Mwanamke kuonekana tofauti na mwanamke mwenzake

goldie ink

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
5,634
9,140
Habari wana jamii wote wa jamii forum,
Naamini ni wazima na mnaendelea vyema pia yapaswa kumshukuru mungu kwa uwezo wake kwa kutuweka salama mpaka dakika hii.

Leo ni mwisho wa wikiendi siku ya jumapili, si vibaya tukabadilishana mawazo na kuelimishana pia.

Labda niende moja kwa moja katika mada / swali husika, kama kichwa cha habari kinavyosomeka vyema hapo juu.

Mwanamke kuonekana tofauti na mwanamke mwenzie, nikiwa na maana ya kwamba katika jamii yetu tumekuwa tukiwaona wanawake kama viumbe ambao wanapenda kujihusisha na jambo/ vitu vizuri zaidi, kama kuvaa nguo nzuri, kuendesha gari zuri, kuishi kwenye nyumba nzuri, kufanya kazi nzuri, hali kadhalika hata kuwa na mahusiano mazuri ya kimapenzi na mwanaume. Lakini ikitokea kinyume na hapo kama anavyotarajia na kuona mwanamke mwenzake anavyo huwa anasikia wivu wa aina fulani, labda nikupe mfano mzuri ili niweze kueleweka vyema katika hii mada/ swali,
" Nikiwa katika kituo cha daladala kuna mwanamke nilimkuta akiwa katika harakati za kusubiri usafiri hapo kituoni, lakini baada ya dakika kadhaa akatokea mwanamke mwingine ambaye alionekana kuvaa vizuri kuliko yule niliyemkuta kituoni hapo, lakini mmoja alimwangalia mwenzake kwa macho ya wivu kana kwamba amependeza zaidi kuliko yeye.

Mfano wa pili.
Nikiwa kanisani wakati nasubiria ibada ya pili nikakutana na mwanamke ambaye tunafahamiana ( Lissa ) tuliongea maneno hapa na pale huku tukikumbatiana na kupeana busu za shavuni, kushikana mikono ili hali bado tupo kwenye maongezi yetu, lakini akatokea mwanamke mwingine ( Anitha ) ambaye ni rafiki wa huyu ( Lissa ) cha ajabu alimtizama rafiki yake kwa macho ya wivu na macho ya kuzungumza kitu Fulani, nikawa nimeshindwa kuelewa maana nimekuwa nikiona wanawake hutizama sana na huleta taswira tofauti.
31302d5225a79463154187252260e409.jpg

SWALI:
swali langu ni kwamba wanawake wanapokutana katika mazingira fulani kwanini..?? hutizama mno kiasi kwamba kuangalia amevaaje, anamuonekano gani, ana shepu zuri au baya, huu mtizamo unaashiria wivu, au kuvutiwa na mwanamke mwenzio jinsi alivyo au inakuwaje....??

NOTE BY:
majina na picha yaliyotumika katika mada hii si ya kweli bali ni mifano ili mada iwe kwenye mpangilio wa kueleweka.
 
Yaani mleta mada uko sahihi, kuna siku nilikwenda kanisani na jirani yangu ambae tunasali pamoja, nilijikuta nimevaa gauni sare na dada mmoja. Ni magauni ya high street, yule dada hakutegemea kukutana na mtu amevaa gauni kama la kwake. Jirani yangu ambae ni mwanaume alicheka sana, alisema hivi nyinyi mnamatatizo gani wanawake? Ingekuwa wanaume tungesalimiana na kuulizana wapi umenunua mfano shati lako.
 
Hawa viumbe wanambwembwe zao wakiwa pamoja wanonyesha wanapendana sana wape kadistance kidogo tu hali inakuwa tete.
 
utakuwa unaishi kijiji cha mtakuja

yaani mnatizamana afu mnasaliana kiisharaza wivu? na kwanini uhisi kakuona kwa macho ya wivu je kama lissa alikopa kiatu kwa huyo dada na anakiona kakivaaa.

ishi kwa kutokujihisi utaona amani tele yote uliyozumgumzia ni kwakujihisi tu.
 
Yaani mleta mada uko sahihi, kuna siku nilikwenda kanisani na jirani yangu ambae tunasali pamoja, nilijikuta nimevaa gauni sare na dada mmoja. Ni magauni ya high street, yule dada hakutegemea kukutana na mtu amevaa gauni kama la kwake. Jirani yangu ambae ni mwanaume alicheka sana, alisema hivi nyinyi mnamatatizo gani wanawake? Ingekuwa wanaume tungesalimiana na kuulizana wapi umenunua mfano shati lako.
Sista uko Sahihi na hii haiishi hapo tu,inakwenda mbali zaidi hata kwenye Mambo ya Msingi katika Maisha,linapo kuja Suala la Haki za Wanawake,Mwanamke Hudhani Mwanaume ni Adui kwake bila kutambua kuwa Adui wa Mwanake ni Mwanam...ke
 
Yaani mleta mada uko sahihi, kuna siku nilikwenda kanisani na jirani yangu ambae tunasali pamoja, nilijikuta nimevaa gauni sare na dada mmoja. Ni magauni ya high street, yule dada hakutegemea kukutana na mtu amevaa gauni kama la kwake. Jirani yangu ambae ni mwanaume alicheka sana, alisema hivi nyinyi mnamatatizo gani wanawake? Ingekuwa wanaume tungesalimiana na kuulizana wapi umenunua mfano shati lako.
Itabidi hili suala lianze kupatiwa mabadiliko taratibu. Wanawake wapendane na kuwa wamoja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom