Mwanamke KAMILI....!!

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,778
59,133
Mwanamke kamili ni mwanamke ambae anajiweza kihisia na kifikra, mwanamke ambae sio tegemezi wala maisha yake hayatawaliwi na kuzira.
. . Badala ya kuzira unajieleza.

Mwanamke ambae anaifahamu nafasi yake kama mama pia mwenzi, anaetambua wakati gani wa kusimamia anachoamini na wakati gani wa kutumia nguvu ya penzi.
. . Na kwa kujua nafasi yake katika mahusiano haina maana anajiweka chini ama anajiweka juu, sio mtu wa "YES SIR" au "NO SIR"
pekee bali ni yule anaejua kwamba ni mshauri/mshawishi wa mwenzi na ndicho anachofanya kila anapoona mwenzake anafanya maamuzi yasiyo mazuri kwao.

Mwanamke wa ukweli ana KIASI kwenye kila jambo, hakubali maisha yake yazungukwe na utando.
. . Kama anapenda kunywa pombe anajua ni kiasi gani kinamtosha badala ya kusababisha aibu kwake na kwa familia yake, anafahamu ni kiasi gani cha mambo ya nyumbani kwake anaweza kushare na watu wa nje n.k

Mwanamke kamili anamwelewa mwenzi wake, haongozwi na fikra za kibinafsi na mawazo ya 'chake ni chake'.
. . Uelewa wa wakati gani yuko vipi na wakati gani anataka/hitaji nini. Haoni yeye anastahili zaidi ya mwenzake, ni mtoaji kama ambavyo ni mpokeaji.

Mwanamke kamili hutimiza majukumu yake,
Haachi nafasi ya yeye kuonekana mzembe.
. . Ndio kuwa na dada/kaka wa kazi imekua mtindo wa maisha kwa wengi, ila kuacha wao ndio waendeshe familia yako ni uzembe. Anaelewa kwamba "Mama mwenye nyumba" kama ilivyo "mzazi" ni zaidi ya kuwa na nyumba/mtoto.

Mwanamke kamili anatambua nguvu ya uanamke wake,
Hua mwangalifu hata atumiapo ulimi wake.
. . Anafahamu kwamba sauti/maneno na matendo yake ndani ya nyumba yanaweza yakavuta watu karibu ama yakawafukuza.

Mwanamke kamili hana makuu,
Huishi vile wawezavyo na sio kama wafanyavyo majuu.

Mwanamke kamili hujipendezesha, hujiweka safi ili mwenzi kumridhisha.

Mwanamke kamili huwajibika, hutatafuta utatuzi wa matatizo badala ya kucharuka.
. . Matatizo, yawe ya chumbani au ya kifamilia anajua anatakiwa atafute utatuzi badala ya kutafuta replacement katika mazingira tata na kukuza/ongeza matatizo.

Mwanamke kamili hachoki kujifunza, habweteki na kusubiria kufukuzwa.

Mwanamke kamili hukwepa shari, na utulivu wake huuchukulia kama fahari.

Kudos to all "Wanawake Kamili" out there, YOU are appreciated. Be blessed!!
 
I prefer huko mtaani, because ur love is my love.

Mtaani it is then. . unipe tu vigezo vichache ambavyo ni binafsi alafu mi ntazingatia vile ambavyo ni general na nnajua unastahili!!Lolz
 
Naomba ufafanuzi hapa
Lawino hapa anaegemea kwenye No Sir au Yes Sir au mshawishi/mshauri?
Kabla sijaongea sana

Mwanamke ambae anaifahamu nafasi yake kama mama pia mwenzi, anaetambua wakati gani wa kusimamia anachoamini na wakati gani wa kutumia nguvu ya penzi.
. . Na kwa kujua nafasi yake katika mahusiano haina maana anajiweka chini ama anajiweka juu, sio mtu wa "YES SIR" au "NO SIR"
pekee bali ni yule anaejua kwamba ni mshauri/mshawishi wa mwenzi na ndicho anachofanya kila anapoona mwenzake anafanya maamuzi yasiyo mazuri kwao.
 
Kwa hayo maelezo, wasio na wenza hawawezi kuwa wanawake kamili!
 
Hii ni thread ya wanawake kamili!
Ngoja nione kama kuna atakayejitokeza hapa aseme yeye si kamili......
Woooote watajiita ni wanawake kamili lakini "wizi mtupu".........

Kwa kuongezea hapo kwa Mwanamke kamili...
1. Mwanamke kamili Hashei wanaume, anamiliki kikojoleo kimoja tu cha mwanaume na kukitumia ipasavyo
2. Mwanamke kamili "hamsumbui" hovyo mwanaume kamili anapokuwa anaburudika na bia na wanaume kamili wenzake
3.Mwanamke kamili hana wivu wa kijinga, ili mradi hajawahi kumfumania mwanaume wake, mme wake anabakia kuwa innocent
4. Mwanamke kamili akimfumania mme wake anamsamehe akijua fika kuwa mwanaume kamili hajaumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja
5.Mwanamke kamili haangaiki kumchunguza mme wake wala kupekuapekua visivyomhusu kama simu nk
 
Back
Top Bottom