UKWELI NADHANI MWANAHALISI IMEANZA KUFILISIKA KIUCHAMBUZI
Nadhani usimlaumu Kubenea kwa habari ya Jana. ile habari ndio iliokuwepo ndani ya Bunge. kwani tayari baadhi ya wabunge wamezungumza waziwazi kama wanasakamwa. SOMA Tamko la Msambya kuhusu mahakama ya kahi alivyosema.
Binafsi naona limefilisika kimawazo na kiuchambuzi.
Mimi ni msomaji sana wa Mwanahalisi ila toleo la jana kuna makala ya Kubenea ihusuyo UDINI KUINGIA BUNGENI, likijenga hoja kuwa mawaziri waislamu wanaonewa ama kukamiwa kwa sababu ni waislamu likitolea mfano wa mgongano wa Ghasia na Jenista, Dialo na Kawambwa na likahoji Mbona hao wabunge hawakuwa wakali baada ya serikali kupitia Chikawe kutoa tamko la mahakama ya kadhi? Kubenea akamailizia kwa uchambuzi wa kama mtoto wa chekechea eti ni kwa sababu chikawe ni Mkristo.
Kila mwenye akili timamu aliyesoma hiyo makala hawezi akasadiki kama imeandikwa na Kubenea na kuchapishwa na Mwanahalisi. UKWELI NADHANI MWANAHALISI IMEANZA KUFILISIKA KIUCHAMBUZI.
Nilijiuliza hivi kweli hata Ndimara Tegambwage hakuweza kumshauri, maana namwamini yule mzee ni kichwa.
Hivi kweli Kubenea alitaka wabunge wawe wakali kuhusu kadhi wakati akijua ni suala linalosigana na KATIBA YA JAMHURI? Hivi kweli Kubenea alitaka hao wabunge wawe wakali ili hali Tanzania ni nchi isiyo na dini? Iweje Mabudha nao wakitaka mahakama yao, na Wakristo watake mahakama yao katika mfumo wa KISERIKALI?
Kuanzia jana nimeingiwa na mashaka sana na uwezo wa kufikiri, na kuchambua wa Kubenea.
Huyu anafanya makusudi kujaza board ya JF na mabandiko yake ili yale ya maana yasiendelee kujadiliwa ipasavyo. Nadhani inabidi tususie kufungua threads anazoanzisha!
Pole kwa hali ya sintofahamu iliyokuandama kichwani kutokana na ugonjwa wako sugu. Mwanahalisi linachapa na kuuza nakala nyingi kuliko magazeti yote yaliyo makini hapa nchini, ukiachia yale ya Shigongo (ya udaku). Linachapa zaidi ya nakala 70,000 kila wiki na ni gazeti la Kswahili lenye circulation kubwa kuliko yote hgapa duniani.
Rekodi ya kuchapisha nakala nyingi iliwahi kushikiliwa na RAI huko nyuma lakini Mwanahalisi limekaa kileleni kwa takriban miaka mitatu au zaidi.
Linakaa siku 3 hadi nne kwenye meza za mauzo kwa sababu baada ya kutoka watu huliuzia kwa siku kadha baadaye. Na pia nitasema kuwa newsroom ya Mwanahalisi, ingawa ni ndogo, ni ya kisasa zaidi (most modern) kuliko zote nilizowahi kutembelea hapa jijini.
Huyu anafanya makusudi kujaza board ya JF na mabandiko yake ili yale ya maana yasiendelee kujadiliwa ipasavyo. Nadhani inabidi tususie kufungua threads anazoanzisha!
.Labda mtu hapendi baadhi ya waandishi wake..
.sasa pasco unasema mpenda mageuzi, mwanahalisi nalo linasema mpenda mageuzi. sasa mbona mtafautiana uansema sio professional. ninwasiwasi na wewe
.
Malaria Sugu, huna haja wala sababu ya kuwa na wasiwasi na mimi kuwa mshabiki wa mageuzi huku nikili cricitisize Mwanahalisi, ndio maana kuna Zitto/Dr/Slaa na Mbowe ni wanamageuzi and yet not the same na Lipumba/Mrema/Mbatia/Mtikila na wote ni wanamageuzi.
Hata wana CCM kama Nape/Sitta/Mwakiembe/Kilango etc pia ni wana mageuzi japo wako ndani ya CCM hao wakipigana from within.
Bado unawasiwasi?.