Mwanamke hawezi kuvumilia manyanyaso

Mwanamke hawezi kuvumilia manyanyaso

Kisai

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
29,126
Reaction score
29,333
Leo nina zawadi mbili (Moja ni hii na ya pili itafata) kutoka kiumeni kwenda kwa wake zetu vipenzi, kwenda kwa dada zetu, kwenda kwa mama zetu kwenda kwa walezi wetu wa kike. Leo nawasemea Wanawake kwa ujumla wao. Hakika hali wa shani Mwanamke hawezi kuvumilia kuishi na mwanaume anaye mnyanyasa.

1. Hata ukiwa tajiri kumzidi Mansa Kan Kan Musa mtawala wa Mali, mja ambaye aliyepewa utajiri wa dhahabu na akazigawa kama pipi kwa watu wenye kuhitajia, aliishi karne ya 13 Miladia mja huyu. Ukimnyanyasa lazima atakuacha na utajiri wako na kwenda sehemu isiyo na manyanyaso.

2. Hata ukiwa mzuri kumzidi nabii Yusufu (Japo hakuna aliye mzidi mja huyu) maadamu utamnyanyasa tu mwanamke, basi kaa ukijua lazima atakuacha na uzuri wako.

3. Hata uwe Mfalme wa kutawala majini na watu (Japo hakuna kwa leo hii) ila mwana wa Daudi yule "The King of the Vast Kingdom" namzungumzia nabii Suleyman, maadamu utamnyanyasa mwanamke, jua mwanamke huyo atashika njia na kukuacha na ufalme wako.

Juu ya nukta hizo tatu kuna mifano mingi, sababu jambo hili liko wazi, hakuna haja ya kuhudhurisha mifano hiyo.

Tuwapende wake zetu na tusiwanyanyase, japo kati yao na sisi,sisi ndiyo tunapenda zaidi kuliko wao, ndiyo maana majukumu ya kuwatunza na kuwalisha na kuwasimamia tukapewa sisi.

Kibwagizo

Wanaume tunasifiwa kuoa wake wengi na hatusifiwi ushupavu wala hela sababu hivi tunavitafuta, kwani wapo wenye hela wana mke mmoja kama tochi (Wana waogopa wake zao kama ukoma) sijui likizima ataenda kuazima kwa jirani,mpaka lije kuwaka nanga isha paa na jua limekucha.
 
Ungeongelea kidogo kuwa wananyanyaswa vipi? Maana mwanamke mwengine unakuta ni mke ila hata kumhudumia mumewe anaona ananyanyaswa.
 
Awali ya yote mkuu weka picha ya nabii yusufu nijipime u handsome!..
Kwanini suala la kuuliza maswaliya msingi kwako huwa ni muhali mzee ?

Tuwekee picha ya babu yako wa kumi.
 
Ungeongelea kidogo kuwa wananyanyaswa vipi? Maana mwanamke mwengine unakuta ni mke ila hata kumhudumia mumewe anaona ananyanyaswa.
Anayesema hivyo huyo si mke ni mwanamke.

Manyanyaso yanajulikana mzee. Hao tunawaita vichwa panzi.
 
Kwanini suala la kuuliza maswaliya msingi kwako huwa ni muhali mzee ?

Tuwekee picha ya babu yako wa kumi.
Swali ni la msingi ila vile tu umelichukulia!.. kama swali si lamsingi basi jua umeua hiyo hoja yako ya kuandika kuwa huyo nabii ni mzuri kushinda wanaume wote!.. Kama hukuwahi kuona sura yake basi umepima vipi huo uzuri wake..? Na je,ulishawahi ona binadamu wote kwenye dunia hii na kuhakiki kuwa ni yeye pekee tu ndio mzuri kushinda wote..?

Swala jepesi mkuu weka picha then tutarudi kwenye maswala anayoona ya msingi!
 
Swali jepesi hilo ndiyo maana nimekujibu kwa swali.
 
Swali jepesi hilo ndiyo maana nimekujibu kwa swali.
Sawa mkuu kwa kutupiga kamba live live..😂
Chakufanya namba moja naishikiria mimi kwa u handsome ndo anafata huyo yusufu.. halafu si ndo huyu aliemkimbia mke wa mfalme akamuachia linguo akaja akasingiziwa kesi..?? Sasa ushamba wote huo anakimbia papuchi si alimnyanyasa mke wa mfalme ndio maana akakosa uvumilivu akamsemelea kuwa alitaka kumbaka!!.. ningalikuwa Mimi walahi hiyo historia hapo isingekuwa hivyo ilivyo..😂

Tukirudi kwenye mada ni kweli mwanamke atakuacha tu ukimnyanyasa maana nature yao Ni kujaaliwa.. wao ni kama bustani ambayo ni sisi ndio tunaotakiwa kuangalia na kuihudumia mwishowe itupatie matunda..
 
Back
Top Bottom