Mwanamke wa hivi hafai hata kidogo

Mwanamke wa hivi hafai hata kidogo

dexterous

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
2,037
Reaction score
3,149
''Baby,This is January, una mpango gani na mimi?""Mwaka huu ukiisha bila kunioa kwakweli sitakuelewa, Monica waofisini anaolewa tarehe 26, my BFF Stella anaolewa March, my roommate Sandra anaolewa na yule BF wake wa South Africa mwezi wa 6, nabaki mimi tu, kwakweli sitaki.""Kama huna mpango wa kunioa mwaka huu niambie kabisa, kuna these 2 guys wananifuatilia muda tu nimewapotezea kwa ajili yako lakini naona hueleweki."

Ukiona Msichana anakwambia hizi sentensi wala usijisumbue kumuoa. Ndoa sio mashindano kwamba usipokimbia fasta atashinda Usaini Bolt.

Anataka umuoe kisa mashosti wanaolewa kwamba ye ataonekana kachelewa, lakini tu anasema kuna vijana wawili wako tayari kumuoa that means hana consistency, ana plan A,B,C hadi Z..Yeye shida ni Ndoa ila sio nani kamuoa. Kaweka Timing, akikukosa wewe basi ana reserve na si ajabu hata hao wawili anaowasema wako pending tayari wameshaweka Signature bila wewe kujua.

Mwanamke wa namna hii, akisema tu hizi shombo, we mwambie samahani mpenzi mahari nimejengea mabanda ya kuku wa Mayai.Nitakushangaa kama utakurupuka na kuanza kututumia Meseji za michango ya Harusi ya 'Crash Programme' kisa demu kakupiga mkwara ili umuwahi uwashinde wale wawili. Huo ni Usukununu!Hautakuwa umeoa Mke ila Umeoa Vodafasta!
 
Na nyie punguzeni kukaa na watoto wa watu miaka na miaka wakati hamna mpango nao.Mie naona message ni nzuri tu mtu unakaa na mtu miaka kibao lakini hata siku moja hakwambii future yenu ikoje lazima mtu uchoke
 
jaman kuna kitu napata shida kuelewa! relationship 7 hardly yrs na ukiwauliza ndoa lin wanakwambia may 2 or 3 yrs to come!!! kkyna watu wana hiyo uhusiano sasa binti kageuka mtumwa!!!
 
mmh mbona shemeji yangu hakukuoa kwa wewe kumshinikiza?
 
jaman kuna kitu napata shida kuelewa! relationship 7 hardly yrs na ukiwauliza ndoa lin wanakwambia may 2 or 3 yrs to come!!! kkyna watu wana hiyo uhusiano sasa binti kageuka mtumwa!!!

possible kabisa mbona kuna watu wana 11 years na wako kwenye 30's wala hawawazi ndoa wala familia
 
jaman kuna kitu napata shida kuelewa! relationship 7 hardly yrs na ukiwauliza ndoa lin wanakwambia may 2 or 3 yrs to come!!! kkyna watu wana hiyo uhusiano sasa binti kageuka mtumwa!!!

Umeoona eeeh.Uvumilivu mwingine haufai kabisaa.Na unakuta mdada anapelekeshwa kisa kufukuzia ndoa halafu at the end unyamaze tu kisa ukisema utapigwa chini
 
Kama mwanamke unayemvua kyupi anathubutu kukwambia such statements basi utakuwa future mume -----.

Kwangu mimi kabla hujamaliza nakuomba tuachane kwa amani because tumekutana wote tushaota meno haina haja ya mizevezo

#TeamExtrimist
 
Kinachotatiza wengi ni muda na umri. mwanamke ana kuzaa/kuzalishwa jambo hili kwao linaendana sambamba sana na umri. Mwanaume ana uchaguzi mkubwa hata umri ukiwa mkubwa, mwanamke kadri umri unavyosonga na ndiyo uchaguzi wake unapungua. Kukumbushwa siyo mbaya. Kukumbushwa ni wajibu ila kutekeleza ni hiari.
 
Umeoona eeeh.Uvumilivu mwingine haufai kabisaa.Na unakuta mdada anapelekeshwa kisa kufukuzia ndoa halafu at the end unyamaze tu kisa ukisema utapigwa chini

ni zaid ya kupekekwa huyu bibt aisee!!! ukizingatia kijana kamzis binti mwaka mmoja tu kyzaluwa sasa binti ashaanza kuobekana mkubwa kwa kijana ila ndo yupo tu!

mara leo huku mara kule! ni huruma kwa kweli!

but huwa nawaza ya Mungu mengi, hiv ndo ibatokea mmoha katangulia mbele za haki, unasema umefiwa na nani! maana official uchumba bado! loooh, cjui tukafiche waoi watoro jaman
 
nimejitahidi kusoma ila ulivyopanga maandishi naona ni hatari kwa macho yangu.
 
''Baby,This is January, una mpango gani na mimi?""Mwaka huu ukiisha bila kunioa kwakweli sitakuelewa, Monica waofisini anaolewa tarehe 26, my BFF Stella anaolewa March, my roommate Sandra anaolewa na yule BF wake wa South Africa mwezi wa 6, nabaki mimi tu, kwakweli sitaki.""Kama huna mpango wa kunioa mwaka huu niambie kabisa, kuna these 2 guys wananifuatilia muda tu nimewapotezea kwa ajili yako lakini naona hueleweki."

Ukiona Msichana anakwambia hizi sentensi wala usijisumbuekumuoa. Ndoa sio mashindano kwamba usipokimbia fasta atashinda Usain Bolt.

Anataka umuoe kisa mashosti wanaolewa kwamba ye ataonekana kachelewa, lakini tu anasema kuna vijana wawili wako tayari kumuoa that means hana consistency, ana plan A,B,C hadi Z..Yeye shida ni ndoa ila sio nani kamuoa. Kaweka Timing, akikukosa wewe basi ana reserve na si ajabu hata hao wawili anaowasema wako pending tayari wameshaweka Signature bila wewe kujua.

Mwanamke wa namna hii, akisema tu hizi shombo, we mwambie samahani mpenzi mahari nimejengea mabanda ya kuku wa mayai.
Nitakushangaa kama utakurupuka na kuanza kututumia meseji za michango ya harusi ya 'Crash Programme' kisa demu kakupiga mkwara ili umuwahi uwashinde wale wawili. Huo ni Usukununu!Hautakuwa umeoa Mke ila Umeoa Vodafasta!

Yaani hiyo situation ndo nipo nayo sasa demu wangukuanzia mwezi wa kumi mwaka wa jana anakula pilau la mashost zake tu...baaasi ni tabu tupu kila siku ndoa letu lini maskini angejua mm plan ni kama three years mbele......
 
kukumbushwa sio mbaya but sio Kwa style ya kusingizia una wanaume wanakusubiri....kuna mmoja alimuacha jamaa yake akaenda Kwa jamaa aliyemuahidi ndoa,matokeo yake akapewa mimba na kuachwa....still single mpaka leo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom