Mwanamke kutoka India ‘akatwa mkono’ Saudia

Mwanamke kutoka India ‘akatwa mkono’ Saudia

BOB OS

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
3,462
Reaction score
7,007
151009111124_kasturi_munirathinam_512x288_bbc_nocredit.jpg

Kasturi Munirathinam amelazwa hospitalini

Wizara ya mashauri ya kigeni ya India imelalamikia serikali ya Saudi Arabia baada ya mwanamke raia wa India kudaiwa kukatwa mkono na mwajiri wake mjini Riyadh.
Mkono wa Kasturi Munirathinam mwenye umri wa miaka 58 alikatwa mkono wa kulia na mwajiri wake alipojaribu kutoroka.Bi Munirathinam alikuwa akifanya kazi kama mhudumu wa nyumbani. Kwa sasa anaendelea kupata nafuu hospitalini.Familia yake inadai amekuwa akiteswa na mwajiri wake.
Maafisa nchini Saudia bado hawajazungumzia kisa hicho.Waziri wa mashauri ya kigeni wa India Sushma Swaraj ameandika kwenye Twitter: "Hili haliwezi likakubalika kamwe. Tumewasilisha malalamiko kwa maafisa Saudia. Ubalozi wetu unawasiliana na mwathiriwa.”"Kukata mkono wa mwanamke kutoka India – Tumekasirishwa sana na ukatili aliofanyiwa mwanamke huyo wa India nchini Saudi Arabia,” Bi Swaraj aliongeza.Familia ya Bi Munirathinam katika jiji la kusini mwa India la Chennai imesema mwajiri wa mwanamke huyo alikasirika baada yake kulalamikia mateso aliyokuwa akitendewa nyumbani.Alikuwa amefanya kazi kwa mwajiri huyo kwa miezi mitatu.Visa vya watu kutendewa unyama na waajiri wao Mashariki ya Kati vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara, raia wanaotoka Afrika Mashariki wakiwa miongoni mwa waathiriwa.

source:Mwanamke kutoka India ‘akatwa mkono’ Saudia - BBC Swahili
 
waarabu kwanini ni wakatili hivi??

Ndivyo walivoumbwa hata hapa bongo kuna makabila ya watu wakatili, wapole, wabaguzi, wenye roho mbaya n.k
Vyote ni kwa ajili ya sifa na utukufu wa Mungu.
 
mkuu amerika kuna wasaidizi wa kazi.


europa kuna wasaidizi wa kazi.

kwanini hizi habari za manyanyaso zitoke uarabuni tu?
Kama ndiyo hivo hapa nchini pia tunatesa!!
cheki..
[h=1]Gazeti Mwananch :
Tajiri adaiwa kumng'ata, kumchoma pasi mtumishi wake kwa miaka mitatu[/h]

mgongo.gif
Yusta Lucas akionyesha makovu yake ya mgongoni ambayo aliyapata kwa kung'atwa na kuchomwa na pasi na mwajili wake. Picha na Esther Kabakaya

[h=3]Kwa ufupi[/h]"Akienda kazini anafunga geti na kunikataza kufungua hata kama mtu atagonga… sokoni nilikuwa naenda siku ambazo yeye yupo tu na huwa akiniamrisha niende haraka na kurudi pasipo kuzungumza na mtu yeyote."

By Daria Erasto, Mwananchi Dar es Salaam. Mfanyakazi wa ndani, Yusta Lucas (20) amekumbana na masahibu yanayofanana na yale ya mtoto Nasra Mvungi (4) aliyekuwa amefungiwa kwenye boksi kwa miaka karibu minne huko Morogoro. Huyu amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam akiuguza majeraha yanayotokana na kuteswa na kufungiwa ndani kwa miaka mitatu.

Binti huyo, mwenyeji wa Mkoa wa Tabora, katika Kijiji cha Kampala amedai kuwa amekuwa akiteswa na kufungiwa ndani ya nyumba na tajiri yake, Amina Maige wa Mwananyamala, Kwa Manjunju katika kipindi chote hicho. Amina anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba OB/RB/9967/2014.
 
Ukatili wa wasaudi dunia nzima inaudahamu.
na hapa nchini jee...

[h=5]Saturday, June 14, 2014[/h][h=1]UKATILI: Mtoto ateswa miaka miwili[/h]

merina_moi.jpg
Mtoto Merina Mathayo (15) akiwa amejeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Dar es Salaam. Picha na Beatrice Moses

[h=3]Kwa ufupi[/h]
  • Akizungumza kwa shida Merina alisema amekuwa katika hali ya mateso tangu mwaka 2012, kwani bosi wake huyo ambaye anamtaja kuwa ni mwanasheria mkazi wa Boko amekuwa na tabia ya kumpiga na vitu mbalimbali akiwa amemvua nguo.

By Beatrice Moses, Mwananchi Dar es Salaam. Mtoto Merina Mathayo (15) amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (Moi) Muhimbili Dar es Salaam, baada ya kuteswa na kujeruhiwa kichwani kwa kipigo maeneo mbalimbali ya mwili na bosi wake kwa miaka miwili.

Merina amelazwa Moi baada ya kupewa rufaa na Hospitali ya Mwananyamala alipokuwa amelazwa awali, kutokana na majeraha hayo ambayo yanadaiwa kusababishwa kung'atwa kwa meno na kupigwa kwa vitu mbalimbali mara kwa mara.
 
waarabu makatili sana pia kwa racism hawajambo Selikali ya ccm inawafuga tu huku dar
 
huyu muarabu pumbavu sana anamkata mkono ....badala mikono yote....kata yote hao wenyewe wanatufanya WATUMWA ndani ya nchi yetu
 
mkuu Zamilumi zamilumi sijui unabisha au unajaribu kulinganisha au unapinga hata sikuelewi.
 
Last edited by a moderator:
Na vipi kuhusu wahindi wao hawana racism?!


Halafu sio SELIKALI ni SERIKALI

Msalimie sana mwalimu wako

hao wahindi ndo balaa... heb jaribu siku kupanda lift moja na wahindi wawili tu pale posta afu uje ulete mrejesho hapa. hawa malofa wanajifanya wana-Take Over kilakitu kene nchi etu
 
Back
Top Bottom