Mwanamke havutiwi na six park zako

simba songea

JF-Expert Member
Feb 8, 2016
1,498
1,211
Wanaume tunadhani kwenda gym kutanua misuli basi mwanamke watadata. Tunajitahidi kuwa na six pack ili wanawake wachanganyikiwe na bodybuilding lakini ukweli ni kwamba mwanamke hivyo vyote havimpagawishi.

Ukweli ni kwamba, kiuhalisia mwanamke ni muoga Mara nyingi wanawake hawajiamini. Mwanamke anapenda akiongozana na mwanaume basi huyo mwaanaume awe na uwezo wa kumtetea akionewa. Wanawake hawapendi wanaume waliopoa au waoga hata wakiongozana nawe anakosa amani moyoni maana mwanaume niliye nae ni muoga hato nitetea nikipigwa.

Wanawake wanapenda mwnaume mwenye kujiamini, wanawake wanapenda wakiongozana na mwanaume barabarani wanavutiwa zaidi na mwnaume anayeongea kwa sauti(sio kupayuka) yaani aongee amsikie kwa ufasaha na sio kuuliza sijui umesamaje?

Sababu mwanamke kimaumbile ni muoga wakati mwingine anaogopa kukuuliza, na akishafanya hivyo basi hatofurahia maongezi maana hasikii unachosema. Kwani hujawahi ona unaongea afu mwanamke anatabasamu tu lakini ukimuuliza swali anashtuka kana kwamba mawazo yake hayapo hapo.

Sio ukweli kwamba wanawake huvutiwa na bodybuilding na ndo maana Wanawake wengi huwaogopa bodybuilder. Pengine wanaume tumetafsiri vibaya wanavyotuchukulia ndomana tukakimbilia gym.

Ni kweli wadada wanapenda amani moyoni wakiongozana na waume zao lakini sio lazima mpaka uwe mwili jumba. Mwanamke anaweza kupenda kuongozana nawe kwa ajili ya kujiamini kwako au uongeaji wako au uchangamfu.
5781035b51d7d8af770ea2392fc95b19.jpg
 
NA WEWE NI MWANAUME ILA UNAJUA KITU WANACHOPENDA KINA DADA??Mmmmh
 
Wewe lazima una kitambi. Sizitaki mbichi hizi. Tuache sisi wanyanyua vyuma na miili yetu. Tatizo liko wapi?
 
Mleta mada inaonekana anaogopa sana wanaume wenye miili jumba. Au walishamnyang'anya mke?
 
Wanaume tunadhani kwenda gym kutanua misuli basi mwanamke watadata. Tunajitahidi kuwa na six pack ili wanawake wachanganyikiwe na bodybuilding lakini ukweli ni kwamba mwanamke hivyo vyote havimpagawishi.

Ukweli ni kwamba, kiuhalisia mwanamke ni muoga Mara nyingi wanawake hawajiamini. Mwanamke anapenda akiongozana na mwanaume basi huyo mwaanaume awe na uwezo wa kumtetea akionewa. Wanawake hawapendi wanaume waliopoa au waoga hata wakiongozana nawe anakosa amani moyoni maana mwanaume niliye nae ni muoga hato nitetea nikipigwa.

Wanawake wanapenda mwnaume mwenye kujiamini, wanawake wanapenda wakiongozana na mwanaume barabarani wanavutiwa zaidi na mwnaume anayeongea kwa sauti(sio kupayuka) yaani aongee amsikie kwa ufasaha na sio kuuliza sijui umesamaje?

Sababu mwanamke kimaumbile ni muoga wakati mwingine anaogopa kukuuliza, na akishafanya hivyo basi hatofurahia maongezi maana hasikii unachosema. Kwani hujawahi ona unaongea afu mwanamke anatabasamu tu lakini ukimuuliza swali anashtuka kana kwamba mawazo yake hayapo hapo.

Sio ukweli kwamba wanawake huvutiwa na bodybuilding na ndo maana Wanawake wengi huwaogopa bodybuilder. Pengine wanaume tumetafsiri vibaya wanavyotuchukulia ndomana tukakimbilia gym.

Ni kweli wadada wanapenda amani moyoni wakiongozana na waume zao lakini sio lazima mpaka uwe mwili jumba. Mwanamke anaweza kupenda kuongozana nawe kwa ajili ya kujiamini kwako au uongeaji wako au uchangamfu.
5781035b51d7d8af770ea2392fc95b19.jpg
Cha ajab mambo ambayo wanawake inabid waseme unawasemea kanakwamba we ni mwanamke
Sasa we endelea kuwapa hella wengine tunapewa
 
Back
Top Bottom