Mwanamke apooza mwili baada ya kufikishwa kileleni

Mwanamke apooza mwili baada ya kufikishwa kileleni

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
7,147
Reaction score
14,708
2.jpg


Lucinda Allen (pichani juu) kutoka Stourbrige alipooza mwili wake baada ya kufikishwa kileleleni (orgasm) kulikosababisha damu kuvuja ndani ya ubongo (brain hemorrhage) wakati akifanya mapenzi. Lucinda anatumia kiti cha magurudumu (wheel chair) baada ya kupooza chini upande wa kushoto wa mwili wake, tukio lililotokea baada ya kupata maumivu ya kichwa wakati wa tendo hali iliyomwacha kwenye maumivu makali.

1.jpg

Lucinda (kwenye wheelchair) akiwa na mumewe pamoja na binti yao

Lucinda mwenye miaka 43, alikuwa mjamzito wakati hali hiyo inamtokea, alikimbizwa hospitali akiwa amepoteza fahamu (coma), ana likaa katika hali ya coma kwa siku sita wakati madaktari wakimfanyia operesheni maalum ya fuvu (craniotomy) ili kupunguza pressure kwenye ubongo wake.

3.jpg

Picha hii inaonesha operesheni maalum ya fuvu (craniotomy)

Ilikuwa ni habari njema pale alipoamka kutoka kwenye coma na kuambiwa kuwa mtoto wake tumboni hakudhurika. Miezi mitatu baadaye alijifungua mtoto wa kike, Marri-Alice, mnamo Novemba 2012.

Kwa sasa Lucinda anataka kuzindua kampeni dhidi ya matatizo haya yanayoonekana kupuuzwa, yaani kuumwa kichwa baada ya kufika kilele (orgasm).

“Hakuna mtu anayeongea kuhusu tatizo la kuumwa kichwa baada ya mtu kufika kileleni,” Lucinda aliliiambia gazeti la Mirror, la Uingereza.

Madaktari walisema kuwa Lucinda alipata kiharusi mara tano ambacho wanaamini kilisababishwa na matatizo ya kuzaliwa ya kwenye mishipa ya damu ambayo pia yalimsababishia maumivu ya kichwa baada ya kufikia kilele cha utamu…
 
Ila kileleni noma sana. Ukifika utasikia mwili unazizima ganzi si ganzi loh. Kumbe wengine wanapooza kabisa.
Hicho kitu hakielezeki ndio maana huwezi kuwa salama pande hizo
 
tusipowafikisha wanalalamika......tukiwafikisha matokeo yake ndio kama hayo.
 
Back
Top Bottom