Mwanamke tunza thamani yako

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,770
10,660
Mwanamke ameumbwa akawekewa nakshi mbalimbali mwilini mwake za kuvutia kama matiti, matako laini, miguu iliyoumbika, hana manyoya bali ngozi laini na nyororo, nywele nzuri, mapaja ya kuvutia, sauti laini n.k.

Biblia inamtaka mwanamke avae modestly, why? Anawajibu wa kuwalinda jirani zake. Imeamriwa mpende jirani yako kama nafsi yako. Wanawake wajifunze kujiheshimu wenyewe kwanza, waheshimu maungo yao, ndipo wapewe heshima wanayostahili. Mavazi ya kuwaacha uchi ni kukiri kuwa wao ni sex objects.

Kama wewe mwanamke unataka kuwa hivyo basi vema, endelea kuvaa nusu uchi, ila usilalamike pale unapotumika halafu huolewi, pale unapopewa mimba ukaachwa, pale unapobakwa n.k. kwa sababu unavutia watu wasio sahihi kwako. Mwanamume sahihi hawezi kuja kwako hata siku moja, kwani mwonekano na tabia yako vinamweka mbali. Wanaume watakutenda kama sex object. Watakutumia kukidhi kiu zao pasipokuwa na malengo na wewe.

Siku hizi wanawake hawawazii ndoa tena, wanafukuzia starehe tu. Wanajikuta wakitumika kwa starehe kuanzia mashuleni mpaka vyuoni, wengine hufikia hata kujiuza huku wakiwa masomoni. Hawawazi ndoa, wanawaza kukidhi mahitaji ya jamii kwa wakati huo. Inapofikia wakati wanahitaji ndoa wanakuwa wameshachelewa tayari. Hivi wewe ni nani hata ukidhi kiu ya jamii hii ya leo?

Jamii ya leo hairidhiki na kitu, imeshavuka mipaka, watu wanataka mpaka mapenzi ya jinsia moja!! hawatosheki tena, unajidai kuwa una boyfriend, kumbe wewe ni sex object!! Unajidanganya unakwenda na wakati kumbe umeshauacha nyuma wakati, unazama shimoni, umeirejea Sodoma na Gomora. Halafu unakimbilia kwenye media kudai haki sawa na heshima, kwa kipi unacholeta kwenye jamiii? Uko wapi mchango wako? Unapolilia haki ya kuthaminiwa uvaaji wako, kwamba ni haki binafsi, eti una uhuru juu ya mwili wako, jamii ikuchukulie vipi? Unavaa kikahaba, unaishi maisha ya kikahaba halafu ukitendwa kama kahaba unalalamika, why?

Banana Zoro alipoimba mapenzi yamekwisha siku hizi hakuwa anatania. Mapenzi ni kweli hakuna tena, yamepoa. Unaanzaje kuwa na mapenzi na mtu ambaye amejiweka uchi kwa jamii, unampendea nini!? Kuna kipi kipya cha kuteka tena akili ya mwanamume? Je ni elimu yake? Kazi yake? Ufundi wake kitandani? Kipi hasa cha kukuvuta kwake? Ndio maana siku hizi ndoa hazikai, wenza wanapendana for the wrong reasons. Hakuna tena mapenzi ya kweli, ni maigizo tu.

Mume ukijigamba mke wangu ni mtamu kitandani, wanaume wengine wanakucheka tu, moyoni wanasema ungejua sisi ndio tuliomfaidi wakati akichipukia. Yaani mume unakuwa huna cha kujisifia juu ya mkeo, unajikuta unaishi kwa pressure tu. Ukimwona anasalimiana na X wake hata kama wamekutana kwa bahati mbaya, tayari amani inatoweka. Mapenzi yatatoka wapi? Unalazimika kutengeneza uadui usio rasmi na wanaume wale unaowajua kuwa waliwahi kumpitia mkeo, halafu unatafuta huruma ya Mungu, kwa lipi hasa? Ndipo ugumu unapoanzia, Mungu kaagiza mpende adui yako uipate mbingu, unaweza wewe? Mapenzi yako wapi hapo? Maigizo tu!!!

Madini yanapata thamani yake kutokana na ugumu wake kupatikana. Almasi, dhahabu n.k. Lakini vitu kama mawe, hayana thamani kwa sababu hata mengine tunayang'oa ili tupate nafasi za kujenga makazi n.k. Mchanga wa kujengea haukuwahi kuwa na thamani mpaka pale mahitaji yalipozidi, ukaadimika.

Sasa wewe mwanamke ukitaka kuwa na thamani kama rubi ama tanzanite, jiweke uwe adimu kupatikana. Watu watoke jasho kweli kweli, wengine mpaka wafirisike juu yako (sio kwa kula pesa zao, bali kwa kununua vitu vya gharama kubwa kama usafiri na vitu vingine ambavyo wanadhani kwa hivyo watakuvutia). Mwishowe utampata mtu sahihi atakayekufaa. Mtu sahihi pamoja na mengine atakuvika pete ya uchumba bila masharti ya ngono.

Itaendelea.....
 
Unapokosoa mwenzio hakikisha nawe si mkosefu.. Bro Jesus alikua na Courage na na Guts za kuwaambia wengine ni wakosefu coz alikua Mwanadamu mkamirifu.

Btw Ujumbe wamepata
 
Mkuu.....ni mama zetu, dada zetu, wake zetu na ni mabinti wetu......tuwaapendege tuu....
 
Unapokosoa mwenzio hakikisha nawe si mkosefu.. Bro Jesus alikua na Courage na na Guts za kuwaambia wengine ni wakosefu coz alikua Mwanadamu mkamirifu.

Btw Ujumbe wamepata
Unakosea sana kuona maonyo kama ukosoaji. Wwpo wanawake wema tu, ila hapa ni kuwakumbusha wale waliokengeuka na sio kuwakosoa. Pia ingekuwa hivyo basi injili ingeendelea kuhubiriwa na Yesu pekee maana ndiye mkamilifu.

Fuata kilicho sahihi yasiyofaa achana nayo. Vinginevyo dunia ya leo imejaa watu wa aina yako, wanaoogopa kuisema kweli kwa kisingizio kuwa itawakwaza watu. Siko hivyo mkuu, kwenye mapungufu yangu niambie nami nitajirekembisha, huo ndio upendo wa kweli
 
Imeandikwa;
“Hero kuchagua jina jema kuliko mali nyingi”

Mithali 22:1

Jina linaweza kubeba hatima ya mtu!

Salamu ziwafikie wale wote wenye majina yenye Uelekeo hasi popote walipo!

Tafadhali kisha chukua hatua!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom