Mwanamke jasiri!

kwamtoro

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
4,922
Reaction score
3,245
Ni yule ambaye afii kimya kimya kwa kuumia na penzi ambalo analo kwa mwanaume anaye mpenda. Mwanamke jasiri ni yule anayejua nini anakitaka, anachukuwa nafasi na ku hit her target.

Dada zangu dunia imebadilika sana na hasa katika mahusiano. Kama unafikiria unampenda mtu fulani kisha unabaki kimya tu, wanawake majasiri wapo wamekuzunguka na uamua kujaribu.

Wanawake walio wise nawependa sana ila wanawake otherwise amsheni akili akili zenu. Kusubiri kutongozwa na mtu ambaye unampenda imepitwa na wakati
 
Hili nalo neno, kumbe tuna wanawake wise na otherwise.
 
ngoja nianze kozi ya kutongoza aisee... loh kumbe kunamajasiri
 
ngoja nianze kozi ya kutongoza aisee... loh kumbe kunamajasiri

...dada nakusihi usianze hiyo kozi,itakuharibu. Hii tafsiri ya mwanamke jasiri imeletwa kuwafeva wanaume wasiojua wajibu wao na wanataka kupotosha jamii. Mwanamke jasiri ni yule mwenye msimamo na mwenye kudhibiti hisia zake kwa manufaa ya kizazi hiki na taifa kwa ujumla...
 

Haaa kweli aisee wanaume wa hiki kizazi wanashindwa kutongoza matokeo yake wanatutwisha sie mizigo. Hatudanganyiki
 
Hahahaaaaaaaaaaa!

Kijana una maono, lakini kiupeo bado mno
Nimeyakubali yako maono, ila bado mapema mno
Naomba kunyosha mkono, ili nitie japo neno
Wakati si konokono, japo hatua hio bado mno.
Ya ngoswe mtuachie ngoswe!

Kutaka kula kingi, hujukuta umeliwa nyingi.
Katu bf sio kingi, labda mumeo ndo umfanye kingi.
Bf atakutia utumwa mwingi, akivike majukumu mengi
Atakuwekea vingi vigingi, nakukupoteze mda mwingi
Ya ngoswe mtuachie ngoswe.

Tangu lini fisi akakataa nyama, busy unamkabidhi bucha?
Wanaume wengi wanyama, japo hodari wakuficha makucha,
Hata akishiba hakati nyama, tena anaifata mawindoni kucha
kirahisi rahisi umpelekee nyama, atakavoiparamia sipati picha.
Ya ngoswe mtuachie ngoswe.

Mwanaume hatongozwi anatekwa, kama kumvuta kuku bandani
Wamlegezea jicho lege lege kutwa, wamkaribisha kwako ndani
Wamgusagusa kimakosa kutwa, wajielezea wema wako wa ndani
Unamkirimia kama wako mpwa, ilihali mmekutana tu kibandani
Ya ngoswe mtuachie ngoswe.

Kiuno wamplegezea na kalio pia. Mwanamke si gogo la mnazi.
Mkitembea wamuwahi kumtangulia, kalio wamtikisia rahisi si kazi
Ukipika waepuka vitu kuungulia, wamkoleza kwakuti pia nazi
Wamsahaulisha wote waliotangulia, nakujisiti kwa stadha ya mavazi
Ya ngoswe mtuachie ngoswe
 
Hahahaaaaaaaaaaa!

Patamu hapo! hivi amjui maisha ni ujasiria mali. Unamuona Dude fighter, Kichwani yupo well. Ndio yule uliyekuwa unamfikiria miaka nenda rudi theni unakufa kimya kimya tu. Ila wewe lara 1 naamini upo wise. Lazima aingie ndani ya kumi na nane kama unataka, ama?????
 
Last edited by a moderator:
Wise na otherwise imenifurahisha mnooo.. M sijui niko wapi
 
Jamani weweee! hata sijui niseme nini.... maana leo ndoto zangu zimetimia. Ninavyokupendaga kwamtoro! mmmh finaly umenifungulia njia mwenyewe kwa mikono yako ..... Love youuu
 
Last edited by a moderator:
Jamani weweee! hata sijui niseme nini.... maana leo ndoto zangu zimetimia. Ninavyokupendaga kwamtoro! mmmh finaly umenifungulia njia mwenyewe kwa mikono yako ..... Love youuu

Loohhh!!! Bahati ya mtende kuokota embe kwenye mwarubaini. Karibu sana happiness win kwenye mikono iliyo salama ila ukubali kuwa na mke mwenza atug
 
Last edited by a moderator:
mtaanza kutongozana wanawake kwa wanawake sasa..endeleeni na ujasiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…