GE2025 Mwanaisha: Nikiwa mbunge mtapita bure daraja la Kigamboni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia ACT Wazalendo, Wakili Mwanaisha Mndeme ameahidi kuhakikisha wanapita kwenye daraja la Nyerere (maarufu kama Daraja la Kigamboni) hawalipi fedha yoyote endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Ameyasema hayo Septemba 06, 2025 akiwa katika viwanja vya Maganila, Kata ya Tungi jimbo la Kigamboni,Mndeme ameainisha changamoto tatu kubwa alizodhamiria kuzitatua jimboni humo.

Amesema pindi akipata nafasi jambo atakaloanza nalo ni uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwa kushirikiana na TANROAD na TARURA.

Ameeleza kuwa miundombinu hiyo imekuwa changamoto na kutokana na ubovu wake wananchi hukwama kupata huduma za msingi kama kupata matibabu kwa wakati na wakati mwingine kuchelewa kwenye kufanya shughuli za maendeleo.

Changamoto ya pili aliyoahidi ni kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa vivuko na kuwa vya bei nafuu.

"Tulikuwa na MV Magogoni, MV Kazi na MV Kigamboni kivuko cha MV Magogoni kipo matengenezo tangu 2023 leo ni 2025 wanasema matengenezo yamefikia asilimia 55%,MV kigamboni kimetengnezwa kwa asilimia 10% tu ina maana tuna miaka mingine takribani saba kivuko kiweze kutengenezwa. CCM imeshindwa kuhakikisha tuna uhakika wa vivuko"

Ahadi ya tatu ya msingi aliyoahidi kuitatua ni kuondoa malipo kwenye daraja la Mwalimu Nyerere (maarufu kama Daraja la Kigamboni) akieleza kuwa atafuatilia kufahamu ni deni kiasi gani NSSF bado inadai kutokana na zile asilimia 60% iliyozitoa katika ujenzi wa daraja hilo ili kujua kama limeisha basi wananchi waweze kupita bila kulipia gharama.

"Tunafahamu moja ya changamoto Wanakigamboni wanapata nayo shida ni daraja la Mwalimu Nyerere ndiyo daraja pekee ambalo linalipiwa katika nchi yetu,lakini suala la kulipia daraja imekuwa ni mzigo kwa wana-Kigamboni tunafahamu liljengwa kwa bilioni mia mbili kumi na tatup kwa ubia (NSSF aslimia 60% serikali 40%) hatuna taarifa huo mkopo ambao NSSF ilichangia daraja imebaki kiasi gani"

Soma Pia: Pre GE2025 - Mwanaisha Mndeme aomba kuteuliwa kugombea ubunge Kigamboni
Your browser is not able to display this video.
 
Hahaha daraja la wana mtandao hilo upite bure wale wapi?

Anadhani liliota kama uyoga?
 
Mradi wa watu huo, aache porojo huyo wakili uchwaraa.
Lol
 
.....atafuatilia kufahamu ni deni kiasi gani NSSF bado inadai kutokana na zile asilimia 60% iliyozitoa katika ujenzi wa daraja hilo ili kujua kama limeisha basi wananchi waweze kupita bila kulipia gharama.....

===========
Akikuta bado halijaisha atafanyaje? atalilipa lote ama..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…