Mwanakondoo ndiye huyo Simba wa kabila la Yuda

Mwanakondoo ndiye huyo Simba wa kabila la Yuda

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,938
Reaction score
41,098
Salaam, Shalom!

Mhubiri anasema, Kila jambo na wakati wake.

1. MWANAKONDOO.

Mfalme aliacha kiti Cha Enzi, akavaa mwili wa Mwanadamu akaonekana maskini, asiye na utukufu kwa kazi maalum ya ukombozi. Kumtoa Mwanadamu kwenye minyororo ya dhambi.

2.SIMBA WA KABILA LA YUDA.

Sasa baada ya kushuka kuzimu na kuitwaa funguo za mauti na kuzimu, akafufuka na kupaa mbinguni, ameketi Katika kiti Cha Enzi mbinguni. Na ametuketisha pamoja naye kutawala Katika ulimwengu wa Roho.

CONCLUSION:

1. Ni muda wa kuuleta ufalme wa Mungu Katika nchi,

- Wezi waitwe kwa majina yao na kuambiwa huu ni wizi, watubu na kuacha wizi.

- Ni muda wa kumrudishia haki yake mjane na yatima aliyodhulumiwa.

- Ni muda wa kuamuru nyakati njema zifuatane nasi Katika nyanja zote za MAISHA, siasa, uchumi,uvuvi,kilimo,ufugaji nk nk.

- Ni muda sasa wa kutawala, ufalme wa Mungu uonekane Katika siasa za nchi yetu, haki uonekane ikitendeka Ili machozi ya walioonewa yaweze kufutwa Tena..

Imebarikiwa sana Nyikani, Taifa la nyakati za mwisho Katika kuonyesha Dunia juu ya ufalme wa Mungu duniani.

Haya sasa , Simba amka ule mawindo yako yako tayari.

Aamin 🙏
 
Siku ukimwona aliyekuja kama Mwanakondoo amebeba upanga uwakao kuwili, akina kwa hukumu,

Kumtenga mwema na mwovu Ili alipwe sawa sawa na matendo yake usishangae.

SI vyema kutangazwa amani wakati wa vita.

Kila jambo na Wakati wake.
 
Ni nani awezaye kuweka uzio Katika nyumba YANGU Ili kumzuia maskini kuingia ndani Ili kupata faraja?
 
(2 Wafalme 6:14,16-19)

14:kwa hiyo akapeleka huko farasi, na magari, na jeshi kubwa, wakafika usiku, wakauzingira mji ule pande zote.

16: Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao,

17: Elisha akaomba akasema, Ee BWANA, nakusihi,mfumbue macho yake,apate kuona. BWANA akamfumbua macho yule mtumishi, naye akaona, na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.

18: Na walipomtekemkia Elisha akamwomba BWANA, akasema,Tuwapige, nakusihi, watu Hawa kwa upofu. Akawapiga akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha.

..Mwisho wa kunukuu....


Ninawapiga upofu wote wanaosimama kuzuia haki kutammalaki juu ya nchi, Giza liwapate, wapapase bila kuona chochote kwa miezi sita kuanzia sasa. Mwenye haki apate Nafasi ya kuongoza watu wa Mungu kuifikia nchi itiririkayo maziwa na asali.

Imekuwa , Aamin
 
Back
Top Bottom