Mwanamke Dar anywa sumu na kumnywesha pia mwanae

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
Mama afariki, mtoto aokolewa
Mwanamke mmoja amefariki dunia Jijini Dar es Salaam baada ya kunywa sumu ya panya ambayo pia alimnyesha mwanae mwenye umri wa miaka sita.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustine Shilogile amesema, tukio hilo la kuhuzunisha lilitokea jana mishale ya saa 8:00 mchana.
Amemtaja mwanamke huyo ambaye hivi sasa ni marehemu kuwa ni Samia Mwambata, 36, mkazi Ilala Mchikichini.
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Shilogile amesema mwanamke huyo alikunywa sumu hiyo ya panya Septemba 26 mwaka huu, na kisha akamnywesha mwanae aitwaye Leice Gerard, 6, kwa nia ya kumuua.
Amesema baada ya tukio hilo, mwanamke huyo na mwanae walikimbizwa katika hospitali ya Amana kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo amsema ilipofika jana mishale ya saa 8:00 mchana, mwanamke huyo alifariki dunia.
Amesema mwanae Leice, alitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani siku hiyo hiyo aliyonyweshwa sumu na mama yake.
Kamanda Shilogile amesema sababu za kifo hicho ni mwanamke huyo kuambiwa na ndugu zake kuwa ana tabia mbaya.
Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Amana na Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
http://ippmedia.com/
 
Ooooh my god mbona dunia ina matukio ya namna hii
ina maana ni ugumu wa maisha ndo inapelekea kujiua na kuua hata kiumbe kisicho na hatia :(
 
Mungu amlaze mahala pema peponi!

Jamani, huyu Mungu mbona tunampa kazi ngumu namna hii? Kila mtu alazwe mahali pema? Mahali pabaya atalazwa nani? Huyu kajiua na kibaya zaidi alidhamiria kumuua na mwanaye! Lol! Kajiamulia mwenyewe alazwe pabaya. Mungu ampe Maisha mema na bora mtoto aliyenusurika.
 
Jamani, huyu Mungu mbona tunampa kazi ngumu namna hii? Kila mtu alazwe mahali pema? Mahali pabaya atalazwa nani? Huyu kajiua na kibaya zaidi alidhamiria kumuua na mwanaye! Lol! Kajiamulia mwenyewe alazwe pabaya. Mungu ampe Maisha mema na bora mtoto aliyenusurika.
Mahali pabaya ni MAFISADI waliosababisha kifo cha huyu mama!!
 
So sad!! Kweli aliona hata mtoto wake akibaki duniani atateseka akaamua naye amnyweshe sumu. Yote haya yatokana na mzigo mkubwa wa matitizo na shida za kijamii. Kwa sasa matukio ya ajabu yatokanayo na matatizo ya kijamii yamekithiri. Wizara ya maendeleo ya Jamii + ustawi wa Jamii wanabidi wakae pamoja waone ni jinsi gani wanatakiwa kuwafikia wananchi kwa counselling!!! Wananchi wengi wamekata tamaa, crimes at peak, you name all.
 
Back
Top Bottom