Mwanamke anayejiweza kimaisha

  • Thread starter Thread starter JS
  • Start date Start date
if you say so....!
 


heeii...ngash2ka mbee...lol
 
Teamo ....................huo u enginer wako uliupata kwa kufata theory na data za Mbongo au Muafrika? Usikute huyo mwalimu wako kasoma huko huko kwa wazungu ndo akaja kukufunza wewe!

Waafrika hatuna tabia ya kudocument vitu na wala kuvi publish ( visingizio kuwa vyuo havina pesa), kwa nini tusifanye reference vitu ambavyo vimekubalika duaniani lkn tukubali maneno matupu ya Muafrika!?

BOXI walibeba na kurudi bongo wakawa walimu wenu vyuo vikuu................ukitaka usitake mkuu theory za mzungu na experimental results zake unazifuata tu
 
VERY UNPRACTICAL!....
wadanganye wanao danganyika!
mi sidanganyiki kwa ma-journal ya ajabu ajabu

Basi wewe una lako jambo. Si muda wote unahangaika na scientific proofs? Zimewekwa hapo halafu unahaha kutafuta mlnago wa kutokea!!!!:disapointed:
Soma hapa?
 
Successive marriages ni zipi?

Unawezaje kuijua successive marriage ya mtu mwingine? Kuna wanandoa unawaona wanatembea na kucheka kwa furaha mbele za watu wakiwa nje........ Wanapokuwa ndani.......Lakini laiti kuta zingekuwa zinasema ungeshangaa ya kusikia........
 
Kwa kawaida pesa haiwezi kuchukua nafasi ya mwanaume. Ni kweli baadhi ya wanaume wanaogopa kuoa wanawake wenye pesa na wapo wanaume wanaotaka kuoa wanawake wenye pesa.Mwenye kuamua uolewe au usiolewe ni wewe mwanamke kwa namna utakovyo kuwa unaishi ikiwa pamoja na kauli zako katika harakati za maisha. Nijuavyo mimi kwenye ndoa hatuoi au kuolewa na pesa, elimu, ama social status.Tunaoa au kuolewa na mtu (personality) tukitegemea maisha yenye furaha, Kwa sababu kufurahi ndicho kitu kinachopendwa na wengi.Mtu anaweza kuoa mwanamke asiye na pesa asipate furaha.Kwa sababu kufurhi ni pamoja na kuthibitisha kuwa wewe ni mwanamke au mwanaume kwelikweli, uthibitisho kuo huanzia kwenye ndoa na unaextend kwenye mambo mengine.Kuwa na pesa bila mume haviwezi kukuletea furaha.Ndoa ni jambo muhimu sana liletalo furaha ikitokea umeolewa au kuoa the right man or woman respectively. Kwa mwanamke mwenye pesa, endelea kutafuta pesa, ishi maisha yenye staha, tawala pesa zako, usitawaliwe na pesa, ishi simple life, usinjionyeshe kuwa unapesa, wala unahitaji la kuolewa. Wapo wanaume wa maana wanaotaka wanawake wa aina hiyo, watakufuata, na wewe usijirahisi walakuwa mgumu sana.Test to prove mtu anakuhitaji wewe na siyo pesa zako maana lolote laweza tokea kwenye maisha pesa zikaisha.Kama mtu kakuoa wewe na siyo pesa, pesa zikiisha wewe unaendelea kuwepo na ndoa inadumu na akioa pesa zako na siyo wewe pesa zikiisha na ndoa inaisha.
 

JS vipi tena! mapenzi kama yapo ya kweli kabisa hujali kwamba huyo umpendaye ana mapesa kiasi gani awe mwanamke au mwanaume, lakini kama unafuata penzi la pochi basi hapo kuna tatizo na mara nyingi penzi halitadumu kwa muda mrefu hasa ikitokea michuzi ikiamua kuingia mitini.

Kama jamaa hana hata kazi ya kuweza kujitimizia mahitaji yake muhimu na kukutegemea wewe kwa kila kitu basi hapo kuna tatizo tena kubwa vinginevyo ni poa tu.

 
Unaweza kurudia tena hapo? Pesa ni kitu kingine bana. On the other side of the coin, kama mwanamke hana kazi ya kuweza kujitimizia mahitaji yake bado ndoa inadunda.

Hoja imerudi pale pale, mwanamke akikuzidi kipato ni hatari kwa ndoa yako. Nazungumzia uzoefu, Teamo usiniulize scientific proof hapa tafadhali.
 
VERY UNPRACTICAL!....
wadanganye wanao danganyika!
mi sidanganyiki kwa ma-journal ya ajabu ajabu



hivi huyu journal zake ni magazeti ya Shigongo?
 
Inategemea na jinsi makuzi yako yalivyokuwa wengine dada zetu mkiwa na uwezo tu hata ukisalimiwa kujibu mpaka umthathimini juu mpaka chini sasa hapo inabidi tukuogope
 
hivi huyu journal zake ni magazeti ya Shigongo?

hahah kaizer bwana ...................labda yeye jornals zake ni 'hansad' za vikao vya bar 😛 (sehemu ile huwa na knowledge kubwa sana ambayo huwezi kui tap kwenye journal tu)

asprin........................mimi sikuulizi na nakubaliana na uzoefu wako japo sio kwa wanaume wote 😀
 
Nimesoma post zote hakuna hata mdada mmoja alie sema kua yeye kamzidi uwezo mumewe na mambo yanaenda! So JS utampata wa level yako!
 

Kwa kawaida katika mila nyingi mwanaume ni mtawala wa nyumba ukiachilia kwa ndugu zetu kina Msimbe ambao huwa wanatawaliwa. Kuatwala maana yake kuwa safi katika nyanja zote. Inapotokea mwanamke kuwa na hali njema ya kipato kuliko mwanaume inakuwa tayari tatizo la kisaikolojia. Huyo mwanaume hata kama hata nyanyaswa atahisi kuwa ananyanyaswa. Kwa hali ya kawaida kuna uwoga kwa wanaume wengi kuoa wanawake kama hao.

Mie niliapa siwezi kuoa mwanamke eti kwa uzuri wake bali awe na hali nzuri ya kiuchumi na akili. Kwa kweli hiyo imenisaidia sana. Leo nakamua na kakazi kangu kazuri Senior Lecturer Chuo Kikuu flani nje ya nchi na mama Senior HR katika sekata flani hapo bongo. Uendeshaji wetu wa familia umekuwa rahisi na mzuri sana kwa wote tunashirikiana in terms of kipato.

Jiulize kwanini maprofesa wengi wake zao ni mama wa nyumbani au wallimu wa upe?
 
kwa jinsi ilivyo kujua successive marriages,ndio hivyo hivyo ngumu kuthibitisha hilo mnalolitetea!
 
sasa hapo ndio hoja inapolala!
swala nI:
1)kutokuwa na kazi
2)kuzidiwa kipato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…