Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,087
- 34,884
MWANAMKE mmoja Saida Hassan [26] amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kutelekeza kichanga cha siku 9 katika nyumba ya moja ya kulala wageni jijini Dar es Salaam. Mwanamke huyo ambaye ni mkazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jana kujibu tuhuma hiyo inayomkabili.
Ilidaiwa mbele ya hakimu Frednand Kiwonde na Mwendesha Mashtaka Inspekta wa Polisi, Benedict Nyagabona kuwa mshitakiwa alitelekeza kichanga hicho gesti Juni 22 mwaka huu.
Ilidaiwa kuwa mshitakiwa kwa makusudi kabisa alimtelekeza mtoto huyo wa kike aliyekuwa na siku 9 kwenye gesti hiyo.
Ilidaiwa kuwa mama huyo alifika kwenye gesti hiyo na kujifanya kama anahitaji chumba na kupatiwa na kisha asubuhi kuondoka na kukiacha kichanga hicho kwenye chumba hicho.
Taarifa za kutelekezwa kichanga hicho zilifika polisi na msako mkali ulifanyika na mmoja wa wana ndugu wa mwanamke huyo aligundua kuwa ni ndugu yake huyo ndiye atakuwa mtuhumiwa kwa kuwa kwa siku hiyo hakuonekana na kichanga hicho.
Mwanamke huyo alichukuliwa na kuhojiwa na kugundulika kuwa yeye ndiye alikuwa mtuhumiwa wa kutelekeza kichanga hicho.
Hivyo mshitakiwa alikana shtaka na kesi kuahirishwa hadi Agosti 5 mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2653894&&Cat=1