea?
   
 20. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #20
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145


  Duh nikali hiyo mbona nilipitaga huko Arusha na sikusikia habari hizo na je pale Arusha yawezekana utowaji wa habari umekandamizwa ??? au police haitoi habari ipasavyo ina wabeba watu fulani fulani na kuwafichia mambo yao na kuwanyanyasa wanyonge ??

   
Loading...