Mwanamke anayejiweza kimaisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke anayejiweza kimaisha

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by JS, Aug 5, 2010.

 1. JS

  JS JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wandugu za leo,

  Hivi ukikutana na mwanamke umempenda na unatamani awe wako wa milele (kumuoa) lakini unakuta bahati nzuri (au mbaya kwa wengine) huyo mwanamke yuko safi kimaisha kazi nzuri kama pesa anazo kama mali anazo pia (sio hawa wamama watu wazima hapana wadada tu wenye umri unaofaa kuolewa) utamuoa hata kama wewe huna thamani ya kiuchumi aliyo nayo?

  kwa nini nimeuliza hivi, kwa sababu katika mazungumzo ya kawaida tu jana kuna rafiki yangu akaniambia watu wataogopa kutangaza nia kwangu nikiendelea kujijenga kimaisha and it got me thinking.

  Sasa wanaume utamuoa tu huyo dada hata kama wewe hali yako si fresh? na wadada utakuwa bread provider kwa huyo mumeo? mapenzi yana nafasi yake na pia uwezo kiuchumi una nafasi. zamani haikuwa hivi lakini kadri siku zinavyozidi kusonga mbele mambo yanabadilika
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Aug 5, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Haya bana.....
   
 3. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kama ulivyosema, mapenzi yana nafasi yake na mali zina nafasi yake. Kama huyo dada ana nafasi ya kujiimalisha ki-kipato yeye ajiendeleze tu. Aendelee kumwomba Mwenyezi Mungu kama ni wa kuolewa ataolewa tu, bwana awe na pesa za kumzidi na au hata kama hana pesa kabisa, kama wakipendana wataoana, na yeye kama ni mjasiriamali atamfundisha mume wake jinsi ya kupata pesa kama ni elimu yake ndo inamfanya afanikiwe basi itabidi amsaidie mume kwa kumpa mtaji na yeye angalau apate vijisenti. Pesa ni pesa na mapenzi ni mapenzi, mapenzi hayachagui tajiri au masikini yenyewe yapo tu. Achana na hiki kitu kinaitwa mapenzi, hata uwe na pesa kiasi gani kama hauna mapenzi ni bure. Na yeye pia hasiogope kutafuta pesa eti kisa hatapata mume. Je? Hakiacha kutafuta hizo pesa na mume pia hasijitokeze? Haoni kuwa atakuwa amekosa bara na pwani!!!!
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wadada wenye pesa na hali nzuri mm nawaogopa sana.
  Kuna ndugu na rafiki zangu kadhaa walibahatika kuoa wadada wa design hii leo wanalia na kusaga meno, wadada tuongee ukweli wakiwa na pesa na wakiolewa jamaa kaja kaona mafanikio kama hayo jiulize nn kitatokea kwa mdau??? Muulize Teamo na Asprin
   
 5. JS

  JS JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wewe binadamu long time no see upo?
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  JS wengi watakuogopa lkn atatokea tu 'jasiri' akupende Kama ulivyo na mali mali zako. Na atakuendesha na kuwa kichwa ya familia bila ya kuudhiwa na Mali zako

  kaza buti mwaya..... Jijenge usisubiri kuolewa
   
 7. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Fidel hapo umenena.Wadada wa siku hizi hasa wenye nazo ni matatizo mtindo mmoja na wengi hawana heshima kabisa,unaweza kuwa nae kwa mapenzi yote lakini mwisho wa siku atakuja kukuumiza tu na inapofikia mkigombana ndio kabisa atakwambia uchukue time kwani hana shida na wewe ulikuwa ni mzigo kwake.
  Kwanza wadada wa dizaini hii huwa ni ngumu sana kuolewa na hata kudumu katika mahusiano.
   
 8. RR

  RR JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Men are scared to bet on their balls :A S wink:
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Aug 5, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Aaah nipo bana lakini ndo hivyo nimefulia....

  Halafu kumbe una hela wewe eeeh.....saidia maskini basi hapa....
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahahahaha mzee unatangaza njaa kabisa.
  Angalia hawa wenye mkwanja huwa wanyanyasaji sana hawakawii kukutupia vilago.
   
 11. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  sasa hivi mie natamani ningejijenga kabla ya kuolewa, ukishaolewa mambo yataenda cvyo ndivyo kabisa, majukumu yanakuwa mengi sana sasa hivi nafanya mambo mengi pesa kidunchu bac full mawazo...jijenge JS atatokea mpenda maendeleo mwenzio mtaenda sawa kabisa.
   
 12. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  sio wote na wengine mnasababisha nyie, ukae kwangu nikusaidie hili na lile bado nijue unanichezea rafu...nakutimua faster.
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Aug 5, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hawa wenye kisu inabidi uwe mjanja jinsi ya kudili nao....unamtumia kwa muda tu halafu unasepa. Ukiweka maskani kwa muda mrefu watakufanya mtumwa....ogopa sana hawa kina JS...
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Atatumia pesa yake kama bakora kukuadhibu na kama ndo unaishi kwake dah unakuwa mtumwa nimeshuhudia jamaa zangu
   
 15. JS

  JS JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  I beg to contradict with your view. Sio wote wenye nazo wana matatizo. unajua pia inategemea na mtu.
   
 16. JS

  JS JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sina hela ila naweza kushare na wewe chochote nilichonacho
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Gaijin, asikwambie mtu, the more successful a woman becomes, the lesser chance of having a right candidate. Hii ni nature yetu wanaume kwani pamoja na mapenzi kuna ile sense ya kuwa protector inakufa kama mamaa yuko mbali kiuchumi

  fikiria jinsi hata kwenye common society inavyokua ngumu watu ku-accept kwamba a woman may have more colors, utasikia ah jamaa yuko poa ila ni mama ndiye mwenye show na jamaa analishwa tu, au ansomeshwa na mkewe nk. being an african man inakua "ngumu kumeza" inapotokea mie ndo mdakaji

  Its true JS kwamba the more successful you become ndipo unapopunguza choices za majamaa
   
 18. JS

  JS JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Fidel mwaya usimsikilize NN wewe kama kuna demu umempenda mtokee tu na umuoe kama una nia hiyo
   
 19. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  mimi siamini kabisa kama hiyo kauli yako inaukweli, mtu anaweza kukukatisha tamaa tu kuwa ukwa umejijenga sana wanaume watakuwa wanakuogopa.Si kweli ila unachotakiwa kuwa makini ni kuhakikisha mwanaume anayetangaza nia kwako awe na upendo wa dhati na sio upendo wa mafanikio yako.
  Lakini kubwa zaidi ni hii tabia yenu wadada wa Kibongo kuona aibu ya kumwambia mwanaume unayevutiwa nawe ukweli kabla ya yeye kukutangazia nia (kama na yeye anavutiwaa na wewe)
  If some man caught your eyes,heart & mind, u better go and tell him.
   
 20. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  sio wote wapo hivyo jamani, wengine wana mapenzi ya kweli...JS uckate tamaa kusaka mafaranga kisa utachelewa/wataogopa kukuoa....saka mafaranga kwa bidii zote utakutana na mwenzio anaekuona anafaa sio hawa wa kujishtukia.
   
Loading...