SoC03 Mwanamke akiwajibika, jamii nzima inawajibika

Stories of Change - 2023 Competition
Jul 5, 2023
5
6
Utangullizi

Wanaweke wakiwezeshwa wanaweza, walisikika mabinti wakipaza sauti zao katika ardhi ya Tanzania, waliotamani kwa muda mrefu kutimiza semi zisemazo ukimwelimisha mwanamke umeelimisha jamii nzima, mwanamke akiwajibika jamii nzima inawajibika na ukimkomboa mwanamke katika maradhi, umaskini na ujinga umekomboa jamii nzima, walipaza sauti hizi wakitambua kuwa jamii nyingi duniani, Africa na katika jamii ya kitanzania licha ya kuwa na wanawake mahiri waliowahi kusimama kulipigania taifa letu na jamii zao michango ya haisimuliwi sana mfano Bi Titi Mohamed hawaimbwi sana kama kina mwl.Nyerere na wengine lakini walifanya makubwa sana kuendeleza jamii hii

Wanawake mashuhuri kama Asha Rose Migiro na wengine na hata leo hii tunae Rais wa awamu ya sita Dr. Samia Suluhu Hassan lakini bado jamii nyingi zinazotumia mfumo dume na nyingine hazijatoa nafasi kubwa ya kuona kama mwanamke anaweza kushiriki katika maendeleo ya kijamii na nyaja zingine na kuleta mabadiliko chanya zaidi.

Pamoja na jitihada nyingi zinazofanyika katika ulimwengu, Afrika na Tanzania kumkomboa mwanamke ili kuikomboa jamii nzima, kumpa nafasi mwanamke atimize wajibu wake ili jamii nzima iwajibike lakini bado tunaona mwanamke anapata nafasi kwa tabu sana katika mashule na vyuoni wanaombwa rushwa za ngono, kunyanyaswa kijinsia, makazini nako hivo hivo, wasanii wa kike tunasikia wakilalamika kuombwa rushwa ya ngono ili wapewe nafasi, lakini pia tunaona katika familia mwanamke hana maamuzi juu ya mali, ardhi, kukumbwa na mila na desturi potofu kama ukeketaji na kunyimwa baadhi ya vyakula, kuna wakati wanawake wakipewa nafasi kubwa wanabezwa hawapewi ushirikiano wa kutosha kama ilivyo kwa mwanaume.

MAZINGIRA WEZESHI KWA MWANAMKE KATIKA KUWAJIBIKA ILI KUCHOCHEA UWAJIBIKAJI KWA JAMII NZIMA.

Ni ukweli usiopingika jitihida mbali mbali zimekuwa zikifanyika kila kona ya dunia ili kuhakikisha mwanamke anapata nafasi katika kila nyanja ikiwemo Nyanja ya maamuzi, mfano katika nchi yetu serikali imekuja na namna mbali mbali ya kuhakikisha wanawake wanapewa nafasi ikiwa ni kutengeneza wizara ya jinsia ,watoto,wanawake na makundi maalumu ,wadau wa maendeleo wanafanya kila jitihada kuhakikisha wanawake wanasimama kuonyesha umhimu wao katika maendeleo ya jamii zao.

Licha ya jitihada hizi za serikali na wadau wa maendeleo ya jamii lakini bado tunaona ukandamizaji kwa wanawake upo na unaendelea kwa kiasi kikubwa kuombwa rushwa ya ngono ili waweze kupewa nafasi hii bado ni kikwazo ,manyanyaso ya kijinsia bado ni kikwazo kwa wanawake kuwajibika kumbe kuna haja ya juhudi kuendelea kuwekwa Zaidi kama
Majukwaa ambayo serikali imeweka, yafanya kazi ili watu waweze kupewa elimu na waweze kubadilisha mtazamo potofu

Uendeshaji wa warsha na semina mbalimbali zenye lengo la kumuhamasisha na kumkomboa mwanamke katika fikra duni na hivyo kumtrngenezea hari ya kuwajibika katika jamii hasa katika maeneo ya vijijini

Uhamasishaji wa nafasi za uongozi katika nyanja mbalimbali kwaajili ya wanawake,ilikutengeneza dhana madhubuti ya kujiamini kwa wanawake kujitoa katika nafasi za uongozi,mfano uongezwaji wa nafasi kwa uongozi wa viti maalum serikalini,na kupewa nafasi za kugombea nafasi mbalimbali serikalini.

MAENEO AMBAYO MWANAMKE AKIWAJIBIKA JAMII NZIMA INAWAJIBIKA
Wanaweka Kama sehemu ya wadau wa maendeleo ya jamii katika Nyanja zote wana umuhimu mkubwa katika kuchochea mabadiliko katika jamii mfano

- Elimu na Afya ;elimu na afya ni mhimu katika maendeleo ya jamii na watu binafsi, mwanamke akipewa nafasi asilimia mia moja ya kujishughulisha na elimu na kulinda afya ya jamii na familia yake , mwanamke anawajibu wa kulinda afya ya watoto wake na watoto wa jirani yake akawajibika vizuri basi jamii itakuwa imewajibika kwasababu mwanamke hufundisha watoto wake na jamii yake na kushirikiana, kuwahamasisha wanawake wenzake na kufanya hivo ni kuikomboa jamii nzima kutoka kwenye ujinga na kulinda afya ya jamii

- Ujasiriamali; Katika jamii ya leo,wanawake wameonekana kua na juhudi kubwa katika maswala ya ujasiria mali,ili kuizi mahitaji, jitihada zinazofanywa na mwanamke wa leo katika ujasiria mali ,zinachochea jamii kuamka na kufanya ujasiria mali unaoleta tija kwa jamii nzima.Mfano,mama lishe.

- Kilimo; Kotokana na tamaduni za kitanzania na uhalisia kwamba, mwanamke ndie mwenye jukumu kubwa kuhakikisha ustawi wa familia hasa katika chakula na afya ya familia kwa ujumla,jambo hili limechochea mwanamke kujihusisha katika kilimo ili kupata uhakika wa chakula kwa familia yake na kufanya hivo jamii huwajibika.

-Mazingira; Kama ilivo ada "Mwanamke ni mazingira" msemo upendwao na wenye kuleta motisha kwa mwanamke ili kutengeneza mazingira bora katika jamii.Hivyo basi,Mwanamke akiwajibika katika kuhifadhi mazingira,huleta ushawishi katika familia yake na jamii nzima hivyo kupunguza na hatimae kutokomeza uharibifu wa mazingira.

-Sanaa na utamaduni; Sanaa na tamaduni ni mojawapo ya vitu vinavyounganisha jamii yetu na kuleta burudani na hivyo kuimarisha mshikamano, upendo na amani katika jamii, mwanamke akiwajibika vema katika sanaa na utamaduni,hujitoa kwa dhati na hivyo kuchochea maendeleo ya jamii kwasababu huunganisha jamii.

Huduma za kijamii; Kila jamii inauhitaji wa huduma mbalimbali ambozo ni muhimu katika kuleta ustawi na kujenga jamii bora yenye --maendeleo.Mwanamke akiwajibika katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kijamii,jamii itapata huduma bora na kuleta ustawi wa jamii nzima na hivyo kuchochea maendeleo.Mfano upatikanaji wa maji safi na salama na miundombinu

- Teknolojia; Katika ulimwengu wa sasa teknolojia ni kiungo muhimu katika kuleta mapinduzi ya kimaendeleo kwa kiasi kikubwa,kwakutambua hili,mwanamke akiwajibika ipasavyo,huleta mwamko katika jamii ilikujihusisha na teknolojia ,kwakua mwanamke ni chachu ya maendeleo hayo katika jamii,mfano,vumbuzi mbalimbali za kiteknolojia.

-Uongozi ,utawala Siasa na ;Mwanamke akiwajibika vema katika uongozi, siasa na utawala,hutengeneza jamii inayowajibika na kujitoa katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.Hii inajidhihirisha pale ambapo mwanamke akipewa nafasi katika uongozi na utawala,huwajibika kwa bidii kubwa na kuleta maendeleo na jamii nzima kuwajibika.
Mfano,Mheshimiwa Raisi Samia Suluhu.

Hitimisho
"Viva viva mwanamke, viva viva mwanamke" ni sauti zilizojawa furaha na ushujaa ndani yake,ikiwa ni ishara ya ushindi katika ukombozi na uwajibikaji kwa mwanamke.

Sauti hizi husikika katika baadhi ya jamii za kitanzania, pale ambapo mwanamke aliwajibika ipasavyo ili kutengeneza jamii inayowajibika katika nyanja mbalimbali ikiwemo siasa,teknolojia,afya,sanaa na tamaduni,kilimo na hata uongozi na utawala bora,Kauli hizi ni ishara wazi kwamba uwajibikaji kwa mwanamke ni muhimu sana katika kuchochea jamii inayowajibika.

Hivyo basi,Mwanamke anaonekana kuwa na nguvu ya ziada katika jamii yetu katika kuhakikisha maendeleo ya jamii, hii ni kutokana na nguvu yake kubwa ya ushawishi katika uwajibikaji wake na hivyo kuwa na ushawishi mkubwa kwa jamii nzima katika kuhamasisha uwajibikaji.

Hivyo jamii inapaswa kutambua nguvu hii na kumpa mwanamke kipaumbele ili kufanikisha lengo la kutengeneza jamii yenye kuwajibika.
 
...andika zuri
 
Ni kweli kabisa na ndio maana wanasisitiza kumuelimisha mwanamke kwa ukimuelimisha ni kwa faida ya jamii nzima vivyo hivyo kwenye uwajibikaji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom