Mwanajeshi amkata vipande vipande mkewe

sijaelewa hivi hii habari inasema huyu jamaa alipojisalimisha aliwekwa lockup maana naona alijisalimisha halafu akarudi nyumbani kisha akatoka tena saa kumi na mbili asubuhi there is something fishy here

HII NDO TZ AISEEE....... YAANI MTU ANASEMA NIMEUA TAYARI, UNAMWAMBIA NENDA KALETE BARUA YA SIJUI BALOZI AU MJUMBE........ SASA KAMA ANGETAKA SI ANGEUA NA MWINGINE?????????????????? MIMI NAONA KITWANGA AANZE NA HUYU MHESHIMIWA ASKARI ALIYEKUWA NA HANGOVER MPAKA AKAMRUDISHA MUUAJI MTAANI AKALETE BARUA.........
 
Mura mangana vita ni vita Mura!
Hao kwenye maluvi Davi huwa hawataki mchezo
Wakurya ukiwakorofisha ni watu hatari sana, kabla sijasoma jina la askari huyo tayari nilikuwa na uhakika kwamba ni mkurya.
 
Labda polisi nao waliogopa kuchezea mapanga, maana mkurya akibadilika ni zaidi ya simba.
 
Last edited:
hangover na rushwa
 
Wanajeshi wasaidiwe kisaikolojia,wanafanya kazi kubwa ya kulinda amani,wanapokua huko kwenye mission mbalimbali huwa wanafanya zaido ya hayo!Hivyo wakiwa uraiani yakiwakuta magumu huwa utekelezaji ndo kama yaliyomkuta huyo mfunga buti.
Wanafanyaga nini huko kwenye mission? Wanaua watu?
 
ukute huyo mwanamke alikuwa anamegwa na msela mwingine nje na mjeda akagundua huku yeye anagharamia kila kitu.
 

Huo utaratibu wa polisi wa kituo hicho ndio kwanza nausikia leo kwamba mtuhumiwa tena wa mauaji anaweza kwenda kwa ridhaa yake mwenyewe kujisalimisha kituo cha polisi na kutumwa na mkuu wa kituo au askari yeyote aliekutwa kituoni kwenda kuchukua barua ya balozi kwanza hicho kituo kimulikwe kwani siamini kama huo ndio utaratibu wa jeshi hilo la polisi.
 
Dah kanikumbusha kisa cha miaka fulani Iringa huko ,jamaa aliua akaenda kituoni kujisalimisha
 
hao polisi wa staki shari ni wazembe sana ndio maana walimiminiwa risasi haiwezekani mtu aje ameua halafu mnamuazchia eti akalete barua..huu ni uzuzu ulopitiliza
 
ukute huyo mwanamke alikuwa anamegwa na msela mwingine nje na mjeda akagundua huku yeye anagharamia kila kitu.
MAELEZO YANASEMA JAMAA ALIOA MKEWA PILI MAHAKA NA IKAMWAMBIA AMPATIE MAMA NYUMBA NA KESI INGEISHA 27 MWEZI HUU...... NA SI VINGINEVYO
 
Last edited:
Nyie wanawake ni tatizo kubwa sana ktk haya maisha, marehemu aliandaa mauti yake mwenyewe, mshahara wa dhambi ni mauti, alikuwa na lengo la kumchuna mumewe kifo kimemchuna yeye.
Hakuna mshindi kwenye hili Mkuu. Huyo Mjeda hana mamlaka ya kutoa uhai wa mkewe na kwa kutenda hilo sio kuwa kajiondelea tatizo; Hatma yake itakuwa nini?!!
 
MAELEZO YANASEMA JAMAA ALIOA MKEWA PILI MAHAKA NA IKAMWAMBIA AMPATIE MAMA NYUMBA NA KESI INGEISHA 27 MWEZI HUU...... NA SI VINGINEVYO

Shuhuda amesema jamaa alikubari kumpatia nyumba, pia anakatwa kazini 200000/= kwa mwezi na bado bibie alikuwa anachukua kodi ya nyumba, lakini shuhuda akaenda mbali kwa kusema maneno yasiofaa mtaani mfano "nitamkomesha nk" ukiangalia kilichotokea na saikolojia na jamaa inaonyesha moja kwa moja jamaa kakosewa ndio maana alivyoua alikuwa na ujasiri wa kusema nimeua na polisi alienda mpaka kwa balozi alifika na kurudi mwenyewe tena polisi, sio hasira ila alidhamiria baada ya kukerwa..
 
SASA AKANYEE DEBE NDO UJIRA WAKE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…