Mwanamke aua mtoto wa mke mwenzake na kutumbukiza mwili kwenye karo ya maji

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,505
13010768_1495669770447436_4938229566484650166_n.png

Mwanamke mkazi wa Mlimwa, Dodoma, Fatuma Mohamed, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wa mke mwenzake, kisha kutumbukiza mwili wake kwenye karo la maji.

Mtoto aliyeuawa, Subira Ganyara mwenye umri wa mwaka mmoja, aliibwa Aprili 19 nyumbani kwa mama yake Agnes Yohana saa 3 usiku wakati akiwa amelala chumbani.

Mtoto huyo alipatikana akiwa amenyongwa na kutumbukizwa kwenye karo la maji lililokuwa wazi.

========================

MWANAMKE mkazi wa Mlimwa katika Manispaa ya Dodoma, Fatuma Mohamed (39), anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wa mke mwenzake, kisha kumtumbukiza mwili wake kwenye karo la maji.

Mtoto aliyeuawa, Subira Ganyara mwenye umri wa mwaka mmoja, aliibwa Aprili 19 nyumbani kwa mama yake mzazi, Agnes Yohana saa 3:00 usiku wakati akiwa amelala chumbani, wakati mama yake akiongea nje na wenzake. Mtoto huyo alipatikana Aprili 20, alfajiri akiwa amenyongwa na kutumbukizwa kwenye karo la maji lililokuwa wazi.

Akielezea tukio hilo, baba wa mtoto huyo, Prosper Ganyara alisema mtoto aliyeuawa alizaliwa Machi 23, 2015. Alisema, mtuhumiwa ni mkewe waliyebahatika kupata watoto watatu, Kabuche Ganyara (13), Ganyara Ganyara (11) na Msafiri Ganyara (7).

Alisema, alifunga ndoa ya Kiislamu na mwanamke huyo lakini hata hivyo ndoa hiyo ilivunjika mwaka 2013 baada ya kukosa maelewano, ndipo alipoanza kudai mahakamani haki ya kuchukua watoto wake ili awatunze lakini, baada ya kesi hiyo kusikilizwa Mahakama ilimpa Fatuma (mtuhumiwa) haki ya kutunza watoto wake.

Alisema, aliamua kukata rufaa Mahakama ya Mkoa Januari mwaka huu ili apate haki ya kulea watoto wake na sasa kesi hiyo bado iko mahakamani. “Mimi nikapata mwanamke mwingine Agness (mama wa mtoto aliyeuawa) nikaenda kwao kujitambulisha na wakati huo yatari alikuwa mjamzito tukakubaliana aendelee kukaa kwa wazazi wake na mimi nitatoa matunzo yote,” alisema baba wa mtoto huyo.

Alisema juzi kati ya saa 2.30 usiku, mama wa Subira alikuwa amekaa pembeni ya nyumba yao akiwa anaongea na wenzake, baada ya mazungumzo aliingia ndani akakuta mtoto hayupo akawauliza majirani wakasema hawajui.

“Wakaanza msako wa kutafuta mtoto usiku ule ule na alipoulizwa ni nani anaweza kuhusika akasema ni mke mkubwa kwani mara nyingi amekuwa akimtolea maneno ya vitisho kuwa kama asipokufa yeye atakufa mtoto,” Gunyara alikariri maneno ya mzazi mwenzake na kukiri hata yeye aliwahi kutolewa maneno hayo.

Pia alisema Fatuma aliwahi kumfuata mama mzazi wa Agness, Esther Udoba akilalamika kuwa mtoto wake ameolewa na mume wake na hivyo ni heri waachane kwani atamuua.

“Hata baba mzazi wa Agness aliwahi kumtolea maneno mazito na kumtolea matusi, nikamshauri akirudia tena atoe taarifa Polisi na mimi nitakuja na nakala ya talaka kama kielelezo kuwa tayari nilikuwa nimeachana na mwanamke huyo,” alisema mwanamume huyo. Alisema walipanga wakutane wazazi wa Agness, Agness, Fatuma na yeye lakini kabla ya hilo halijafanyika ndio tukio hilo limetokea.

Chanzo: Habarileo
 
View attachment 341588

Mwanamke mkazi wa Mlimwa, Dodoma, Fatuma Mohamed, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wa mke mwenzake, kisha kutumbukiza mwili wake kwenye karo la maji.

Mtoto aliyeuawa, Subira Ganyara mwenye umri wa mwaka mmoja, aliibwa Aprili 19 nyumbani kwa mama yake Agnes Yohana saa 3 usiku wakati akiwa amelala chumbani.

Mtoto huyo alipatikanaakiwa amenyongwa na kutumbukizwa kwenye karo la maji lililokuwa wazi.
mama weee kisa si angemuua huyo mwanaume mtoto mchanga amekosa nini? aisee sijui inakuwaje mtu unakuwa na roho ya kikatili hivi
 
View attachment 341588

Mwanamke mkazi wa Mlimwa, Dodoma, Fatuma Mohamed, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wa mke mwenzake, kisha kutumbukiza mwili wake kwenye karo la maji.

Mtoto aliyeuawa, Subira Ganyara mwenye umri wa mwaka mmoja, aliibwa Aprili 19 nyumbani kwa mama yake Agnes Yohana saa 3 usiku wakati akiwa amelala chumbani.

Mtoto huyo alipatikanaakiwa amenyongwa na kutumbukizwa kwenye karo la maji lililokuwa wazi.
Kwa Mwanamke sishangai kilichotokea, Hawa wenzetu wana majabu mioyoni mwao
 
Maswali mengine siyo mazuri kuuliza......eti wee mwanamke aliyekuwa anagegedwa ni mke mwenzio au hako kachanga(r.i.p)????
 
R.I.P katoto inasikitisha sana. lakiniJamani ee mambo mengine yanasababishwa na insanity. Mnalaumu wanawake wee mnajua huyo mama yamemkuta yapi? Labda amepata msongo wa mawazo uliovuruga akili zake. Labda huyo Anyesi alikuwa mchepuko then akasababisha ndoa ya mwenzake ivunjike maumivu juu ya maumivu akajikuta hawezi tena kukaa na watoto wake. Simtetei lkn mambo mengine yakikukuta km hauna stable mind lazima uwe lunatic..
 
There is nothing like lunacy here. Wivu wa kijinga pamoja na ushetani. Nashauri watu wasiwe wanaingilia ndoa za wenzao. Na kama zitaingiliwa watoto wasihusishwe.
 
Jaman mwisho wa dunia umefik binadam wameku na roho mbay kuliko ht wanyama
 
Back
Top Bottom