Mwanahalisi: Dr.Olimboka asisitiza, waliotaka kumuua wanatoka Ikulu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Taarifa ambazo zimeandikwa katika gazeti hilo zimedai kuwa Dr. Olimboka amesema uzushi na uongo wa kupikwa na jeshi la polisi juu ya utekeaji na mupigwa kwake kuwa ni Mkenya ni kupindisha hali ya mambo na ukweli na kasisitiza watesi wake wanatoka Ikulu.

Naamini hapa Kova kwa msemo wa Mh. Sugu kuwa Arudi studio akatengeneze filamu yake ya kichina hii aliyoitoa ishavuja.
 
Kova aache usanii wa kijinga asijitwishe zigo ambalo haliwezi kulibeba Ikulu yahusika moja kwa moja acheni visingizio
 
Hizo mahakama za kangaroo?

Kweli Fisi akiwa hakimu mbuzi anajisumbua kuleta ushahidi, hakuna haki.

Unahukumiwa,
kupigwa meno ya koo,
na kufyonzwa damu yote,
hadi ufe.

kisha mzoga wako,
kutafunwa kiulaini,
na mob zima la fisi
na mifupa yako,
kubemendwa,
bila kusaza kitu.

Hukumu hii pia,
ina upatilizo wa ndugu zako ,
popote wakipatikana,
ni halali ya fisi yeyote,
kuwafanya kitoeo.
 
Hakika serikali ya dhaifu inazidi kuvuliwa nguo zote sasa cjui nn kitafuata hapo.......
 
liko mahakamani msizunguzie!!!!!!!!!!!!!!!!
Arusha nako kesi ya ubunge kulikuwa na mahakama wakati Judge "anaamrishwa" kuhukumu kinyume cha ukweli anaoujua, labda mkate uendelee kuwapo. Wananchi majority wakawa kinyume naye pale Arusha. Kule Ukonga kilinaswa kimemo kikimwamuru Judhe ahukumu in favor of Boss aliyemwajiri, kinyume cha ukweli halisi na kila mtu ni shahidi (angalau dhamira ziwasute kama ni binadamu wastaarabu kweli) wakati mbunge aliyekimbia na masanduku ya kura kinyume kabisa na kanuni alipohakikishiwa kushinda. Sasa ni mahakama gani uisemayo ambayo itaenda kinyume na Boss wake juu ya suala ambalo DUNIA nzima inafuatilia kwa makini, na tayari Boss na msaidizi wake wamekanusha kuhusika hata kabla kesi haijaenda mahakamani? Au unataka kutuambia hakimu huyo ameshuka kutoka mbinguni na analipwa na Mungu? Acha siasa katika mambo ya kimsingi. Kuweni na aibu nga kidogo tu mheshimiwe tujue kuna watu.
 
Hahaaa nyie wana suala hili ni marufuku kuzungumza liko mahakamani
 
Ndio maana kale ka mama, Yule mwanamziki lukuvi na mwanasheria anayelalia upande mmoja wamesimamia miguu na mikono yao kuhakikisha wanafuta sooo.


This is Only in Tanzania
 
Safari hii watayafunga hata masaburi yao kila wanapojificha matone ya moto yanawamwagikia na watakoma miaka hii na sasa wanakubali kuwaua watu ili tu kuchafua vyama vingine.
 
Back
Top Bottom