Mwanamke ajifungua watoto watano (5) huko Kahama...!!!

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Mwanamke mmoja kwa jina Shija Buswega wilayani kahama mkoani shinyanga amejifungua watoto watano. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana mwanamke huyo alijifungua watoto hao kwa msaada wa mumewe tu kwani alishikwa na uchungu usiku wa manane na kutokana na umbali kutoka kijijini kwao hadi kituo cha afya iliwawia vigumu kupata msaada wa mkunga hali iliyomlazimu mume wake kuchukua jukumu la kumzalisha mkewe.

Inasemekana kuwa mwanamke huyo hiyo ni mimba yake ya kumi na huko nyuma aliwahi kuzaa watoto mapacha mara mbili. Asubuhi alipelekwa katika hospitali ya wilaya Kahama ambako alipatiwa matibabu ya awali lakini baadaye madaktari walishauri apelekwe katika hospitali ya rufaa bugando mwanza yeye na watoto wake kwa matibabu zaidi. Hadi sasa afya ya mama na watoto wake wote inaendelea vizuri. Watoto hao ni wasichana watatu na wavulana wawili.....Source RFA!
 
Mungu amsaidie awakuze wakiwa na afya na furaha tele
...Ni kweli mkuu ni jambo jema sana lakini nikiangalia upande wa pili wa malezi kiukweli kabisa hiyo famili ina changamoto kubwa sana..
 
Mungu amsaidie aweze kuwapa mahitaji yote yanayohitajika pia naomba serikali na wahisani mbalimabli wajaribu kumpa msaada wa kutosha Mama huyu na familia yake coz ana timui ya kutosha.
 
Mungu mkubwa amsaidie aweze kuwakuza vizuri baada ya kuona habari hii kwenye gazeti swali lilliloniijia kichwani ilikuwa je? Mwanamke huyu atawanyonyeshaje hao watoto labda hapa wanawake wa humu JF wanaweza kunisaidia
 
Hongera zake sana jamani!

But serikali lilione hili na litoe msaada wa malezi kwa hawa watoto

Si jambo la kawaida , ni vigumu sana kwa huyu mama kuweza kuwalea hawa watoto wote peke yake jamii inapaswa kutoa msaada kwa huyo mama.

Tuangalie uwezekano wa kumpatia msaada MTZ mwenzetu.
 
1. Kwanza nampongeza sana kwa kujifungua watoto wote hao watano bila matatizo yoyote tena nyumbani
2. Nampongeza na mume wake kwa kujali na kumsaidia yeye peke yake bila msaada wa majirani
3. Nampa pole sana huyo mama kwa kazi hiyo ngumu maana naijua vizuri nina watoto naelewa, kweli natoa pole ya dhati kabisa
3. Mungu awajalie afya njema na wakue wote salama bila matatizo yoyote na tupo nyuma yake tunamuombea
4. Wito wangu ni kwa Serikali, kwa kweli Serikali imsaidie huyu mama na baba kuwalea watoto hawa maisha yao yote kwani kwa kweli hawataweza wenyewe, Mhe JK, Waziri Mkuu na viongozi wote waandamizi familia hii isadiwe kiserikali kwa kila kitu juu ya hawa watoto na mama yao.
 
Matatizo mengine tunajitakia wenyewe mimba ya kumi why?????? ila hongera kwa kujifungua namtakia malezi bora na mungu amsaidia
 
Matatizo mengine tunajitakia wenyewe mimba ya kumi why?????? ila hongera kwa kujifungua namtakia malezi bora na mungu amsaidia

Pengine hana elimu ya uzazi wa mpango. Lakini pia, serikali ina wajibu kwa unique cases kama hizi.
 
Matatizo mengine tunajitakia wenyewe mimba ya kumi why?????? ila hongera kwa kujifungua namtakia malezi bora na mungu amsaidia

Kisimba, hujakaa kijijini nini. Hakuna maisha huko. Giza likiingia ni kujifungia ndani, hakuna redio na kama zipo hela ya betri ni mgogoro. ukishapiga msosi moja kwa moja kitandani what follows is known, usishangae ndo maisha ya kijijini.

Ndio maana kijana akimaliza darasa la saba na kufeli yuko tayari kuanzisha familia whatever his age hivyo hivyo kwa mabinti.

Cha msingi tuangalie jinsi ya kumsaidia huyu mama wa watu idadi hiyo ya watoto sio rahisi kwa mtanzania kuwahudumia tuanzishe mchango wa kumsaidia.
 
hawa JK Ndio anawakimbia kabisa
Mengi kapate baraka mzee wangu na vijana wa kileo hao ANCIENT DAYS
 
Mungu alivyoumba ulimwengu na mwanadamu alisema ENENDENI MKAIJAZE DUNIA!

upo sahihi lakin hakusema mkaongezeke ili muishi kwa mateso pata kapicha maisha haya ya bongo watoto 20 anakipato gani cha kuwatunza!
ewe kikwete uliye msikivu dhihirisha unagushwa ma matatizo ya watz kwa kumsaidia huyu mama na wanae.
 
Sad news nimesoma gazeti la leo, wawili kati ya mapacha hao wamefariki. So sad, Karne ya ishirini bado vifo vya watoto wachanga vinashindwa kuepukika, jamani what a tragedy.

Tunashindwa nini kuwafanya watoto hao wawe hai?????

Au ndo tuseme nguvu nyingi ilienda kwenye kampeni mpaka huduma hospitalini zimekwisha????
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom