Mwanamke jifunze kutumia akili na sio moyo, pale unapoamua mwanaume yupi umkubalie au umkatae kati ya wale wanaokutongoza

Artifact Collector

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
6,539
10,007
Kuna bidada ameleta mada kwamba "yule ambae humpend ndo mume" Kuna kitu ambacho nimekiona Kwa wanawake wengi wa jf na wanawake katika jamii tunazo ishi, wanasema mwanaume kama moyo umegoma basi achana nae, na hii inatokana na wao kuongozwa na hisia na sio akili.

Moja ya laana Mungu aliyempa mwanamke ni yeye kutawaliwa na mwanamme, na hii ni kwa sababu mwanaume amepewa uwezo na wepesi wa kutumia akili, kuliko mwanamke, na haina maana kwamba mwanamke amekatazwa kutumia akili hapana, ila Kwa wanawake wengi hawana wepes wa kutumia akili kama ilivyo kwa wanaume, kwa sababu wanawake wengi ni wepes sana kutumia moyo katika maamuz tofaut na wanaume.

Moja ya vitu muhimu vya kufahamu ni akili na moyo vinashindana, na kila kiungo kimoja wapo kinataka kuongoza maamuzi ya binadamu, Ili lazima tulifahamu, ndo maana unaweza ukawa na hela, moyo unakuambia kainywee bia, akili inakuambia itunze, na hata katika maisha mtu anayetumia akili kuliko wenzake, lazima atakua kiongozi katika familia, kazin na sehemu nyingine, na ili ufanikiwe katika nyanja zote za maisha hakikisha akili inaongoza moyo na sio vinginevyo.

Mwanamke unapomkataa tu mwanaume Kwa kisingizio cha moyo umegoma ni hatari sana, kwa sababu moyo haujapewa uwezo wa kuona mbali kama ilivyo akili, mfano wanawake wa miaka 20's wengi wao wanaongoza na moyo (hisia), na ndo maana ikitokea hajaolewa na anamiaka 30's ghafla anaanza kutumia akili na sio moyo tena, na hata perception zake za maisha zinabadilika.

Lakini kama angekuwa anatumia akili tokea akiwa na miaka 20's, kuna uwezekano asingefika 30'bila kuolewa, na hata wale wanaoolewa Kwa sababu moyo umekubali, wanakuja gundua wamefanya makosa, Kwa sababu moyo haujapewa uwezo wa kuona mbali kama ilivyo akili. Hata katika familia mama akiwa anatumia akili kuliko baba atakua kiongozi wa familia, Kwa kumalizia moyo unanafasi yake katika kuchagua mwenza, lakin akili ndo iwe mwamuz wa mwisho
 
Moyo nao una ubongo. Haukubali kila kitu akili inachouambia. Sasa chaguo ni lako, tumia akili au moyo.

Sent using my Nokia Torch
 
Ndio mana kila kitu kina faida na hasara zake
Zipo faida na hasara za kufuata moyo pale unapotafuta mwenza
Zipo faida na hasara pia za kufuata akili katika kutafuta mwenza

Kuna muda ni wa kutumia akili kweli ila katika masuala ya hisia naona ni heri kuhusisha moyo zaidi...
Sijajua nikifika huko 30's unakosemea ila kwa wakati huu wacha tu niangalie moyo ulipo
 
Sis wanaume tutaendelea kutumia akili
 
Naomba kuwasilisha...
IMG-20181220-WA0006.jpg
 
Ndio mana kila kitu kina faida na hasara zake
Zipo faida na hasara za kufuata moyo pale unapotafuta mwenza
Zipo faida na hasara pia za kufuata akili katika kutafuta mwenza

Kuna muda ni wa kutumia akili kweli ila katika masuala ya hisia naona ni heri kuhusisha moyo zaidi...
Sijajua nikifika huko 30's unakosemea ila kwa wakati huu wacha tu niangalie moyo ulipo
Okay....
Nikuelewa kwamba, kwasasa unaangalia moyo ulipo ili kuitimiza furaha yako...
Naamini ukifika huko mbeleni (30's) utaanza kutumia akili ili kutimiza ndoto ama future yako...
 
Okay....
Nikuelewa kwamba, kwasasa unaangalia moyo ulipo ili kuitimiza furaha yako...
Naamini ukifika huko mbeleni (30's) utaanza kutumia akili ili kutimiza ndoto ama future yako...

Ila hadi nifike huko nitakuwa nishakamilisha furaha yangu...AmEn!😊
 
Acha kwanza walimwengu tuwafundishe kutumia akili baada yakuwatumia
Sis wanaume tutaendelea kutumia akili
HAHAah kwa kweli

Acha sisi wanaume tutimie akili tu maana huo moyo ulichotufanyia mwanzoni Dunia ndo inajua

kujinyima ni jambo zuri sana kwa mustakabali wa baadae

Ila kila mtu afuate nyendo zake si lazima tufanane
SISI TUTATUMIA AKILI KWA 60% kwenye kila amuzi letu
 
Ndio ukweli unaofunikwa

Back
Top Bottom