Mwanamke: Je, unapendwa au unatumiwa?

Mwanamke: Je, unapendwa au unatumiwa?

Challya

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2019
Posts
469
Reaction score
609
Wakati uliopita niliandika uzi ambao ulikuwa unaelezea kuhusu mwanaume anayetumiwa na anayependwa na niliahidi kuandika pia kuhusu upande wa wanawake pia.
Kwa wanawake ni hivi;

MWANAMKE ANAYEPENDWA
1. Huyu mwanaume wake humtimizia mahitaji yake bila hata yeye kuanza kuomba, yaani mwanaume wake huwa hasubiri hadi akumbushwe.
2. Mwanaume wake humtambulisha kwa wazazi wake na ndugu zake na sio kwa marafiki tu.
3. Mwanaume wake humshirikisha katika masuala yake ya maendeleo.
4. Mwanaume wake akiongea nae hana "umimi" bali ana "usisi"
5. Mwanaume wake hapendi avae nguo za kuonyesha maungo yake bali hupenda avae nguo za heshima za kusitiri mwili wake wote.
6. Mwanaume wake humsikiliza na kumuheshimu hawezi kumfokea mbele ya watu.
7. Mwanaume wake hawezi kufanya mapenzi kinyume na maumbile na yeye.
8. Mwanaume wake hupenda kumfanya yeye awe mwakilishi wake katika sehemu mbalimbali akiwa yeye hayupo, kwamfano vikao au mikutano.
9. Mwanaume wake hubadili tabia ambazo mwanamke hapendi.
10. Mwanaume wake hupenda kumridhisha kitandani.

MWANAMKE ANAYETUMIWA;
1. Huyu hadi apewe mahitaji yake ni hadi asumbue vya kutosha
2. Huyu mwanaume humshauri kuvuta sigara, bangi na hata madawa kulevya.
3. Huyu kuliwa tigo ni kawaida tu.
4. Mwanaume hupenda avae nguo za kuonyesha maungo yake.
5. Huyu kupewa mimba na kuambiwa atoe ni kawaida tu, anaweza hata aambiwe atoe mimba mara tano
6. Huyu mara nyingi mwanaume hufanya nae mapenzi ili yeye aridhike na sio mwanamke aridhike.
7. Mara nyingi mwanaume wa huyu hupenda mahusiano yawe siri ,yaani unakuta uhusiano unajulikana tu na marafiki ambao wengi ni mabaharia.
8.Huyu huwa hashirikishwi kabisa kwenye masuala ya kimaendeleo.
9. Huyu kufokewa au kudhalilishwa mbele ya watu ni kawaida tu.
10. Mwanaume huwa anahakikisha pesa yake ameitumia vizuri haswa katika mwili wa huyu mwanamke.

=============

Soma kuhusu Wanaume: Je, unapendwa au unatumiwa? - JamiiForums
 
Na sisi Wezi sugu wa waume za watu tupo fungu gani mkuu[emoji22]
maana mambo yetu yapo kotekote tupe basi muongozo tujue wapi nyumba ndogo/wapi one night stand maana wanatuchanganya
 
Na sisi Wezi sugu wa waume za watu tupo fungu gani mkuu[emoji22]
maana mambo yetu yapo kotekote tupe basi muongozo tujue wapi nyumba ndogo/wapi one night stand maana wanatuchanganya
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dah!
 
Inategemea mtazamo wa mtu juu ya mwanamke mfano mimi pande zote mbili ulizozioanisha kuna sifa zangu.
Halafu hiyo picha ungeiondoa tu,haina maana hata.
 
Na sisi Wezi sugu wa waume za watu tupo fungu gani mkuu[emoji22]
maana mambo yetu yapo kotekote tupe basi muongozo tujue wapi nyumba ndogo/wapi one night stand maana wanatuchanganya
Kumbuka Agnes Mushi wa moshi yupo atakudhalilisha. Take care
 
Na sisi Wezi sugu wa waume za watu tupo fungu gani mkuu[emoji22]
maana mambo yetu yapo kotekote tupe basi muongozo tujue wapi nyumba ndogo/wapi one night stand maana wanatuchanganya
Wewe utakuwa unawapa limbwata[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom