Mwanamke miaka 64 kizimbani kwa utapeli

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,400
MKAZI wa Boko Magengeni, Elizabeth Balali (54), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya hakimu Bonifasi Lihamwike, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Veronika Mtafia, alidai kati ya Oktoba 19 na Desemba 5 mwaka 2017 eneo la Tegeta, Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa alijipatia Sh milioni 25 kupitia Benki ya CRDB akaunti namba 0152151528100 kutoka kwa Rodrick Kisenge kwa madai ya kutaka kumuuzia kiwanja kitu ambacho si kweli.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamhuri ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hakimu Lihamwike alisema dhamana yake ipo wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika ambao mmoja atatakiwa kutoa hati ya nyumba na mwingine bondi ya shilingi milioni moja.

Mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakaposomwa Machi 18.

Wakati huo huo, Richard Mhimbila (35) mkazi wa Goba, amepandishwa kizimbani kwa shtaka la kujipatia fedha kwa udanganyifu.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya hakimu Joyce Mushi, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuru, Abudi Yusuph, alidai Oktoba 8 mwaka jana katika Benki ya Equity Bank iliyopo Quality Center, Wilaya ya Temeke kwa lengo la udanganyifu, mshatakiwa alijipatia Dola za Marekani 2,050 kutoka kwa Andrew Mwasalemba akijidai atamnunulia gari kutoka Japan huku akijua ni uongo.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamhuri ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hakimu Mushi alisema dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya shilingi milioni 5.

Mshtakiwa alikidhi masharti ya dhamana na kuachiwa hadi kesi yake itakaposomwa tena Machi 22.


= Mtanzania
 
Back
Top Bottom