tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,863
- 3,854
Kuna mama mmoja (jina ninalo) ana tabia ya kutafuta visa na mikasa kwa kuchunguza maisha, makosa madogo madogo ya ndugu jamaa hasa wa upande wa mumewe. Visa hivi huanza mara tu baada ya ndugu hao na jamaa hao kuonesha mafanikio kielimu, kimaisha na kibiashara. Tena hutafuta chokochoko hata pale pasipo na sababu maalumu. Kitu cha ajabu ni kuwa upande wa ndugu zake hakuna hata mmoja aliyetoka sana kimaisha. Lakini mama huyu anakumbatia na kutetea sana upande wake ikiwemo kuwakabidhisha ndugu zake miradi kadha wa kadha ya mumewe. Ndugu za mumewe hawana noma na hilo na wanawachukulia ndugu hao wa mke kama ndugu zao. Sasa je kwa nini mama huyu anafanya visa na mikasa kwa ndugu wa mume tu. Hebu changieni wadau!