Mwanamke KAMILI....!!

Utashambuliwa hapo hujui kunaimani tofauti humu!
but ukweli unabaki palepale!
Atakayenishambulia ana yake coz hapo nimejielezea mm na sio wote atiiiii!
Nimeongelea ninachokiamin mm binafsi ni c lzm kila mtu akiamin!!
 
Mwanamke kamili ni mwanamke ambae anajiweza kihisia na kifikra, mwanamke ambae sio tegemezi wala maisha yake hayatawaliwi na kuzira.
. . Badala ya kuzira unajieleza.

Mwanamke ambae anaifahamu nafasi yake kama mama pia mwenzi, anaetambua wakati gani wa kusimamia anachoamini na wakati gani wa kutumia nguvu ya penzi.
. . Na kwa kujua nafasi yake katika mahusiano haina maana anajiweka chini ama anajiweka juu, sio mtu wa "YES SIR" au "NO SIR"
pekee bali ni yule anaejua kwamba ni mshauri/mshawishi wa mwenzi na ndicho anachofanya kila anapoona mwenzake anafanya maamuzi yasiyo mazuri kwao.

Mwanamke wa ukweli ana KIASI kwenye kila jambo, hakubali maisha yake yazungukwe na utando.
. . Kama anapenda kunywa pombe anajua ni kiasi gani kinamtosha badala ya kusababisha aibu kwake na kwa familia yake, anafahamu ni kiasi gani cha mambo ya nyumbani kwake anaweza kushare na watu wa nje n.k

Mwanamke kamili anamwelewa mwenzi wake, haongozwi na fikra za kibinafsi na mawazo ya 'chake ni chake'.
. . Uelewa wa wakati gani yuko vipi na wakati gani anataka/hitaji nini. Haoni yeye anastahili zaidi ya mwenzake, ni mtoaji kama ambavyo ni mpokeaji.

Mwanamke kamili hutimiza majukumu yake,
Haachi nafasi ya yeye kuonekana mzembe.
. . Ndio kuwa na dada/kaka wa kazi imekua mtindo wa maisha kwa wengi, ila kuacha wao ndio waendeshe familia yako ni uzembe. Anaelewa kwamba "Mama mwenye nyumba" kama ilivyo "mzazi" ni zaidi ya kuwa na nyumba/mtoto.

Mwanamke kamili anatambua nguvu ya uanamke wake,
Hua mwangalifu hata atumiapo ulimi wake.
. . Anafahamu kwamba sauti/maneno na matendo yake ndani ya nyumba yanaweza yakavuta watu karibu ama yakawafukuza.

Mwanamke kamili hana makuu,
Huishi vile wawezavyo na sio kama wafanyavyo majuu.

Mwanamke kamili hujipendezesha, hujiweka safi ili mwenzi kumridhisha.

Mwanamke kamili huwajibika, hutatafuta utatuzi wa matatizo badala ya kucharuka.
. . Matatizo, yawe ya chumbani au ya kifamilia anajua anatakiwa atafute utatuzi badala ya kutafuta replacement katika mazingira tata na kukuza/ongeza matatizo.

Mwanamke kamili hachoki kujifunza, habweteki na kusubiria kufukuzwa.

Mwanamke kamili hukwepa shari, na utulivu wake huuchukulia kama fahari.

Kudos to all "Wanawake Kamili" out there, YOU are appreciated. Be blessed!!
Mimi naamini ni mwanamke kamili japo sijatimiza nusu ya hayo yote !
 
Gwaride kubwa.. (6x6=36)......unaweka materio yapi anga hiyo mtaalamu..??

"KUWAJIBIKA , KUMUELEWA MWENZAKE, HACHOKI KUJIFUNZA na KUTOKUA MBINAFSI"
Yote hayo yanahusika japo yapo kwenye vipengele tofauti.
 
Back
Top Bottom