POKEA_SALAM_ZANGU.
.
1) Mwanamke Elimu Kazi Pesa na Mali zako haziwezi kukufanya uwe mke BORA katika ndoa yako bali ni heshima Kujali hekima na busara zako kwa Mumeo.
.
2) Mwanamke anae muheshimu na kumskiliza mmewe ni mwanamke bora ambae kila mwanaume angetamani kuwa nae.
.
3) Tabia yako na misimamo yako ndio itakayomfanya mumeo ajute au afurahie kukuoa wewe.
.
4) Kuwa mke bora inakubidi uwe vizuri katika kutawala hasira Mdomo na maamuzi yako na sio kulipiza visasi.
.
5) Kuwa kiongozi huko kazini kwako ni jambo Jema ila kuwa mke mnyenyekevu nyumbani kwenye Ndoa yako hiyo ni jambo Jema zaidi.
.
6) Usiweke mashindano na mumeo, mpe hongera na mtie moyo kwa kila hatua anayopiga katika maisha sio Umdharau kwakuwa Umempita Vingi.
.
7) Kuwa na ubinadamu, sio kosa lake dogo tu unamsema vibaya Kwa Ujeuri wako wa Mali Elimu na Vyeo Vyako vya kazini hiyo haipendezi atajiona yupo jeshini na sio Ndoani.
.
8) Kuwa mkarim katika maongezi mpaka huduma zingine jua kila mwanaume anamuheshimu mwanamke mkarimu na mwenye huruma.
.
9) Usijaribu kumpa Adhabu mumeo mara kwa mara hasa ya kumnyima chakula cha Kitandani , hii itamlazimu kutafuta chakula nje ya ndoa yaani kwa Mama_Ntilie ([emoji23][emoji23] ).
.
10) Hakuna ubaya kama utakua unakubali kosa pale utakapo kosea.
Kuwa mrahisi kukubali kama kweli ulikosea.
.
Na omba radhi inapobidi na pia hakikisha haurudii tena kuvifanya anavyovichukia hii utamfundisha hata yeye Kuwa hivyo.
.
11) Jiandae kumsamehe mumeo pale anapokosea kwa maana mke atoae msamaha kwa mumewe ni mke mwema tofauti na yule aliejaa visasi chuki na kujiona.
.
12) Tengeneza maamuzi ya kuwa mke mwema, pasi na kuwa na hofu yoyote na Mungu atakubariki katika vile unavyomuomba.
.
13) Mke mwema hatafutwi kwa kuangaliwa Umbo Sura Miguu yani alivyojazia Bali mume mwema hutazama Tabia busara upole hekima upendo ili hata ukizeeka au kukatwa kiungo au kuumwa atazidi kukupenda tu Kwa sifa hizo.
.
14) Wewe ni mwanamke na yeye ni mwanaume basi huu utofauti usihusahau daima.
.
15) Alafu wewe mwanaume Mola kakujaalia mke anayejitambua basi na wewe uamke ujitambue na ushikamane nae jua mke mwema anataka Upendo zaidi kuliko Pesa na Mali zako.
.
.NB: picha inanogesha tu uzi!!!
.
CC: livewise1
View attachment 1141096