Mwanamke auawa kikatili

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WATU watatu wamefariki katika matukio tofauti jijini Dar es Salaam likiwemo la mwanamke mmoja kuuawa kikatili na mwanaume anayesadikiwa kutafutwa na polisi.

Chanzo cha habari kinadai kuwa mwanamke huyo ambaye ni mkazi wa Kinondoni pia ni mke wa mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Muddy mwili wake ulikutwa ufukweni mwa bahari (Coco Beach) ukiwa umegongwa na kitu chenye ncha kali kichwani eneo la kisogoni huku sehemu ya tumbo ikiwa imekatwa na kusababisha utumbo kutoka nje.

Mmoja wa ndugu wa maraehemu ambaye hakupenda kutajwa jina lake alisema kuwa marehemu alitoweka nyumbani kwake wiki iliyopita bila kutoa taarifa jambo lililowafanya wamtuhumu mume wa marehemu (Muddy) kuwa alihusika na upotevu wa marehemu huyo.

Alisema baada ya shutuma hizo Muddy alichukua jukumu la kwenda kituo cha polisi na kutoa taarifa za kupotelewa na mkewe katika mazingira ya kutatanisha.

“Baada ya taarifa hiyo, jeshi la polisi lilipookota mwili huo lilimpigia simu mume wa marehemu huyo na kufika katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili kutambua mwili uliookotwa ufukweni mwa bahari na alibaini kuwa ni wa mke wake,” alisema.

Akizungumza jana na waandishi wa habari Kamanda Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alikiri kuokotwa kwa mwili wa mwanamke huyo huku ikisadikiwa mwanaume anayetafutwa na jeshi hilo kwa mauaji ya wanawake watano ndiye aliyehusika na mauaji hayo.

Alisema kuwa baada ya uchunguzi uliofanywa na polisi kwa kushirikiana na madaktari wa hospitali ya Mwananyamala unaonyesha kuwa kabla ya kuuawa marehemu alifanyiwa mapenzi kinyume na maumbile na vitendo vingine vya kikatili.

Kenyela alisema mwili wa marehemu umesafirishwa jana kuelekea Moshi vijijini eneo la Kilema mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi huku jeshi la polisi likiendelea kumsaka mwanaume aliyehusika na ukatili huo.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kuwa mwanaume huyo mpaka sasa anakadiriwa kuua wanawake watano katika kila mwezi.
 
wakiambiwa wawe waaminifu katika ndoa zao hawasikii! huyo muuaji akipatikana anatakiwa kupewa nishani ya heshima ya juu ya mlima kilimanjaro kwa kuwashikisha adabu wanawake vicheche walio kwenye ndoa! dunia hii ni ya wanaume bwana, wanawake tuacheni tule nchi msijilinganishe na sisi!
 
Mbona unahukumu kabla ya kujua kuwa huyo mwanamke hakuwa mwaminifu? Tuwe na uhakika ndipo tulaumu. Wote wanaouwawa wanakuwa sio waaminifu? Hutendi haki hata kidogo!!!!!!!!!
wakiambiwa wawe waaminifu katika ndoa zao hawasikii! huyo muuaji akipatikana anatakiwa kupewa nishani ya heshima ya juu ya mlima kilimanjaro kwa kuwashikisha adabu wanawake vicheche walio kwenye ndoa! dunia hii ni ya wanaume bwana, wanawake tuacheni tule nchi msijilinganishe na sisi!
 
wakiambiwa wawe waaminifu katika ndoa zao hawasikii! Huyo muuaji akipatikana anatakiwa kupewa nishani ya heshima ya juu ya mlima kilimanjaro kwa kuwashikisha adabu wanawake vicheche walio kwenye ndoa! Dunia hii ni ya wanaume bwana, wanawake tuacheni tule nchi msijilinganishe na sisi!

haaaa niwewe nini?we hujajua anatumia vigezo gana kuwapata,na mbona wengine ni wanafunzi?
 
haaaa niwewe nini?we hujajua anatumia vigezo gana kuwapata,na mbona wengine ni wanafunzi?

hahahaa, ningekuwa mimi mbona ningeringa?? huyu jamaa bomba sana, na vichece wa kwenye ndoa shikeni adabu zenu, jamaa namfagilia sana tuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom