Mwanamke na Mwanamme

YNNAH

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
1,702
969
[h=5]Watu wawili, mwanamke na mwanamme walikwenda kwa daktari mtaalamu wa mambo ya uzazi.

Daktari akawauliza, "Ninaweza kuwasaidia nini?"

Mwanaume akamwambia, "Tafadhali daktari unaweza kututazama tukifanya mapenzi ili uweze kufahamu tatizo letu?"

Daktari akashangaa. Hata hivyo akakubali kuwatazama. Walipomaliza kufanya mapenzi, daktari akawaambia, "Mbona sijaona tatizo lolote na namna mnavyofanya mapenzi?"

Watu wale wakamlipa gharama ya ushauri wa kitaalamu sh. 10,000/= kisha wakaondoka zao.

Jambo lile likaendelea kwa majuma kadhaa. Kila wiki wanakuja kwa daktari, daktari anawatazama wakifanya mapenzi. Daktari anawaambia hawana tatizo lolote. Kisha wanamlipa pesa. Wanakwenda zao.

Siku moja, baada ya daktari kuona jambo hilo linamchanganya sana, akaonelea ni vema kuwauliza. "Lakini ninyi ndugu, ni nini hasa tatizo mlilonalo mnalotaka mimi kulifanyia uchunguzi?

Mwanaume akamjibu daktari, "Wala hatuna tatizo lolote dokta. Huyu mwanamke ni mke wa mtu hivyo hatuwezi kufanyia mapenzi nyumbani kwake. Mimi pia ni mume wa mtu hivyo hatuwezi kufanyia mapenzi nyumbani kwangu. Pia hatuwezi kumudu kufanyia mapenzi kwenye hoteli kwa kuwa gharama ni zaidi ya laki moja kwa siku moja. Nyumba za kulala wageni za kawaida gharama yake unakuta haipungui elfu hamsini. Kufanyia kwenye gari ni hatari zaidi maana polisi wa patroo wakitukuta tutatakiwa tuwahonge zaidi ya elfu thelathini.

Lakini hapa kwako tunafanya mapenzi kwa shilingi elfu kumi tu. Zaidi, tunafanya mapenzi tukiwa chini ya ulinzi wa hali ya juu zaidi ulimwenguni.

Vipi tunaweza tukaweka apointimenti nyingine tuje hapa Jumatatu ijayo?"[/h]
 
Mhh hawana lolote wanaogopa kufumaniwa tuuu chezea mume wa mtu na mke watu ila hawaogopi kunasa kweli

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom