1. Kwanza nampongeza sana kwa kujifungua watoto wote hao watano bila matatizo yoyote tena nyumbani
2. Nampongeza na mume wake kwa kujali na kumsaidia yeye peke yake bila msaada wa majirani
3. Nampa pole sana huyo mama kwa kazi hiyo ngumu maana naijua vizuri nina watoto naelewa, kweli natoa pole ya dhati kabisa
3. Mungu awajalie afya njema na wakue wote salama bila matatizo yoyote na tupo nyuma yake tunamuombea
4. Wito wangu ni kwa Serikali, kwa kweli Serikali imsaidie huyu mama na baba kuwalea watoto hawa maisha yao yote kwani kwa kweli hawataweza wenyewe, Mhe JK, Waziri Mkuu na viongozi wote waandamizi familia hii isadiwe kiserikali kwa kila kitu juu ya hawa watoto na mama yao.