Mwanamke auawa, achunwa ngozi Mbeya

Mwanamke auawa, achunwa ngozi Mbeya

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

Barakaeli-Masaki.jpg

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakaeli Masaki

Na Pendo Fundisha, Mbozi

WATU wasiofahamika wamemuua mwanamke mkazi wa Kijiji cha Idiwili, Kata ya Iyula wilayani Mbozi na kumchuna ngozi ya shingo.

Pamoja na kumchuna ngozi marehemu, wauaji hao pia walinyofoa macho, ulimi na koromeo la marehemu.

Baada ya mauaji hayo ya kinyama wauaji hao waliutelekeza porini mwili wa marehemu huyo, Angelina Kameza (26).

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakaeli Masaki alisema:

"Tumepokea taarifa ya mauaji hayo ya kinyama lakini bado tunaendelea na upelelezi kujua chanzo chake ni kipi.

"Hatuwezi kuhusisha tukio hilo na imani za ushirikina kama baadhi wanavyosikika ila uchunguzi unafanyika kwa kuwa mwili wa marehemu ulikutwa hauna baadhi ya viungo.

"Lakini uchunguzi wa awali unaonyesha marehemu alikuwa katika ndoa ya wanawake sita baada ya kuolewa na mwanaume mwenye umri wa miaka 70 aliyezaa naye watoto wawili.

"Kabla ya kuolewa na mzee huyo, enzi za uhai wake aliolewa na mwanamme mwingine aliyefariki dunia katika mazingira yanayofanana na haya kwani naye alinyofolewa baadhi ya viungo vya mwili vikiwamo macho, ulimi na koromeo," alisema Kamanda Masaki.

Aliwataka wananchi kutoa taarifa katika vyombo vya dola watakapopata taarifa za wauaji hao.

CHANZO:Mtanzania
 
Yale mambo ya Mbozi ya miaka ile yamerudi tena..???!!! jamani kwani huko hakuna mamba..??! si mkawachune hao...?
 
Sasa naanza kuamini kuna baadhi ya watu(binaadamu) na wanyama ukiwalinganisha, basi wanyama wana akili sana kuliko baadhi ya watu(binaadamu)
 
Kule kuchunwa ngozi,kupigwa nondo za kichwa huku albino na vikongwe hawana amani,binadamu ni viumbe wa ajabu sana.
 
Uchaguzi mkuu mwakani majanga yameanza kuonekana mapemaa, maalbino kuumiwa na haya ya kuchunwa ngozi, hizi imani hapa ni shida nchi hii.
 
Haswaaa - Adui mkubwa wa walio wengi, tena hata baadhi ya wasomi wakubwa, ni imani potofu za kishirikina.
 
Duh maskini mtoto wa watu!

Wazazi wake nawapa pole ya kutoka moyoni kwangu
 
Sure.. .but whl women.....kila story sikuizi wanawake ...jaman tutaisha
 
Aliwataka wananchi kutoa taarifa katika vyombo vya dola watakapopata taarifa za wauaji hao.

Hebu angalia conclusion ya kamanda wa Polisi....!!!
 
Tumeshazoea kuchukulia poa issues za washika dau wao...
Ila wanajua kufuatilia habari za akina mchange dhidi ya wanaharakati wema.
That is nonsense men!
 
Taarifa za polisi huwa zna utata sasa, unakaa kwamba sio ushirikina, lakini maelezo yako yote yanatoa picha kuwa ni mambo ya kishirikinaaaa

Barakaeli-Masaki.jpg

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakaeli Masaki

Na Pendo Fundisha, Mbozi

WATU wasiofahamika wamemuua mwanamke mkazi wa Kijiji cha Idiwili, Kata ya Iyula wilayani Mbozi na kumchuna ngozi ya shingo.

Pamoja na kumchuna ngozi marehemu, wauaji hao pia walinyofoa macho, ulimi na koromeo la marehemu.

Baada ya mauaji hayo ya kinyama wauaji hao waliutelekeza porini mwili wa marehemu huyo, Angelina Kameza (26).

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakaeli Masaki alisema:

"Tumepokea taarifa ya mauaji hayo ya kinyama lakini bado tunaendelea na upelelezi kujua chanzo chake ni kipi.

"Hatuwezi kuhusisha tukio hilo na imani za ushirikina kama baadhi wanavyosikika ila uchunguzi unafanyika kwa kuwa mwili wa marehemu ulikutwa hauna baadhi ya viungo.

"Lakini uchunguzi wa awali unaonyesha marehemu alikuwa katika ndoa ya wanawake sita baada ya kuolewa na mwanaume mwenye umri wa miaka 70 aliyezaa naye watoto wawili.

"Kabla ya kuolewa na mzee huyo, enzi za uhai wake aliolewa na mwanamme mwingine aliyefariki dunia katika mazingira yanayofanana na haya kwani naye alinyofolewa baadhi ya viungo vya mwili vikiwamo macho, ulimi na koromeo," alisema Kamanda Masaki.

Aliwataka wananchi kutoa taarifa katika vyombo vya dola watakapopata taarifa za wauaji hao.

CHANZO:Mtanzania
 
mkoa wa mbeya una maajabu sana.
ndio mkoa unaongoza kwa kuwa na uwingi wa makanisa ya kilokole.asilimia kubwa ya wakazi wa mkoa huo hujifanya wameokoka na wanahofu kubwa sana ya mungu.lakini pia ndio mkoa unaoongoza kwa matukio ya ushirikina na mauaji ya kutisha kama hili la wachuna ngozi.
 
Mkoa wa Mbeya naona umelaaniwa ule kwani maovu na laana nyingi hapa Tanzania zinaanzaga kule.
 
Strange amekufa kifo kama alichofariki mume wake wa kwanza kabla hajaolewa na babu kizee wa miaka 70
 
Back
Top Bottom