Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,113
- 24,642
Kuna hili suala la wanawake kutongozwa kisha kumwambia mwanaume kuwa ametongozwa na flani na ameahidiwa kitu gani.
Binafsi limenitokea mara kadhaa, kuna wanawake ambao ni marafiki tu wa kawaida ninakuwa nao wamekuwa wakinieleza pale wanapotokewa na wanaume.
Takribani asilimia kubwa hata kama ni marafiki wapya wa kike nimekutana na hili jambo, hivi nia kubwa inakuwa ni nini? Halafu imekuwa kwamba yule anayetongozwa anasema amemkataa huyo aliyemtongoza na anakuwa anamponda.
Sasa humu bila shaka kuna wenye tabia hiyo, hivi huwa nia ya mwanamke kutongozwa na kimwambia mwanaume ambaye hata siyo mume/mchumba au hajawahi kukutaka ni nini? Wanaume mliokutana na hili suala kama mpo mlichukuliaje?