Amejifungulia nyumbani? Hakuna maelezo ya mkunga/daktari? Hadithi ya kijinga kabisa.Hivi haya magazeti yanasimamiwa na chombo gani kuhakikisha yanatoa habari zisizopotosha?
Nilikuwa nataka kuuliza swali hilo hilo, huyu MziziMkavu huwa anavituko visivyo na ushahidi na wala sio mara ya kwanza kuleta uzi usiokuwa na mashiko. Binaadamu hawezi kuzaa mnyama au mnyama kuzaa binaadam.
Nyani Ngabu kuwadanganya watanzania wala sio kazi ilimradi tu uwaaminishe hata kama hukutoa ushahidi wataamini, ndio tabia za watanganyika wameshazoewea kudanganywa na wanapenda kudanganywa
yaani haya magazeti ya udaku kwa story za kutunga ni kiboko!, yaani nilivyokuja kwa speed kumuona huyo chatu kumbe wameweka tu picha za sijui wahanga wa mafuriko jangwani hao!!!
Nyani Ngabu kuwadanganya watanzania wala sio kazi ilimradi tu uwaaminishe hata kama hukutoa ushahidi wataamini, ndio tabia za watanganyika wameshazoewea kudanganywa na wanapenda kudanganywa
Lakini hiyo yote ni kwa sababu tunapenda kuendekeza ujinga.
Kwa mfano tu, ukitaka kuleta kizaazaa sehemu jaribu kuchukua paka halafu shingoni mfunge matambara halafu weka na kikaratasi chenye maneno ya Kiarabu (na si lazima hayo maneno yamaanishe chochote...unaweza ukaungaunga tu herufi, basi).
Halafu kabla watu wengine hawajaamka ile alfajiri kamtupe uani kwa mtu.
Hahahaaa.....naweza kukuhakikishia kuwa watu siku hiyo hawatalala. Wanaweza wakashinda hata kwa mganga wakijaribu kujua hayo maneno yanamaanisha nini.
Unaambiwa mtoto kazaliwa hospital lakini jina hospital hakuna hivi hizi enzi za utandawazi kweli azaliwe mtoto kama huyo hata wandishi wa habari wa magazeti makini wasijue lakini sishangai ndio udaku huo