Mwanamke kutaka mahali mil500 ni sawa?

Mwanamke kutaka mahali mil500 ni sawa?

IKIRIRI

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
2,734
Reaction score
3,027
Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm, Diva amesema kwa sasa haangalii tena ukubwa wa mahari bali anachohitaji ni mapenzi ya kweli.

Kipindi cha nyuma mtangazaji huyo alikaririwa akisema ili kuolewa anahitaji kutolewa mahari ya Tsh. Milioni 500 ila kwa sasa hataki tena hilo.

“Milioni 500 imebadilika sasa hivi nahitaji mtu mwenye mapenzi na mimi ya ukweli, sitaki mtu anayekuja kunitumia kwa vitu vyake halafu inaaza kuathari kazi yangu, no 500 just need real love,” amesema Diva.


BONGO 5


Je, ni sawa kwa mwanamke kutaka mahari ya milioni 500?

Mtazamo tu wadau cz Leo kajinadi...
 
Kama yeye mwenyewe ameridhia ni sawa kabisa Ila awe mpyaaa hajaguswa
 
Mtaji tosha huo
Ni mtaji tosha kwa maskini kwa matajiri wakubwa hiyo ni pesa ya kumnunulia mchumba Pete ya uchumba ya Almasi tupu na chain za kuvaa za madini ghali.tulushaongea sana humu kuwa kila MTU aoe saizi yake.Huyo mtoto wa kike unakuta wazazi wake wamempa biashara na maghorofa ulaya na marekani na anamiliki ndege za abiria na visima vya mafuta kwake milioni 500 ni nini?tatizo hapa maskini ambao hawajawahi shika hata milioni 10 wataka dezo ndio wanajitia ohh anajiuza.unaijua hadhi ya huyo mwanamke?
 
Ni mtaji tosha kwa maskini kwa matajiri wakubwa hiyo ni pesa ya kumnunulia mchumba Pete ya uchumba ya Almasi tupu na chain za kuvaa za madini gari.tulushaongea sana humu kuwa kila MTU aoe saizi yake.Huyo mtoto wa kike unakuta wazazi wake wamempa biashara na maghorofa ulaya na marekani na anamiliki ndege za abiria na visima vya mafuta kwake milioni 500 ni nini?tatizo hapa maskini ambao hawajawahi shika hata milioni 10 wataka dezo ndio wanajitia ohh anajiuza.unaijua hadhi ya huyo mwanamke?
Mahari haitangazwi hadharani
 
Back
Top Bottom