Mwanamke Epuka mwanaume wa namna hii

Mwanamke Epuka mwanaume wa namna hii

Cybercurex

Member
Joined
Jan 19, 2023
Posts
98
Reaction score
238
Huyu si mwingine Bali ni mom's boy.

Hii ni term inayotumika kumwelezea mwanaume ambaye anamtegemea Mama yake katika umri ambao anatakiwa ajisimamie mwenyewe.

Ni mwanaume ambaye hawezi kufanya chochote bila kumshirikisha Mama yake.Ni kweli kuna mambo
yanahitaji ushauri wa wazazi lakini kuna mambo yanahitaji uamuzi binafsi au wa ushauri wa mwenza.

Huyu ni Mwanaume wa kuepuka sana katika mahusiano kwasababu ni dhahiri hawezi kuwa Baba/Mwanaume bora.sifa kuu ya Mwanaume ni uwezo wa kujisimamia vizuri.

Muda wote mama yake atakuwa na sauti kuliko yeye na hata mkewe. Maamuzi mengi huamuliwa na mama yake,kitu kidogo anakwambia ngoja nimuulize mama, jina la mtoto...hadi aamuulize mama kufanya biashara au mradi wowote hadi amuulize mama yake, akihitaji mtoto hadi amuulize bi mdashi,akipata shida kidogo kwa mama.

Kiufupi Mwanaume kama huyu hata kuoa na mwanamke yupi wa kuoa ni msukumo wa Mama yake.Yaani mama yake akisema simtaki mwanamke fulani,naye huyo anachana naye anamfuata anayemtaka mama
yake.

Mara nyingi hana siri,yaani yeye mambo ya faragha atamsimulia mama yake yote.Ukifuatilia kwa makini utagundua wengi wamekuwa hivyo kutokana na malezi waliyopata wakiwa wadogo.Na wengi bila shaka wanakuwa wamelelewa na mzazi mmoja yaani Mama.

Je, ulishawahi kukutana na Mwanaume au jamaa la namna hii

Karibu
 
Wanaume wengi ni watoto wa mama kama hujui...wamama wengi hu admitt kupendelea watoto kiume kuliko wa kike.....
Ni sawa ni watoto wa Mama hata wanawake pia. Nazungumzia wanaume ambao hawawezi kufanya maamuzi bila ridhaa ya mama zao.Yani mama mpaka ampe go ahead .Mambo ambayo hata yanayomhusu yeye na mwenzi wake anayapeleka kwa mama yake.
 
sawa,ila wa mama wanaspend /more /a lot of time raising kids,no wonder wanakua na strong influence on their kids, mimi sioni tatizo kama mtu anamuuliza mama yake kila kitu unless huyo mwenza wake ana interpret this as a sign of weakness, au mama in question ni mkorofi asiyempenda mkwewe.
 
Huyu si mwingine Bali ni mom's boy.
Hii ni term inayotumika kumwelezea mwanaume ambaye anamtegemea Mama yake katika umri ambao anatakiwa ajisimamie mwenyewe.

Ni mwanaume ambaye hawezi kufanya chochote bila kumshirikisha Mama yake.Ni kweli kuna mambo
yanahitaji ushauri wa wazazi lakini kuna mambo yanahitaji uamuzi binafsi au wa ushauri wa mwenza.

Huyu ni Mwanaume wa kuepuka sana katika mahusiano kwasababu ni dhahiri hawezi kuwa Baba/Mwanaume bora.sifa kuu ya Mwanaume ni uwezo wa kujisimamia vizuri.

Muda wote mama yake atakuwa na sauti kuliko yeye na hata mkewe. Maamuzi mengi huamuliwa na mama yake,kitu kidogo anakwambia ngoja nimuulize mama, jina la mtoto...hadi aamuulize mama kufanya biashara au mradi wowote hadi amuulize mama yake, akihitaji mtoto hadi amuulize bi mdashi,akipata shida kidogo kwa mama.

Kiufupi Mwanaume kama huyu hata kuoa na mwanamke yupi wa kuoa ni msukumo wa Mama yake.Yaani mama yake akisema simtaki mwanamke fulani,naye huyo anachana naye anamfuata anayemtaka mama
yake.

Mara nyingi hana siri,yaani yeye mambo ya faragha atamsimulia mama yake yote.Ukifuatilia kwa makini utagundua wengi wamekuwa hivyo kutokana na malezi waliyopata wakiwa wadogo.Na wengi bila shaka wanakuwa wamelelewa na mzazi mmoja yaani Mama.

Je, ulishawahi kukutana na Mwanaume au jamaa la namna hii

Karibu
Burna Boii.. Dangote.. list iendelee[emoji28][emoji28]

Kwa kifupi Mama zetu wanatufunza vyema Sana kuepukana na wanawake matapeli
 
Wapeni maua yao, wametafuta one to trust. Ambaye ni mama yake
Bora Mali na miradi uiache kwa mama sio pasua vichwa wa sku hizi unaeza andika mitoto kumbe yote sio yako
Kumuamini Mama ni kitu kizuri kaka,lakini kuna ile hali Maamuzi ya kiutu uzima hayaonekani. Kuna mtu anamtegemea mama yake kiasi kwamba siku asipokuwepo mambo yanaharibika kabisa.
 
Ni kila mtu na utashi wake wa kupembua mambo
 
Back
Top Bottom