Mwanahabari huyu kanishangaza sana

Mwanahabari huyu kanishangaza sana

aliyekwambia huyu mwanahabari nani? mimi nammjua kama msanii wa maigizo
 
aliyekwambia huyu mwanahabari nani? mimi nammjua kama msanii wa maigizo

Hilo swali linamfaa mtangazaji Angalien Mpendu wa star tv maana ndie aliemualika studio za star tv za Dar-es-salaa kama mwandishi sambamba na bwana Balile.

Mimi ni mjumbe tu "niliyegafilika" na kauli ile kama wewe.
 
Aina hiyo wa waandishi au wana habaro wapo wengi sana hapa nchini,kuna yule mwingine wa ile redio ambayo nilishaacha kuisikiliza yapata miaka miwili iliyopita anaitwa kibonde sijui kishimo sijui kitu gani?hivi naye hajapata ukuu wa wilaya?
 
Mtu akifika mahali akiongozwa na njaa tabu tupu. Mi sintomlaumu maana najua ni njaa tu inayomsumbua.
 
Mdomo Wake Tu Umekaa Kichuchunge Na Macho Yake Nayo Yamekaa Kisanii Sanii Je Wewe Ulitegemea Mbichwa Wake Utoe Madini Kama Ya Mtani Wangu Balile? Na Ili Kudhihirisha Kuwa Huyo Sina Malengo Ni POPOMA Unaambiwa Eti Yeye Ndiyo Afisa Uhusiano Wa Ile Redio Iliyouzwa Iitwayo Njia Ya Kwenda Mbinguni Na Nadhani Uliona Jinsi Balile Na Wale Wanafunzi Akina Mansoor Na Juma Walivyomdharau Na Kiukweli Leo Sina Malengo Ameumbuka Na Amejiaibisha. Huyo Ndiyo Mwanadiplomasia Wetu Siku Za Baadae.

Je Ulisikia Lile Dongo La Mwisho Ambalo Balile Alimtupia Sina Malengo? Siku Nyingine Akijua Kuwa Anakwenda Studio Halafu Mgeni Mwingine Ni Balile Awe Anachomoa Tu Kwani Napenda Mno Balile Alivyokuwa Akimdhihaki Kidiplomasia Kwa Mfano Kuna Sehemu Balile Alimwambia Kuwa Hicho Chuo Cha Diplomasia Unachosoma Wewe Sasa Mimi Nimesoma Hapo Miaka 11 Iliyopita. Hapo Sina Malengo Nilimwona Alivyonywea Kwani Kiuwezo Kumpambanisha Ktk Vipindi Vya Hoja Balile Na Sina Malengo Wa Mawingu Iliyouzwa Ni Sawa Na Kumpambanisha Daniel Sturridge Wa Liverpool FC Na Juma Javu Wa Yanga FC.
Ukiandika vizuri tu utapeli weka bila kuweka haya sijui trite 'mafumbo'!
 
Muda mfupi uliopia nilikuwa natazama kipindi cha "Jicho letu ndani ya habari" kinachorushwa na star tv.

Kama kawaida, kipindi hiki kilikuwa kinajadili namna magazeti yalivyoripoti habari za wiki nzima na kwa wiki hii mjadala mkubwa ulikuwa ni kuhusu kuhojiwa na Tume ya Maadili kwa mama Tibaijuka na mwenzake Andrew Chenge.

Waalikwa katika kipindi hicho walikuwa ni mhariri Balile na mwanahabari Simon Simalenga kwa upande wa studio za Dar-es-salaam.Na kwa upande wa Mwanza, wageni walikuwa ni wanafunzi wawili wanaosomea uandishi wa habari katika chuo cha SAUT Mwanza.

Kauli ya mama Tibaijuka kuwa alitumia shilingi milioni 10 kununulia mboga ilichukua nafasi katika mazungumzo hayo kwani iliripotiwa sana na vyombo vya habari.

Ilipofika zamu ya mwandishi Simalenga kutakiwa kutoa maoni yake juu ya kauli hiyo ya mama Tibaijuka,kwanza alianza kwa kurejea kauli za kejeli zilizopaswa kutolewa na viongozi wengine siku za nyuma ambapo aliitaja kauli ya Mramba kuwa hata watanzani wakila nyasi lazima ndege ya raisi lazima inunuliwe;kauli ya Andrew Chenge, kuwa mabilioni yale ni vijisenti na kauli hii mpya ya mama Tibaijuka.

Cha ajabu,alianza kwa kusema yeye huwa haamini maneno ya kusikia mpaka ashuhudie mwenyewe akimanisha kuwa haamimi kama kauli hizo ziliwahi kutolewa na viongozi hao.Huo ulikuwa ni kama utangulizi tu.

Aliponishangaza zaidi mwandishi huyu ni pale alipojaribu kuetetea kauli ya mama Tibaijuka kuwa, milioni 10 ilikuwa ni hela ya mboga tu kwa kusema "inawezekana hiyo milioni 10 mama Tibaijuka alitumia kununulia mboga kwa ajili ya shule anayomiliki".

Yaani hapa mwandishi huyu alikuwa anajaribu kutuambia kuwa, alichomanisha prof.Tibaijuka ni kuwa, milioni 10 zile labda alizitumia kununulia mboga kwa ajili ya wanafunzi wa shule yake na kwamba waandishi wenzake walitakiwa wachunguze kauli ile kabla ya kuiripoti tu kama ilivyotolewa.

Swali;
Je,inawezekana mwanahabari huyu yuko sahihi na kwamba waandishi wenzake walitakiwa kuifanyia utafiti kauli ile kwanza kabla ya kuiripoti?

Anawania u DC lakini naona amechelewa muda umekwisha
 
Hayo ni makosa ya Star TV. Huwezi kuleta mjadala mkubwa unaogusa jamii halafu ukaalika watu wenye uelewa finyu wa mambo kujadili kama huyo Simalenga. Alichokisema Simalenga ndio mwisho wa uwezo wake katika kuchambua unategemea nini zaidi? Kama kituo cha TV kinachotazamwa na watu wengi tena wengine wenye uelewa mkubwa lazima utafute Watu Bora wa kujadili sio bora watu, maana nia ya kupata majawabu ya kusudio yatapotea kabisa.
Mfano unaleta mada "Kwa nini Tanzania pamoja na rasilimali ilizo nazo bado inaendelea kuwa masikini?" Halafu wachangiaji wa mada hiyo unamuweka Nape Nnauye au Livingstone Lusinde unategemea kupata nini zaidi ya kuharibika kwa mjadala? Star TV wanapaswa kuliangalia hilo maana wamekuwa na tabia hiyo mara nyingi sana ya kuleta mada ya msingi ila watu wasio kidhi vigezo kujadili.

Mleta mada ungeandika "mwanafunzi huyu" ndo ungekuwa sahihi zaidi kwani aliyekuwa anahojiwa ni mwanafunzi wa uandishi wa habari na si mwanahabari, lakini ukweli lipo tatizo katika uandaaji wa vipindi vya star tv, utakuta mwandaaji na wongozaji wa kipindi wote mbugila sasa unategemea nini?
 
Mleta mada ungeandika "mwanafunzi huyu" ndo ungekuwa sahihi zaidi kwani aliyekuwa anahojiwa ni mwanafunzi wa uandishi wa habari na si mwanahabari, lakini ukweli lipo tatizo katika uandaaji wa vipindi vya star tv, utakuta mwandaaji na wongozaji wa kipindi wote mbugila sasa unategemea nini?

Huyo ni mwanahabari kwa mujibu wa Star tv.
 
Simalenga Ni Gamba gumu....Anataka ukuu wa wilaya...Sidhani kama mtu aliyesoma Diplomasia anaweza kuwa kichwa nazi kama yule jamaa...

STARTV ni muda sasa wa kutafuta wachangiaji mahiri kwenye Vipindi vyenu hasa hivyi vya asubuhi...
 
Nimemuona mara kadhaa akifanya uchambuzi wa "kiwango cha chiiini kabisa". Sijui ni kwanini Mzee Mpeendu anapenda kumwalika. Hivi hakuna "Magwiji" wengine kama Balile?!

Tafadhali Star tv tuleteeni vichwa kwenye hicho kipindi. Mnatutesa walaji wenu. Huyo kijana mpelekeni kwenye uchambuzi wa Maigizo kama mnampenda.
 
Kauli ya milioni 10 ni hela za mboga tu kutolewa na kiongozi mkubwa mbele ya time ya maadili ni kauli tata inayoibua maswali mengi kuliko majibu,Serikali hii ya CCM kwa sasa imejaa viroja na wananchi wanaikenulia meno tu.
 
wanahabari wa hapa nchini wengi wao ni matatizo mfano mkuu aliposema uliwe sijui wa liandikaje baada ya kuripoti kilichojiri wanaripoti vingine sijui ni siasa au kutafuta ukuu wa wilaya kwa mfano wangeweza kueleza mapungufu ya wanasheria wa tume ingesaidia maana yalikuwa wazi nao pia waadilifu
 
sasa mwandishi kama huyo Simalenga akikutana na mtu mmoja niliyemsikia kwenye Tv anaitwa mzee Farijala hapo ndipo utasikia kichefichefu kabisa
 
Huyu Simalenga anaejinadi mwanahabari na mwanadiplosia siku moja ajitokeze kwenye "This week in perspective" ajadili masuala ya Burundi the symptoms of a failed state and renewed conflicts in the great lake region and its implications to the EAC.

Hii itatusaidia kuupima uwezo wa huyu bwana anayejipendekeza kwa Joka lisiloweza kungata machungwa machungu.
 
hii mijadala inayofanywa kwenye Television zetu na kuitwa watu mamluki wa kujitoa fahamu inanikera sana
Unakuta mtu kaacha mke na watoto nyumbani anaenda kuongea utumbo badala ya kuelimisha
Njaa mbaya sana
 
Back
Top Bottom