Mwanamke ukipendwa pendeka

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
17,014
Reaction score
23,662
Nawasalimu members wenzangu

Ndugu zangu nilikuwa tuna jirani yetu mmoja alikuwa ana uhusiano wa kimapenzi na binti mmoja anayeitwa Rehema. Huyu jirani yetu alikuwa ni mpole, mstaarabu pia ni mtaratibu alikuwa anampenda sana mchumba wake huyo, hata ikitokeaga mkwaruzano ambapo ni kawaida katika mahusiano huyu jamaa ndio anajishusha.

Kwa upande wa kipato, ana kipato cha kawaida na amekuwa akimuonyesha upendo mpenzi wake Rehema sana ikiwemo kumfulia nguo zake, kumpikia, kumtoa out kwa kipato hiko hiko cha kawaida alichonacho mpaka ikafika hatua ya kutaka kumuoa kabisa.

Mpenzi wa huyo jamaa Rehema alikuwa na rafiki yake anaitwa Grace although nakupendwa kwake na huyo jamaa lakini alikuwa na tamaa za maisha mazuri so njemba mmoja alikuwa anaishi Kimara Korogwe ambaye alikuwa na maisha mazuri na rafiki yake Grace ndio alimuunganishia so wakawa na uhusiano lakini pia huyo njemba alikuwa na mke wake kabisa.

Pamoja na Grace kumuunganishia shoga yake Rehema kwa huyo njema lakini pia akamchomesha kwa mpenzi wake kwa kumuonyesha picha za mabusu kati ya mpenzi wake na njemba huyo ambaye anaishi Kimara Korogwe.

Baada ya kujua huo ukweli akaamua kumuacha mpenzi wake bila hata vurugu kwa amani, kumbe lengo la Rehema ni kutaka kuwa na uhusiano na mpenzi wa Grace wa kwanza na alikuwa anampenda sana ndo maana akamchomesha rafiki yake Grace.

Baada ya muda kidogo tukasikia kwamba Rehema ana uhusiano na mpenzi aliyekuwa wa Grace huku kwa upande wa Grace akamwagwa na yule njemba wa Kimara Korogwe baada ya mke wa huyo njema kugundua kupitia message za mumewe. Badala la timbwili kuwa kubwa kati yake na mkwewe huyo njema akaona amuache
Grace.

NB: Wanawake inapotokea ukapendwa jitahidi upendeke na muache na tamaa msije mkawa kama Grace ingawa now sina taarifa zake maana sasa hivi haishi tena mtaani kwetu. Kutokana na hizi tabia za kama Grace ndio maana hamuolewinmaana baadaye mnakuja kusumbua makanisani kuombewa mara upo kwa Kakobe mara kwa Gwajima mara kwa Rwakatare. Mnasumbua sana. Kuna wanawake wengine mnapata wanaume bora alafu mnashindwa kuwatumia vizuri.
 
Nani alikuambia mwanamke anashauriwa nani wa kumpa kitumbua chake?
 
Nimfulie?
Nimpende?
Nimtunze?
Nimtoe out?
Alafu tubwagane bila sababu

Hastahili risasi, ila basi hata rungu la kisogo limtembelee. πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Yaani hapa kama haujaishi uswahili ama kusoma magazeti ya Shigongo utapata tabu sana kuelewa!
 
Nyie wenzangu mmeelewa hii story?

ebu ngoja nirudie kwa makini...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…