Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
Mwanamke mmoja kwa jina Shija Buswega wilayani kahama mkoani shinyanga amejifungua watoto watano. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana mwanamke huyo alijifungua watoto hao kwa msaada wa mumewe tu kwani alishikwa na uchungu usiku wa manane na kutokana na umbali kutoka kijijini kwao hadi kituo cha afya iliwawia vigumu kupata msaada wa mkunga hali iliyomlazimu mume wake kuchukua jukumu la kumzalisha mkewe.
Inasemekana kuwa mwanamke huyo hiyo ni mimba yake ya kumi na huko nyuma aliwahi kuzaa watoto mapacha mara mbili. Asubuhi alipelekwa katika hospitali ya wilaya Kahama ambako alipatiwa matibabu ya awali lakini baadaye madaktari walishauri apelekwe katika hospitali ya rufaa bugando mwanza yeye na watoto wake kwa matibabu zaidi. Hadi sasa afya ya mama na watoto wake wote inaendelea vizuri. Watoto hao ni wasichana watatu na wavulana wawili.....Source RFA!