Mwanamke akatwa masikio yake na mumewe

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mwanamke mmoja wa miaka 23 kutoka nchini Afghanistan ameielezea BBC kwamba mumewe alimfunga kamba na kumkata masikio yote mawili katika mzozo wa kinyumbani katika mkoa wa kaskazini wa Balkh.

Mwanamke huyo Zarina kwa sasa yuko katika hali nzuri hospitalini.

''Sijatenda dhambi lolote'' ,alisema.''sijui kwa nini mume wangu alinifanyia hivi''.

Mume huyo kwa sasa ameenda mafichoni katika Ulaya ya kashinda kufuatia shambulio hilo kulingana na maafisa wa polisi.

Zarina ameambia chombo cha habari cha Pajhwok kwamba shambulio hilo ambalo anasema halikusababishwa na hatua yoyote lilifanyika baada ya mumewe kuamka.

Mwanamke huyo aliolewa akiwa na umri wa miaka 13 na ameiambia BBC kwamba uhusiano wake na mumewe haukuwa mzuri.

Zarina alilalamika kwamba mumewe alijaribu kumzuia kutowatembelea wazazi wake, amesema hataki kuwa naye tena.

"Ananishuku sana na kila mara unituhumu kwa kuzungumza na wanaume wengine wakati ninapoenda kutembelea wazazi wangu'' ,alisema.

Ametaka akamatwe na kushtakiwa.

Chanzo: BBC
 
Baadhi ya mianaume ya ukanda huo ni zaidi ya mashetani! Kwao uovu dhidi ya ubinadamu hususan wanawake na watoto ni kitu cha kawaida mno. Limemkata mwenzie masikio bila sababu halafu hilooo limekimbilia Ulaya kama likimbizi. Trump akiyapiga marufuku mnakuja juu.

Limemtenda hivi mkewe tena lililomwoa akiwa kigori (13) ndio litakuonea huruma wewe mtu baki? Sijui kwanini neno upendo na kuvumiliana hayamo kabisa kwenye kamusi ya haya majitu.
 
dini hairuhusu hii
hii roho ya mtu binafsi haisuiani na dini!
 
Ila kuna wanawake hawawasikilizi kabisa waume zao.. labda alikata asikie vizuri.. teh
 
Back
Top Bottom