Mwanamke aliyeumizwa pita hapa ufarijike

Mwanamke aliyeumizwa pita hapa ufarijike

Ukiona jitu zima linatafuta mke, mume . Kwenye jf , Facebook, kanisani,msikitini nk, jua ana matatizo na sifa mbaya ktk jamii inayomzunguka. Ninadra sana kuishi .

Wewe unasifa nzuri? Lugha uliyotumia inatosha kubaini tabia yako..halafu kama jambo halikuhusu si lazima uchangie...hata mpumbavu akinyamaza huonekana kuwa ana hekima.
 
Habari wana jamvi wote.
Natafuta mwanamke aliyeumizwa kwenye mahusiano, nataka aliye umizwa kwa sabbu anajua uchungu wake naamini hawezi niumiza.pia kama unasifa na hujawahi kuumizwa lkn upo serious pia unakaribishwa. lengo langu ni kuuanza safari mpya ya mahusiona na kufarijiana. Namaanisha kuanza nae maisha ya ndoa.

Mimi ni mwanaume WA miaka 37, elimu degree,kazi nimejiajiri,naishi moro, kabila mnyamwezi, dini mkristo, mrefu na mwili WA wastani.

Mwanamke nimtafutae awe yuko hiv, miaka kat ya 30 mpaka 42, elimu yyte mwenye shughuli ya halali ya kumpatia kipato, kabila lolote, dini mkristo na kama si mkristo awe tayari kubadiri, asiwe mfupi sana, mcheshi, anayejua uchungu WA kusaritiwa. Aliyetayari anifuate pm.
Nipo serious naomba mizaha isipate nafasi.
Karibuni.


Wadau nimekuja tena, lkn safari hii lengo langu ni kuleta mrejesho.

Kwanza niwashukuru wote kwa kuchajia na kunitia moyo.

Pili niwashukuru wote waliokuja pm na kukosa vingezo, nipende kuwatia moyo wasikate tamaa.

Hatimaye nimefanikiwa kumpata niliyekuwa namtafuta...tunaendelea na mipango mingine ya kufahamiana zaidi then process zianze.
Asanteni sana
 
Nalia kwa mashart na vigezo kunitupa mkono,
Anyway Mungu awatangulie na kuwaongoza.vyema
 
Back
Top Bottom